SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Apr 27, 2015

TAMBWE AWAGARAGAZA SIMBA SC ‘KIZIMBA CHA TFF’, WATAKIWA KUMLIPA MAMILIONI YAKE, VINGINEVYO WATAKOMA!

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI Amissi Tambwe ameshinda kesi dhidi ya klabu yake ya zamani, Simba SC juu ya mafao yake.
Simba SC ilimtema mshambuliaji huyo wa Burundi ndani ya Mkataba, lakini ikashindwa kumlipa, naye akafungua kesi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kesi hiyo jana imesikilizwa mbele ya Kamati ya Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa na Tambwe ameshinda.  
Madai ya Tambwe jumla ni dola za Kimarekani 7,000 (Sh. Milioni 14 za Tanzania), kati ya hizo 1,000 zikiwa ni mshahara wa mwezi mmoja na nyingine za kuvunjia Mkataba.
Tambwe akiwa na Wakili Frank Macha jana jioni ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam 

Simba SC wamepewa hadi Aprili 30 kuwa wamemlipa Tambwe dola 5,000 na nyingine wamalizie Mei 10, mwaka huu- na wakishindwa kufanya hivyo watakatwa fedha zote mara moja katika mapato ya mechi zao.
Tambwe aliongozana na Wakili wa klabu yake, Yanga SC, Frank Macha wakati Simba SC iliwakilishwa na Katibu wake, Stephen Ally.

MAGAZETI YA MICHEZO LEO 27 APRIL YAPO HAPA

DSC01841 DSC01842 DSC01843 DSC01844 DSC01845 DSC01846

GERRARD, LAMPARD WAPEWA 'HESHIMA YAO' ENGLAND

VIUNGO  wa zamani wa kimataifa wa England, Steven Gerrard na Frank Lampard usiku huu wamepewa tuzo kutokana na mchango wao mkubwa katika Ligi Kuu ya England.
Wawili hao wanaohamia Marekani mwishoni mwa msimu baada ya kucheza England kwa muda mrefu, wamepewa tuzo hizo na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) usiku huu.
Wote Gerrard na Lampard wanapewa heshima ya wachezaji wa 'kizazi cha dhahabu' England na kwa pamoja wameichezea timu ya taifa mechi 220 baina yao.
Steven Gerrard and Frank Lampard (right) were honoured with the merit award at the PFA awards on Sunday
Steven Gerrard na Frank Lampard (kulia) wamepewa tuzo na PFA usiku wa jana.

CHICHARITO AMSUTA HENRY, AIPIGIA MBILI REAL IKICHAPA MTU NNE LA LIGA

NYOTA ya mshambuliaji Javier Hernandez ‘Chicharito’ imeendelea kung’ara baada ya kuifungia mabao mawili Real Madrid ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya wenyeji Celta Vigo Uwanja wa Balaidos katika mchezo wa La Liga usiku wa kuamkia leo.
Real sasa inapunguza pengo la idadi ya pointi inazozidiwa na vinara wa La Liga, Barcelona hadi kubaki pointi mbili (81-79), timu zote zikiwa zimecheza mechi 33.
Wenyeji ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tisa kupitia kwa Nolito, kabla ya Real kusawazisha kupitia kwa Toni Kroos dakika ya 16 na Chicharito akafunga la pili dakika ya 24.
Hata hivyo, wenyeji wakasawazisha tena dakika nne baadaye kupiria kwa Mina, kabla ya James Rodriguez dakika ya 43 na Chicharito dakika ya 69 kuifungia Real bao la tatu na la nne.
Chicharito ndiye aliyeifungia Real bao pekee la ushindi katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, lakini Nahodha wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry akamkandia ‘kinoma’.
Alisema alishangilia kama ametwaa Kombe la Dunia- na alishangilia bila ya mtu aliyemoa pasi, Ronaldo ambaye ndiye alifanya kazi kubwa. Na Henry ambaye sasa ni mchambuzi wa Sky Sports, akasema Chicharito anayecheza kwa mkopo kutoka Manchester United, hakucheza vizuri na hana uhakika kama atapewa nafasi zaidi kikosini Real. 
Javier Hernandez scored two more important goals for Real Madrid as they look to keep up with Barcelona in the quest for the La Liga crown
Javier Hernandez akishangiia baada ya kuifunjgia Real Madrid mabao mawili jana 

HAZARD MCHEAJI BORA WA MWAKA ENGLAND


Eden Hazard with the PFA Player of the Year trophy following a ceremony in central London on Sunday
Na Anwar Binde,
Baada ya kusubiri kwa misimu miwili hatimae Eden Hazard wa Chelsea ameibuka mchezaji bora wa mwaka wa England na kutwaa tuzo ya PFA.
Hazard mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 13 na na kusaidia wafungaji (assists) 8 katika michezo 33 ya ligi kuu ya nchi hiyo na kuisaidia timu yake kushika ususkani katika msimamo wa ligi.
Naye Harry Kane mwenye umri wa miaka 21 ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora chipukizi huku naye Ji So-Yun wa Chelsea akiibuka mshindi kwa upande wa wanawake.
Hazard ambaye msimu uliopita aliibuka mshindi kwa upande wa chipukizi alikabidhiwa tuzo yake katika hoteli ya Grosvenor jijini London jana Jumapili. ” ninafuraha sana. Nataka siku moja niwe mjichezaji bora kabisa  na nilichofanya msimu huu ni kucheza vizuri na timu yangu imecheza vizuri sana” alisema Hazard baada ya kupokea tuzo hiyo. “sijui kama nastahili kushinda lakini jambo hili ni zuri kwangu. Ni jambo zuri kupigiwa kura na wachezaji kwasababu wanajua kila kitu kuhusu mpira” aliongeza mchezajia huyo.
“Tunaukalibia ubingwa labda hii ndio funguo ya kuelekea ubingwa huo,msimu uliopita tulimaliza nafasi ya tatu lakini kwa sasa ni tofauti ,tunayo nafasi na uwezo wa kuwshinda taji msimu huu”alisema hazard
Hazard alieisaidia timu yake kupata pointi zote 3 dhini ya Manchester united kwa kufunga goli pekee katika mchezo uli[igwa pale Stanford Bridge pia ametajwa katika kikosi cha wachezaji bora 11 wa kulipwa katika ligi kuu ya uingereza huku akiambatana na wachezaji wengine watano kutoka Chelsea ambao ni John Terry,Gary Cahil,Branislav Inanovic, Nemanja Matic na Diego Costa.