Mchezaji kutoka Manchester United
Ander Herrera amesema kuwa wanaisubiri Arsenal kwa nguvu zote hapo
jumatatu katika kombe la FA huku akisema kwa mkazo kuwa hawaiogopi bali
wanaiheshimu.
Mara baada ya mechi ya mwisho
kuisha na Manchester United kupata point 3 dhidi ya Newcastle jana
jumatano Herrera na kikosi chake kwa ujumla sasa nguvu zao zimebakia
kwenye mechi ijayo dhidi ya Arsenal kwenye kombe la FA tu katika uwanja
wa Old Trafford.
Herrera ambaye amekuwa katika
kiwango kizuri hasa katika siku hizi za usoni inampa picha nzuri katika
muelekeo wa mechi ijayo kukutana na washika bunduki hao na huku Kocha
wake akiwa na matarajio ya kufika fainali itakayochezwa katika uwanja wa
Wembley huko huko England mnamo May 5.
” Sasa hivi tunaangalia mbele
zaidi hasa mechi yetu ijayo dhidi ya Arsenal, sababu ndiyo nafasi nzuri
zaidi ya kutwaa kombe” Alisema hayo wakati anaongea na MUTV.
Herrera aliongezea kwa kusema
kuwa ” Inatakiwa tuwaheshimu sana Arsenal sababu wanacheza vizuri, sisi
ni Manchester United na hatuogopi, tunaenda kucheza mbele ya mashabiki
wetu na hatuna budi kushinda” alisema Herrera.
Arsenal Wenger alifanikiwa
kushinda pia katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Crystal Palace wa 2-1
huku ukiwa ni ushindi wake wa 8 katika mechi 10 za ligi.