Mar 6, 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA STUDIO ZA KISASA ZA AZAM TV TABATA LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi la jengo la Azam TV, Tabata Relini, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa studio za kisasa kampuni hiyo.

Rais Kikwete akikata utepe wa jengo la studio za Azam FC. Kulia ni Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group, wamiliki wa Azam Media Limite, ambao ndiyo wamiliki wa Azam TV, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara. 

Rais Kikwete akizundua studio za Azam TV kwa kutangaza pamoja na mzee Bakhresa kushoto
Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media Limited, Yussuf Bakhresa katika hafla hiyo  

Rais Kikwete akijibu maswali ya mtangazaji mkongwe nchini, Tido Mhando (kushoto) ambaye ni Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited 

Rais Kikwete akielekezwa jambo na wahusika ndani ya studio hizo

Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry (kulia) akiwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim na wanasiasa, Mwigulu Mchemba na Ibrahim Lipumba katika hafla hiyo
Wakuu wa Azam TV wakifurahia hotuba ya Rais Kikwete

Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Watangazaji wa Azam TV

Mkurugenzi wa Azam TV, Yussuf Bakhresa kulia akiwa na Waziri Fenella, Rais Kikwete na baba yake, mzee Bakhresa katika meza kuu

Wasanii Mwasiti na Barnaba wakitumbuiza katika shughuli hiyo      

0 maoni:

Post a Comment