Mar 6, 2015

HERRERA: TUNAIHESHIMU ARSENAL


ander HerreraNa Amplifaya Amplifaya
Mchezaji kutoka Manchester United Ander Herrera amesema kuwa wanaisubiri Arsenal kwa nguvu zote hapo jumatatu katika kombe la FA huku akisema kwa mkazo kuwa hawaiogopi bali wanaiheshimu.
Mara baada ya mechi ya mwisho kuisha na Manchester United kupata point 3 dhidi ya Newcastle jana jumatano Herrera na kikosi chake kwa ujumla sasa nguvu zao zimebakia kwenye mechi ijayo dhidi ya Arsenal kwenye kombe la FA tu katika uwanja wa Old Trafford.
Herrera ambaye amekuwa katika kiwango kizuri hasa katika siku hizi za usoni inampa picha nzuri katika muelekeo wa mechi ijayo kukutana na washika bunduki hao na huku Kocha wake akiwa na matarajio ya kufika fainali itakayochezwa katika uwanja wa Wembley huko huko England mnamo May 5.
” Sasa hivi tunaangalia mbele zaidi hasa mechi yetu ijayo dhidi ya Arsenal, sababu ndiyo nafasi nzuri zaidi ya kutwaa kombe”  Alisema hayo wakati anaongea na MUTV.
Herrera aliongezea kwa kusema kuwa ” Inatakiwa tuwaheshimu sana Arsenal sababu wanacheza vizuri, sisi ni Manchester United na hatuogopi, tunaenda kucheza mbele ya mashabiki wetu na hatuna budi kushinda” alisema Herrera.
Arsenal Wenger alifanikiwa kushinda pia katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Crystal Palace wa 2-1 huku ukiwa ni ushindi wake wa 8 katika mechi 10 za ligi.

0 maoni:

Post a Comment