SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 7, 2015

MAYWEATHER AANZA MATANUZI YA 'MZIGO' WALIOVUNA KWA KUMCHAPA PACQUIAO, AMWAGA DOLA 100,000 KWENYE PATI LA CHRIS BROWN

Floyd Mayweather (right) was in fine form on a night out in Las Vegas after his points victory on Saturday
Floyd Mayweather (kulia) akiwa kwenye pati ya sherehe ya kuzaliwa kwa mwanamuziki Chris Brown iliyofanyika usiku wa kuamkia leo klabu ya Drai's mjini Las Vegas, Marekani. 
Mayweather, who is also known as the Money Man, counts his $100 bills during his night out in Las Vegas
Mayweather, ambaye Alfajiri ya Jumapili alimpiga Manny Pacquiao kwa pointi katika pambano la utajiri mkubwa kwenye historia ya ngumi za kulipwa, haopa anahesabu dola za Kimarekani 100,000 kulipa bili usiku huo mjini Las VegasThe undefeated boxer dips his hand into his bag, held by a member of his entourage, to pull out money

Bondia huyo ambaye hajawahi kupoteza pambano katika mara zote 48 alizopanda ulingoni, hapa anatoa fedha kwenye begi lililoshikiliwa na mmoja wa wapambe wake
Mayweather holds up a wad of cash as he celebrated Chris Brown's 26th birthday at Drais nightclub
Mayweather akiwa ameshikilia fedha wakati wa kusherehekea Chris Brown kutimiza miaka 26
Mayweather talks to his invited guests at the plush Las Vegas Boulevard venue 
Mayweather akizungumza na wageni waalikwa katika pati hilo 

MOURINHO KUONGEZA MKATABA MPYA CHELSEA, ASEMA ATAKAA DARAJANI HADI ABRAMOVICH AAMUE

KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho (pichani juu) amekubali kuongeza Mkataba wa miaka miwili katika Mkataba wake wa sasa, taarifa za vyombo vya Habari Uingereza zimesema leo.
Mourinho, mwenye umri wa miaka 52, alirejea Chelsea mwaka 2013 kwa Mkataba wa miaka minne na msimu huu ameiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 na Kombe la Ligi.
Mara ya kwanza alipokuwa kazini Stamford Bridge, kuanzia mwaka 2004 hadi 2007, alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu England mwaka 2005 na 2006, sambamba na mawili ya Kombe la Ligi na moja la FA.
Mourinho tayari ndiye kocha anayelipwa zaidi England, mshahara wa jumla ya Pauni Milioni 8.4 kwa mwaka na gazeti la The Sun la Uingereza limeripoti kwamba Mkataba mpya utafanya awe analipwa Pauni Milioni 10.5 kwa mwaka.
Akizungumza baada ya Chelsea kutwaa taji la Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace Jumapili, Mourinho alisema atabaki katika klabu hiyo kwa muda mrefu atakaotaka Roman Abramovich, mmiliki wa klabu.
"Kama ambavyo nimekuwa nikisema tangu mwanzo wa msimu, nitabaki hapa kwa namna ambavyo Abramovich atataka mimi nibaki," amesema Mreno huyo. "Siku atakaponiambia ondoka, nitaondoka,”amesema.

MESSI AMFANYA KITU MBAYA GUARDIOLA CAMP NOU, APIGA MBILI BARCA IKIILAZA 3-0 BAYERN

BARCELONA imeanza vyema Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bayern Munich, Uwanja wa Camp Nou nchini Hispania.

Lionel Messi akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia Barcelona katika ushindi wa 3-0 usiku huu Uwanja wa Camp Nou
Bayern Munich sasa watatakiwa kushinda 4-0 katika mchezo wa marudiano Allinz Arena ili kutinga Fainali ambako watacheza na mshindi wa jumla kati ya Real Madird, mabingwa watetezi na Juventus. 
Lionel Messi alionyesha kiwango cha hali ya juu na kufunga mabao mawili katika mchezo huo, la kwanza dakika ya 77 na la pili dakika tatu baadaye. 
Neymar akafunga bao la tatu dakika 90 na kumtoa kinyonge Uwanja wa Camp Nou kocha wa zamani wa Barca, Pep Guardiola.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Alves, Pique, Mascherano/Bartra dk89, Alba, Busquets, Iniesta/Rafinha dk87, Rakitic/Xavi dk82, Neymar, Messi na Suarez.
Bayern Munich; Neuer, Rafinha, Boateng, Benatia, Bernat, Lahm, Schweinsteiger, Alonso, Thiago, Muller/Gotze dk79 na Lewandowski.