Uongozi
wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umesema umefika mbali katika suala
lake na beki wake, Hassan Kessy na una imani kubwa ataendelea kubaki na
kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.
Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wameanza mazungumzo na Kessy na yako katika hatua nzuri sana.
“Tuko
katika hatua nzuri sana ya mazungumzo. Tumeanza mazungumzo kipindi sasa
na tuna matumaini makubwa Kessy ataendelea kubaki Simba,” alisema
Kaburu katika mahojiano na SALEHJEMBE.
“Tunaamini Kessy tunamhitaji, naye ni kijana anayeipenda Simba. Hivyo tukifikia makubaliano, tutaingia mkataba na kuwataarifu.”
Kumekuwa na taarifa huenda Kessy ana mpango wa kujiunga na Yanga hali iliyoonyesha kuwaudhi baadhi ya mashabiki wa Simba.
Hata
hivyo kumekuwa na mgawanyiko kuhusiana na beki huyo wa kulia mwenye
uwezo wa kupiga krosi nyingi. Wengine wakisema abaki na wengine
wakikubali aende zake.