MECHI
mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinazozihusu timu za Azam na
Yanga zilizopangwa kufanyika mapema wki ijayo, zimeahirishwa.
Mechi
hizo ni kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC Jumanne ya Machi 22 Uwanja wa
Manungu, Turiani, Morogoro na Yanga SC dhidi ya Mwadui FC Jumatano ya
Machi 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwaka huu.
Sababu
za kufutwa kwa mechi hizo ni kupisha ratiba ya timu ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke akipasua katikati ya wachezaji wa Azam FC, Serge Wawa (kulia) na Farid Mussa (kushoto)
taifa
Stars itakuwa na mchezo wa kufuzu AFCON Kundi G dhidi ya Chad mjini
N’jamena Machi 25, kabla ya timu hizo kurudiana Machi 28, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Na
baada ya mechi za mwishoni mwa wiki za michuano ya klabu barani, Afrika
wachezaji wa Stars wanatarajiwa kukusanywa Jumapili kabla ya safari
Jumanne kuelekea Chad.
Yanga
SC baada ya ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR Jumamosi mjini Kigali, watarudiana
na timu hiyo ya jeshi la Rwanda Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Na
Azam FC baada ya kushinda 3-0 mjini Johannesburg, Afrika Kusini dhidi
ya wenyeji Bidvest Wits katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza
Kombe la Shirikisho Afrika, watarudiana na timu hiyo Jumapili, Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Pamoja na hayo, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kesho na mwishoni mwa wiki.
Azam FC wataikaribisha Stand United kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa
Stand United ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 22 haina nafasi
ya ubingwa na wala haimo kwenye hatari ya kushuka daraja, hivyo huo ni
mchezo ambao hauwatii ‘presha’ hata kidogo.
Lakini
Azam FC ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi zake 47 za mechi 20 katika mbio
za ubingwa dhidi ya Yanga yenye pointi 50 za mechi 21 na Simba iliyo
kileleni kwa pointi zake 54 za mechi 23 – inahitaji ushindi ili
kujiimarisha.
Simba itashuka tena dimbani Jumamosi kucheza na Coastal Union Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mar 15, 2016
TFF YASOGEZA MBELE MECHI MBILI ZA YANGA NA AZAM FC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 maoni:
Post a Comment