NIMAA.. |
Kipa wa Simba, Peter Manyika Jr ameingia kwenye shutuma nzito zinazosababisha
kushuka kwa kiwango chake ambapo inadaiwa kuwa uhusiano wa kimapenzi na mrembo
mmoja anayejulikana kwa jina la Nima ndiyo sababu.
Manyika
Jr amekuwa akionekana sehemu mbalimbali akiwa na mrembo huyo ambaye inadaiwa ni
mtoto wa mbunge, pia picha zao hutawala kwenye ukurasa wa Instagram, lakini
baada ya kugundua zimeshasambaa kwa watu mbalimbali, mrembo huyo alizifuta
picha hizo.
Inaelezwa
kuwa hali hiyo ya kushuka kiwango imewakera viongozi wengi wa Simba pamoja na
baba wa mchezaji huyo Manyika Peter ambaye alimuweka chini mwanaye na kumkanya.
Akizungumza kuhusiana na hilo, kipa huyo mwenye umri wa
miaka 19, alisema: “Huyo dada ni rafiki yangu wa kawaida na wala sina uhusiano
naye wa kimapenzi. Tatizo letu
Watanzania tukiona jambo basi tunalikuza kupita kiasi.”
Kuhusu
picha wakiwa pamoja alisema: “Kweli tulipiga picha lakini hiyo siyo sababu ya
kusema kuwa ni mpenzi wangu.”
Alipoulizwa
kuhusu kukanywa na baba yake juu ya jambo hilo, alisema: “Kweli baba
aliniuliza, nilimueleza ukweli kuwa hakuna kitu kama hicho.”
Alipotafutwa baba mzazi wa kipa huyo, Manyika Peter ambaye alikuwa na
haya ya kusema: “Sitaki mwanangu apotee, nilipata taarifa hizo na nikamuita na
kuzungumza naye kwa kina lakini aliniambia kuwa yule ni rafiki yake, hata hivyo
nikiwa kama mzazi nilimkanya na kumpa mwongozo wa nini anatakiwa kukifanya
kufika mbali kisoka.
“Kama
alidanganya kuwa hayupo na mwanamke huyo, hilo silijui kwa sababu hivi sasa
siko naye nyumbani, muda mwingi yupo na timu yake ya Simba lakini
nitalifuatilia suala hilo.”
SALEHJEMBE ilimtafuta Nima ambaye inaelezwa ndiye aliyekuwa mrembo katika
wimbo wa Mbagala wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, naye alifunguka: “Manyika
siyo mpenzi wangu ila ni rafiki yangu, mimi najua ana mtu wake lakini siyo
mimi, hiyo video niliyokuwa nimeiweka Instagram tulipiga tukiwa tunatokea
mazoezi ya Simba na hata siku hiyo mchumba wa Manyika alikuwa anajua kuwa nipo
naye.”
0 maoni:
Post a Comment