Kocha wa klabu ya washika
mitutu wa London Arsenal Arsene Wenger ameibuka na kumtetea kiungo
mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Uingereza Jack Wilshere,
kuwa kiungo huyo sio mvutaji wa sigara licha ya picha zake kusambaa
katika mitandao ya kijamii akiwa ameshika sigara jijini London.
Wenger amesema mchezaji huyo
inabidi aangalie maisha yake ya baadae katika mchezo wa soka kwani bado
ni kijana mdogo mwenye uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu la kimataifa,
lakini matukio yake ya ajabu yanaweza kumfanya ashindwe kufanya vizuri
siku za hapo baadae.
Ni mara ya tatu sasa mchezaji
huyo kupigwa picha akiwa anavuta sigara katika maeneo mbalimbali ya
starehe na picha zake kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Lakini wenger amekanusha madai
kuwa katika klabu ya Arsenal kuna tatizo kubwa la wachezaji wake kuvuta
sigara wakiongozwa na kiungo Wilshere.
“Hakuna utamaduni wa uvutaji
sigara katika kikosi changu, niliongea na Jack kuhusu swala picha zake
zinazoonyesha akivuta na kusema yeye sio mvutaji, lakini inabidi
aangalie maisha yake,” alisema Wenger.
0 maoni:
Post a Comment