SIMBA inaanza mazoezi leo jioni
jijini Tanga kujiandaa na mechi ya keshokutwa dhidi ya Coastal Union
itakayopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Afisa habari wa klabu hiyo,
Humphrey Nyasio amezungumza na mtandao huu na kueleza kuwa kikosi kipo
salama na wapo tayari kwa mechi hiyo.
Nyasio amefurahishwa na jinsi
mashabiki walivyowapokea kwa furaha jijini Tanga na wamejipanga kuwapa
furaha zaidi kwa kushinda kipute hicho.
Hata hivyo, Afisa habari huyo
ameongeza kuwa beki wa kati Joesph Owino amebaki Dar es salaam
akiendelea kufanya mazoezi mepesi na kikosi cha Simba B.
0 maoni:
Post a Comment