Feb 6, 2015

KIFARU ATAMBA KUWAFUNGA YANGA JUMAPILI

HIKI NDIYO KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KILICHOIFUNGA YANGA KWA MABAO 2-0. ATAKOSEKANA KESSY AMBAYE AMEJIUNGA NA SIMBA.

Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ametamba kwamba wanakuja jijini Dar es Salaam kuendeleza ubabe wao kwa Yanga.


Yanga inashuka dimbani Uwanja wa Taifa jijini Dar keshokutwa Jumapili kuwakaribisha Mtibwa Sugar ambao waliwatwanga kwa mabao 2-0 katika mechi ya mzunguko wa Ligi Kuu Bara.

Kifaru amesema wana nafasi kubwa ya kuwafunga Yanga katika mechi ya pili kama walivyofanya kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

“Tuliwafunga wakapoteana, tunakuja huko Dar es Salaam na tunatarajia kufika Dar es Salaam, kesho.

“Sisi tumejiandaa sana na hakuna ishu ya mbwembwe au vinginevyo, nakuhakikisha njoo uone tunavyowamaliza Yanga hiyo Jumapili,” alisema Kifaru.


Msemaji huyo ametamba kwamba baada ya kikosi chao kupunguza kasi, kinataka kuanza kuamsha moto katika mechi dhidi ya Yanga.
USIKOSE KUFUATILIA BLOG HII WWW.HAJIBALOU.BLOGSPOT.COM KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

0 maoni:

Post a Comment