Na Haji balou
Mchezo kati ya Sido fc dhidi ya Wakaanga sumu umemalizika katika uwanja wa shule ya msingi muungano kwa sare ya goli 2-2.
Katika kipindi cha kwanza magoli ya Sido fc walifungwa namo dakika ya 7 na 15 yote yakipachikwa na Haikosi Mpwate na goli la Wakaanga Sumu likufungwa na Bocho Shabani dakika ya 24.
Katika kupindi cha pili Wakaanga Sumu walisawazisha goli dakika ya 70 goli lililofungwa na Stamili Abduli
Mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa Wakaanga sumu 2-2 Sido fc.
Nimezungumza na kamisaa wa mashindano ya ligi Shamte Mohamedi Shamte kuzungumzia sakata la mechi mbili za juzi kati ya Kubota fc Vs Kubota fc na Jana Z fc Vs Kigamboni fc kutokumalizika uongozi uliamua haya.
Timu zote ambazo zimeanzisha fujo katika mechi ya Jana Na juzii zimefungiwa katika mashindano hayo ya Kombe la mbuzi timu hizo ni Vijuso fc Na Zfc.