May 18, 2016

CANNAVARO AMEFUNGUKA KUHUSU YEYE KUCHEZA TAIFA STARS KAMA ATAITWA NA MKWASA

Na Haji balou
Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Nadir Haroub Cannavaro kutangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa ya Tanzania
kutokana na kuvuliwa unahodha bila kupewa taarifa rasmi, tuliwahi kusikia kocha wa Taifa Stars Boniface Mkwasa akisema kuwa bado Cannavaro yupo katika mipango yake.

Cannavaro amefunguka haya kuhusu yeye kucheza Taifa Stars kama kocha Mkwasa akimuita katika kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza na Kenya May 29 “Kwanza ieleweke sina tatizo na kocha Mkwasa hata kidogo ni kocha ambaye napenda kufanya nae kazai
akiniita nitamtafuta tutakaa chini kushauriana kiutu uzima halafu nitamwambia mimi naomba tu kwa
sasa niendelee kupumzika kuchezea Stars”

0 maoni:

Post a Comment