May 17, 2016

MASHABIKI WAANZISHA FUJO ZFC IKILALA 3-0

Na Haji balou
Mashindano ya kombe la mbuzi vijana yameendelea tena hii Leo kwa mchezo mmoja uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi muungano baina ya Zfc dhidi ya Kigamboni fc mchezo ambao hauku malizika kwa dakika 90.

Mpaka mchezo unavunjika Kigamboni fc ilikuwa inaongoza goli 3-0 magoli yaliyo fungwa Na Uwesu Mbala katika dakika ya 35, 65 Na 80.

Vurugu kubwa zilizo anzishwa Na mashabiki wa Zfc katika dakika za mwishoni  mwa mchezo wakidai mwamuzi wa Mchezo huo anawapendelea wapinzani wao.

0 maoni:

Post a Comment