May 16, 2016

VIJUSO FC YAICHAPA KUBOTA MECHI YAVUNJIKA

Image result for SPORTS
Na Haji balou
Mashindano  ya ligi ya Mbuzi vijana Cup yameendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa Shule ya Msingi Muungano kati ya Vijuso fc dhidi ya Kubota fc.

 Mchezo huo ambao haukumalizika baada ya kutokea fujo katika dakika ya 84, mpaka mchezo huo unavunjika tayari  Vijuso fc walikuwa wanaongoza goli 4-1 dhidi ya Kubota fc.

Baada ya mchezo huo kuvunjika kocha wa Kubota fc Ramadhani Ngazulu alitoa lawama zake kwa refa wa mchezo huo kwa kudai amewapendelea kwa kiasi kikubwa wapinzani wao na yeye ndio chanzo cha kuvunjika kwa mechi hiyo.

Lakini juhudi za kuwapata viongozi wa ligi hiyo hazi kufanikiwa na watatoa maelezo zaidi pale ambapo tutawapata pia watafafanua kanuni za ligi kuhusu mechi ikivujika hatua gani ambazo zinafuatwa.

0 maoni:

Post a Comment