Na Haji balou
KLABU ya Azam FC itamkosa kiungo
Farid Mussa Malik (pichani kushoto)
katika wa mchezo wa marudiano
hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance nchini Tunis wiki ijayo.
Baada ya kufunga bao la kusawazisha katika ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Farid sasa anajiandaa kwa safari ya majaribio Ulaya.
Bado wakala wa Farid hajaweka wazi basi anampeleka wapi kijana huyo, lakini inaelezwa atampeleka au
Ubelgiji, Scotland au Hispania ambako kote kuna timu za kumjaribu.