Na Haji balou
Mkuu wa Kitengo cha Habari na
Mawasiliano cha Simba, Haji Manara
amepata ajali mbaya.
Manara amepata ajali baada ya
kuchomoka tokea ndani ya Bajaj na
kuanguka barabarani.
Kuanguka huko kumesababisha Manara kupata majeraha sehemu za mkononi na usoni hukua kisema amenusurika kifo kutokana na ajali hiyo.
Manara ameelezea tukio hilo:
“Nilikuwa nakwenda kumuona shangazi yangu, nikaamua kuacha gari nichukue Bajaj. Sasa tukio hilo limetokea hivi; Bajaj ilipiga tuta wakati nikiwa sijashika, ndiyo nikachomoka.
“Hakika nimeumia na nina maumivu
makubwa sana, lakini namshukuru Mungu kwa kuwa ilikuwa ni ajali mbaya sana hasa kama kungekuwa na gari nyuma.”
HARAKATI ZA SOKA INATOA POLE KWA MANARA NA KUMUOMBEA APATE NAFUU MAPEMA NA KUPONA KABISA.
0 maoni:
Post a Comment