SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 1, 2015

TAZAMA WACHEZAJI WA YANGA WALIVYOSHOO LOVE TUNISIA


IMG-20150430-WA0102
 Kutoka kulia, Mkuu wa idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, Jerryson Tetege, Amissi Tambwe na Mbuyu Twite wakishoo ‘Love’ nchini Tunisia baada ya kutua wakitokea Dubai.
Yanga na Etoile du Sahel zitachuana jumamosi kuanzia saa 3:00 kwa saa za Tanzania katika mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho.
Mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1 uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Cheki Mjomba Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani walivyotupia kofia kisela

BEKI MBELGIJI AFARIKI DUNIA

IMG_20150430_204737
Beki wa klabu ya Sporting Lekeren ya nchini Ubeligiji,Gregory Mertens amefariki dunia leo siku tatu tangu aanguke uwanjani wakati akikichezea kikosi cha akiba cha timu hiyo dhidi ya Genk.
Mchezaji huyo aliyewahi kuiwakilisha ubelgiji katika timu chini ya miaka 21,alianguka kufuatia kusumbuliwa na matatizo ya moyo.
Beki huyo ,24, alianguka uwanjani dakika 15 baada ya mechi hiyo kuanza na hivyo kupatiwa huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi .
Msemaji wa Lokeren Herman Van De Putte amesema kuwa ,hili ni pigo kwa wachezaji,familia yake, mashabiki na familia ya soka kwa ujumla
Taarifa kutoka katika klabu hiyo inasema ” Licha ya matibabu mazuri yaliyotolewa na madaktari wa timu,madaktari wa hospitali lakini ilionekana hali ilizidi kuwa mbaya zaidi “
Wachezaji mbalimbali ,Romeu Lukaku,Fabrice Muamba,Jelle Vossen na wengine wengi wameandika katika akaunti zao za twita,instagram ujumbe wa kumuombea mchezaji huyo kwa mungu.

YANGA SC ‘WACHOMESHWA’ SAA MBILI UWANJA NDEGE TUNIS, WAPEWA BASI KUSAFIRI KILIMOTA 140 KUWAFUATA ETOILE ‘KIJIJINI KWAO’

Na Prince Akbar, TUNIS
MSAFARA wa Yanga SC imetua salama mjini Tunis na baada ya kugandishwa kwa saa zaidi ya mbili Uwanja wa Tunis, imeanza safari ya basi kuelekea mji mdogo wa Sousse kwa wenyeji wao, Etoile du Sahel umbali wa kilomita 140.
Yanga SC iliondoka usiku wa jana kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudaino hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.
Wachezaji walio safarini na Yanga SC ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’, mabeki Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
Wachezaji wa Yanga SC wakiwa Uwanja wa Ndege wa Tunis, ambako waligandishwa saa zaidi ya mbili kusubiri basi la kuwapeleka mji mdogo wa Sousse 


Viungo ni Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’, wakati washambuliaji ni Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva. 
Yanga SC inahitaji ushindi wa ugenini au sare kuanzia mabao 2-2 kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Etoile katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki iliyopita.

JOHN TERRY SASA NDIYE BEKI MFUNGAJI BORA KIHISTORIA LIGI KUU ENGLAND

NAHODHA wa Chelsea, John Terry sasa ndiye mchezaji wa nafasi za ulinzi aliyefunga mabao mengi zaidi Ligi Kuu England baada ya Jumatano kufunga katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Leicester.
Nahodha huyo wa zamani wa England alimtungua kipa Kasper Schmeichel Uwanja wa King Power jana kufunga bale la 38 tangu aanze kucheza Ligi Kuu.
Bao hilo linamfanya Terry, ambaye amefunga kila msimu katika misimu 15 iliyopita Ligi Kuu kumfikia beki wa zamani wa Everton, David Unsworth. It was Terry's 38th Premier League goal during his career equalling the record for a defender

MABEKI WATANO WAKALI WA MABAO KIHISTORIA ENGLAND 

John Terry -  Mabao 38
David Unsworth - Mabao 38
Ian Harte - Mabao 28
Leighton Baines - Mabao 26
William Gallas - Mabao 25
Kwa kuwa Terry bado yuko vizuri na anaendelea kucheza Chelsea kuna matumaini makubwa atafunga tena na kuwa beki mfungaji bora katika historia ya Ligi Kuu England.
Unsworth, ambaye aliichezea timu ya taifa ya England pia, alikuwa mkali kwa guu lake la kushoto katika kufunga.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 41 sasa, ambaye mabao yake mengi alifunga akiwa na klabu hiyo ya Merseyside, Everton, alikuwa mtaalamu wa kupiga mikwaju ya penalti na mipira ya adhabu na Terry anafuata nyayo zake vizuri.