NAHODHA
wa Chelsea, John Terry sasa ndiye mchezaji wa nafasi za ulinzi
aliyefunga mabao mengi zaidi Ligi Kuu England baada ya Jumatano kufunga
katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Leicester.
Nahodha
huyo wa zamani wa England alimtungua kipa Kasper Schmeichel Uwanja wa
King Power jana kufunga bale la 38 tangu aanze kucheza Ligi Kuu.
Bao
hilo linamfanya Terry, ambaye amefunga kila msimu katika misimu 15
iliyopita Ligi Kuu kumfikia beki wa zamani wa Everton, David Unsworth.
Terry akishangilia baada ya kufunga bao lake la 38 katika Ligi Kuu England na kuwa beki mfungaji bora kihistoria
MABEKI WATANO WAKALI WA MABAO KIHISTORIA ENGLAND
John Terry - Mabao 38
David Unsworth - Mabao 38
Ian Harte - Mabao 28
Leighton Baines - Mabao 26
William Gallas - Mabao 25
Kwa
kuwa Terry bado yuko vizuri na anaendelea kucheza Chelsea kuna
matumaini makubwa atafunga tena na kuwa beki mfungaji bora katika
historia ya Ligi Kuu England.
Unsworth, ambaye aliichezea timu ya taifa ya England pia, alikuwa mkali kwa guu lake la kushoto katika kufunga.
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 41 sasa, ambaye mabao yake mengi alifunga
akiwa na klabu hiyo ya Merseyside, Everton, alikuwa mtaalamu wa kupiga
mikwaju ya penalti na mipira ya adhabu na Terry anafuata nyayo zake
vizuri.
0 maoni:
Post a Comment