Apr 29, 2015

VAN PERSIE ‘AFUFUKA’, APIGA MBILI MAN UNITED IKISHINDA 4-1 ENGLAND

MSHAMBULIAJI Robin van Persie usiku huu amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 wa  U21 ya Manchester United dhidi ya vijana wenzao wa Fulham Uwanja wa Craven Cottage.
Van Persie ambaye amekuwa nje ya Uwanja tangu Februari kutokana na majeruhi, alifunga mabao hayo katika dakika za 13 na 80, huku mabao mengine ya United yakifungwa na Joe Rothwell dakika ya 20 na 43.
Mholanzi huyo, Van Persie alirejea uwanjani kikosi cha kwanza cha United Jumapili timu hiyo ikifungwa 3-0 na Everton katika LIgi Kuu ya England.
Kikosi cha Fulham kilikuwa: Norman, Donnelly, Buatu, Baba, Sheckleford, Mesca, Edun/de la Torre dk67, Smile, Evans, Plumain, Redford/Humphreys dk60.
Manchester United: Lindegaard, Love, Blackett, Thorpe, Kellett, Rothwell/Willock dk81, Goss/Fletcher dk88, Grimshaw, Pereira, Van Persie/Weir dk81 na Januzaj.
Van Persie made an appearance for Manchester United Under 21s away at Fulham on Tuesday night
Van Persie akipongezwa na wenzake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 wa U21 ya Manchester United dhidi ya Fulham usiku wa Jumanne

0 maoni:

Post a Comment