Apr 29, 2015

MESSI, SUAREZ KILA MMOJA APIGA MBILI BARCA IKIUA 6-0

TIMU ya Barcelona imezidi kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu Hispania, La LIga baada ya leo kuifunga Getafe mabao 6-0 Uwanja wa Nou Camp na sasa inawazidi Real Madrid kwa pointi tanio.
Lionel Messi aliwafungia wenyeji bao la kwanza dakika ya 10 kwa mkwajunwa penalti baada ya Luis Suarez kuangushwa. 
Luis Suarez akaifungia Barca bao la pili dakika ya 25, kabla ya Neymar Jnr kufunga la tatu dakika tatu baadaye na hilo kuwa bao la 100 kwa timu yake hiyo msimu huu.
Xavi akaifungia bao la nne timu ya Luis Enrique dakika ya 30, kabla ya Suarez kufunga lake la pili katika mchezo huo na la tano kwa Barca dakika ya 40 na Messi akafunga bao lake la 48 msimu huu la sita kwa timu yake dakika mbili tu baada ya kuanza kipindi cha pili.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Bravo, Alves/Montoya dk68, Bartra, Mathieu, Adriano, Busquets, Xavi/Pedro dk59, Rafinha, Suárez, Messi na Neymar.
Getafe: Guaita, Alexis, Lago, Velazquez, Lacen, Arroyo, Pedro Leon/Escudero dk76, Baba, Juan Rodriguez/Felip dk65, Freddy na Emi.
Neymar celebrates with Lionel Messi after giving Barcelona a 3-0 lead at the Nou Camp on Tuesday night
Neymar akisherehekea na Lionel Messi baada ya kuifungia Barcelona bao la tatu usiku huu

0 maoni:

Post a Comment