KOCHA
wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ametaja sababu za
wakati wote kumuona Cristiano Ronaldo yuko juu ya Lionel Messi wakati
anazungumza na John Parrott wakicheza pool table, maarufu pia kama
snooker.
Kocha huyo
mwenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya soka ya Uingereza
amezungumza na Parrott na mtangazaji Hazel Irvine katika mahojiano
maalum ya BBC ya michuano ya Ubingwa wa Dunia Crucible.
Ferguson
amesema wakati wote anaulizwa nani ni mchezaji bora duniani?, kabla ya
kufafanua kwa nini humchagua mchezaji wake wa zamani United dhidi ya
nyota wa Barcelona.
Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson (kushoto) akizungumza na John Parrott kwenye meza ya snooker
Ferguson anaamini Cristiano Ronaldo ni mzuri zaidi ya Lionel Messi kwa sababu anaweza kufunga akiwa na timu yoyote
"Watu wengi kwa urahisi tu wanasema Messi na huwezi kukataa maoni yao,"alimuambia bingwa wa mwaka 1991 wa Snooker duniani.
"Ronaldo
anaweza kuchezea Millwall, QPR, Doncaster Rovers, (timu moja) yoyote,
na akafunga hat-trick. Sina uhakika kama Messi anaweza kufanya hivyo. Ronaldo yuko fiti mno, ana kasi, mzuri wa kurukia mipira ya juu kupiga kichwa na mkali.
"Nafikiri Messi ni mchezaji wa Barcelona,' amesema.
Kocha
huyo wa zamani wa United wakati wote amekuwa na uhusiano mzuri na nyota
huyo anayecheza Real Madrid kwa sasa tangu aondoke Old Trafford, na
Ferguson anampa heshima Mreno huyo sambamba na Ryan Giggs na Paul
Scholes kama wachezaji bora duniani aliowahi kuwafundisha.
0 maoni:
Post a Comment