May 5, 2015

MAJAJI WALIMPA USHINDI PACQUIAO, 'MC' AKAMTANGAZA MAYWEATHER AMESHINDA, USHAHIDI HUU HAPA!

UTATA mwingine umeibuka kutoka 'Pambano la Karne' baina ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililofanyika Alfajiri ya juzi ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas, Marekani. 
Karatasi ya kuandika matokeo raundi kwa raundi ya majaji wote watatu, Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti inaonyesha bondia aliyekuwa kona nyekundu, Pacquiao ndiye aliyeshinda pambano, wakati mtangazaji 'MC' wa pambano akamtangaza bondia wa kona ya bluu, Mayweather ndiye mshindi.
Inaonekana kama majaji walijichanganya katika kutumia karatasi hizo na pointi za Mmarekani, Mayweather 'Mtu Pesa' wakizihamishia kwa Mfilipino, Pacquiao, lakini kwa nini iwe kwa majaji wote watatu? 
Hii inazidi kuzua shaka kwamba inawezekana Mayweather alipewa ushindi kimakosa- bali kwa mujibu wa karatasi za majaji mshindi ni Pac Man aliyekuwa anatokea kona nyekundu. 
Karatasi halisi za majaji Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti zinavyoonyesha na picha inawaonyesha mabondia hao katika kona zao, Mayweather ya bluu (kushoto) na Pacquiao nyekundu (kulia).

0 maoni:

Post a Comment