May 6, 2015

TEVEZ AWAONDOA ‘VICHWA CHINI’ REAL TURIN, JUVE YANG’ARA NYUMBANI 2-1

REAL Madrid wameanza vibaya Nusu Fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji Juventus Uwanja wa Juventus mjini Turin usiku wa jana.
Real sasa itahitaji ushindi wa 1-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Madrid ili kuking’oa ‘Kibibi Kizee cha Turin’ katika michuano hiyo na kwenda kutetea taji lake.
Alvaro Morata alianza kuwafungia Juventus dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 27.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amefikisha mabao 76 na sasa ndiye anayeongoza kwa kufunga katika historia ya mashindano hayo.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester zote, United na City, Muargentina Carlos Tevez aliifungia bao la ushindi Juve kwa penalti dakika ya 57 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Dani Carvajal.
Tevez wheels away in celebration after restoring the Old Lady's lead from the penalty spot against the current Champions League holders
Tevez akishangilia baada ya kuifungia bao la uishindi Juventus dhidi ya mabingwa watetezi, Real Madrid usiku wa jana

0 maoni:

Post a Comment