BONDIA
Manny Pacquiao anaweza kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa
kutoorodhesha maumivu yake ya bega kwenye fomu maalum ya taarifa za
bondia kabla ya pambano lake na Floyd Mayweather alilopoteza kwa pointi.
Pacquiao
anaweza kuwa nje ya ulingo hadi mwaka mmoja wakati anajiandaa kwenda
kufanyiwa upasuaji wa bega baada ya kuumia mazoezi akijiandaa na pambano
hilo.
Lakini nyota
huyo wa Ufilipino anaweza kuchukuliwa hatua kwa kusaini fomu ya maelezo
muhimu ya bondia kabla ya pambano, bila kuorodhesha maumivu ya bega
lake.
+9
Manny Pacquiao pichani jana akiwa amefungwa mkono wakati akijiandaa kwenda kufanyiwa upasuaji
+9
Fomu ya maelezo muhimu ya Pacquiao kabla ya pambano haikuorodhesha maumivu ya bega lake
BIN ZUBEIRY imeipata nakala ya fomu ya maelezo muhimu ya bondia kabla ya pambano, ambayo inaonyesha kwamba Pacquiao alitumia dawa kadhaa za maumivu.
Aidha,
neno hapa likiwa linafuatia limepigiwa mstari baada ya swali; ‘Ulikuwa
una maumivu yoyote kwenye mabega yako, chini ya mabega, au mikononi
ambayo yanahitaji vipimo vya uthibitisho wa kupona?’
Kwa
kusaini fomu hiyo, wote Pacquiao na mshauri wake Michael Koncz wanaweza
kuchukuliwa hatua kwa sababu, mwishoni kuna maelezo yasemamo; "Maelezo
ya hapo juu ni kweli na sahihi nikiwa na akili zangu timamu,".
Adhabu
ya kosa hilo kwa kawaida huwa ni kufungwa jela kati ya mwaka mmoja na
minne na kutozwa faini hadi dola za Kimarekani 5,000 (Sh. Milioni 20). Pacquiao anaweza pia kutozwa faini na kufungiwa na Kamisheni ya Michezo Nevada.
Mwenyekiti
wa Kamisheni, Francisco Aguilar amesema kwamba ofisi ya Mwanasheria
Mkuu itachunguza kwa nini maumivu hayo hayakuorodheshwa.
"Na tutafanya majadiliano fulani. Kwa sababu Kamisheni inapaswa kupata maelezo ya kila wakati ya bondia. Tiba aliyopata iliorodheshwa kwenye fomu, lakini si ya maumivu halisi. Hili
si pambano letu la kwanza. Hii ni biashara yetu. Kuna utaratibu, na
unapojaribu kukiuka utaratibu, hatuwezi kufanya kazi na wewe,"amesema.
+9
Floyd Mayweather alipigana kwa ustadi wa hali ya juu dhidi ya mpinzani wake huyo mjini Las Vegas
0 maoni:
Post a Comment