Na Haji balou
Ligi ya Mbuzi Vijana Cup wilaya ya Liwale imeendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano kwa Kombaini fc kuibuka na ushidi wa 3-1 dhidi ya Likongowele fc.
Magoli ya Kombaini fc yamefungwa na Mpilipili katika dakika ya 18 Sudi mbwana katika dakika ya 45 goli la mwisho limefungwa na zuberi zuberi dakika ya 65 goli la kufutia machozi kwa upande wa Likongowele fc limefungwa na Faraji Manyai katika dakika ya 25.
Baada ya mchezo kumalizika kapteni wa Likongowele Ramadhani mmango amesema kuwa kwa upande wao hawakucheza vizuri na timu yao ilikosa maelewano hasa eneo la kiungo.
Pia kocha wa Kombaini Haji mkutuma alisema mchezo ulikuwa mzuri lakini refa hakuwa katika upande wao ingawa wameibuka na ushindi wa goli 3-1 na malengo yao ni kushika nafasi ya kwanza katika kundi lao ili kusonga mbele katika mashindano.