SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Sep 1, 2016

KIUNGO MTANZANIA APATA TIMU AFRIKA KUSINI

Na Haji balou
KIUNGO wa zamani wa
Simba SC na Azam FC,
Abdulhalim Humud ‘Gaucho’
amejiunga na klabu ya Real
Kings FC ya Ligi Daraja la
Kwanza Afrika Kusini.

Humud ambaye msimu
uliopita alichezea Coastal
Union ya Tanga iliyoshuka
daraja kutoka Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara,
amesaini mkataba wa
mwaka mmoja kujiunga na
timu ya Durban, Kwazulu-
Natal.

Real Kings walipanda Ligi
Daraja la Kwanza mwaka
huu na wakafanikiwa kufika
fainali ya ligi ya ABC
Motsepe League.

Wakala aliyefanikisha
Humud kusaini Real Kings,
amesema leo kwa simu
kutoka Durban kwamba ana
matumaini mchezaji huyo
atafanya vizuri Afrika
Kusini.

Jul 15, 2016

JORDAN IBE AIHAMA LIVERPOOL

Na Haji balou
Timu ya Bournemouth imekamilisha usajili wa winga wa Liverpool Jordan Ibe kwa Ada ya Euro million 15.

Ibe amesaini mkataba wa miaka minne ya kuitumikia Timu hiyo inayotumia uwanja wa Vitality.

LUIS NANI ASAINI TIMU HII HAPA LA LIGA

Na Haji balou
Mchezaji wa zamani wa Manchester United ya Uingereza Luis Nani amesaini mkataba mkataba wa miaka mitatu ya kuitumikia Valencià ya Hispània.

Nani amesajiliwa kwa Euro million 8.5 akitokea katika klabu ya Fenerbahce ya uturuki ambayo aliisaidia kushika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Besiktas.

Jul 14, 2016

MHISPANIA WA AZAM FC ATAJA TOFAUTI YA MAKIPA WA HISPANIA NA TANZANIA

Na Haji Balou
KOCHA Mkuu wa makipa wa Klabu
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam
FC, Jose Garcia, amesema kuwa makipa
aliowakuta ndani ya timu hiyo wapo
vizuri.

Kocha huyo hakusita kuelezea utofauti
wa makipa kutoka Tanzania na Hispania
mara baada ya kuwaona wa Azam FC,
ambapo alisema magolikipa wa hapa
wana nguvu sana lakini wanakosa mbinu.

“Watanzania wana nguvu sana, ila
wanakosa mbinu, lakini kwa upande wa
kule Hispania wako vizuri zaidi na
wanazo mbinu, na hicho ambacho
nimeongea na wenzangu ili tuweze
kukifanyia kazi,” alimalizia kocha huyo
mwenye umbile kubwa na mrefu
atayesaidiana majukumu hayo na Idd
Abubakar.

Ukiondoa makipa wa Azam FC, Aishi
Manula, Mwadini Ally na Metacha Mnata
aliyepandishwa kutoka timu ya vijana na
Kauju Agustino wa Azam B wanaendelea
kufanya maandalizi ya msimu mpya, kuna
makipa wengine wawili wa kigeni
wanawania nafasi moja ya kusajiliwa,
Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Juan
Jesus Gonzalez (Hispania).

CHANZO WWW.AZAMFC.COM

WACHEZAJI KUMI WALIO KAMILISHA USAJILI LIGI KUU BARA

Na Haji Balou
AKlabu za Ligi Kuu Bara kwa ajili ya msimu
mpya ligi kuu bara 2016/2017, kwa kuboresha
baadhi ya maeneo yenye mapungufu na
kuyaongezea nguvu.

Atupele Green (ametoka Ndanda kwenda
JKT Ruvu)
Mfungaji bora wa kombe la shirikisho FA na
klabu ya Ndanda kwa msimu uliomalizika
amemwaga wino kuitumikia JKT Ruvu kwa
msimu mpya, kwa uwezo wake mkubwa wa
kufumania nyavu atakua msaada mkubwa
kwa JKT Ruvu.

Mohamed Mkopi (ametoka Prisons kwenda
Mbeya City)
Moja ya matatatizo msimu uliomalizika
Mbeya city ni ubutu wa safu ya ushambuliji,
Mkopi ni mzuri kwenye kufunga na
kutengeneza nafasi za kufunga kwa wenzake,
kwa usajili huu Mbeya City watafaidika nao.

Hassan Kessy (ametoka Simba kwenda
Yanga)
Amesaini kuitumikia Yanga kwa miaka miwili,
usajili huu ni bora kwa Yanga sababu upande
wa beki ya kulia Yanga imekua aina mpinzani
kwa muda mrefu Juma Abduli amekuwa
akitawala, ujio wa Kessy Yanga utaleta
upinzani sahihi kwenye nafasi hiyo.

Shiza Kichuya (ametoka Mtibwa kwenda
Simba)
Mmoja wa viungo bora msimu uliomalizika
akiwa Mtibwa, amejiunga na Simba kwa ajili
ya msimu mpya, uwezo wake mkubwa
uwanjani utakuwa faida kwa Simba hapa ni
kama Simba imepiga bao kwa usajili wa
Kichuya.

Muzamili Yassin (ametoka Mtibwa kwenda
Simba)
Hakuna shaka na uwezo wa Muzamili ni
mmoja wa viungo bora chipukizi kwa msimu
uliomalizika, huu ni moja ya usajili bora
kwenda Simba kutokana na uwezo mkubwa
wa Muzamili kutengeneza nafasi za kufunga
kwa wenzake na ndicho kitu Simba walikuwa
wamekosa kwa kipindi kirefu tangu kuondoka
kwa Boban.

Edo Christopher (ametoka Toto kwenda
Kagera)
Kagera wanazidi kujiimarisha kwa ajili ya
msimu mpya baada ya kuponea kushuka
daraja msimu uliomalizika, ujio wa Edo
kwenye eneo la ushambuliaji utaongeza
chachu kutokana na uwezo wake wa kufunga
na uzoefu kwenye ligi kuu bara.
Juma Mahadhi (ametoka Coastal kwenda
Yanga)
Ni usajili bora kufanywa na Yanga kwa msimu
ujao, uwezo wake mkubwa kwenye mechi
dhidi ya Mazembe kwenye kombe la
shirikisho umeleta faraja kubwa kwa wapenzi
wa Yanga pamoja na wanachama.

Aziz Gilla (ametoka Mgambo JKT kwenda
JKT Ruvu)
JKT Ruvu wanajiimarisha kwenye maeneo
mbali mbali kwa ajili ya msimu mpya, ujio wa
winga mpya Aziz Gilla utakuwa msaada
kwenye timu yao hasa nidhamu yake na
uhamasishaji wa wenzake.

Vicent Andrew (ametoka Mtibwa kwenda
Yanga)
Amesaini Yanga kwa mkataba wa miaka
miwili licha ya ugumu wa namba kwenye
eneo analo cheza kwa sababu imejaza watu
wenye uzoefu lakini ni moja ya usajili bora
sababu ana uwezo wa kucheza namba zaidi
ya tatu uwanjani.

Dany Mrwanda (ametoka Majimaji kwenda
Kagera)
Kikubwa ni uzoefu wake kwenye ligi utakuwa
msaada mkubwa kwa Kagera timu ambayo
inajiimarisha kwa msimu mpya.

Jul 7, 2016

VALDEZ ASAINI TIMU HII HAPA ENGLAND

Na Haji balou
Kipa wa zamani wa Fc barcelona Na Manchester united Victor Valdez amesaini mkataba wa miaka miwili Na klabu ya Middlesbrough ya nchini England.

Valdez mwenye umri wa miaka 34 amekuwa Na wakati mgumu tangu atue Manchester united akitokea  Barcelona baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika klabu hiyo.

Kupitia account yake ya Twitter Valdez aliandika hivi  “Very Proud to be part of Middlesbrough.

“A new challenge for me from today!”.

MANYIKA JR AZUNGUMZIA SKENDO YA MAPENZI INAYOMKABILI

Na Haji balou
Mchezaji wa timu ya Simba Peter manyika Jr amesema yeye ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu isipokuwa mashabiki wengi wanamsema kutokana Na jinsi wanavyo mwona.

Manyika alisema hayo alipokuwa akihojiwa Na Sauda mwilima kupitia kipindi cha Mcheza kwao kinachorushwa na channeli ya Star Tv.

Pia alipoulizwa kuhusu skendo za mapenzi zinazo mkabili Manyika alisema kuwa "Siku zote ukiwa maarufu watu watazungumzia sana mahusiano yako kutokana Na aina ya mpenzi ambaye unatoka nae".

"Kiukweli Mimi nipo Na mpenzi wangu huyu huyu ambae ninae kwa miaka miwili sasa Ila kwakuwa watu wanaongea waache waongee" alisema Manyika Jr.

Mashabiki walianza kumtuhumu Manyika Jr anashuka kiwango baada ya kugundua anatoka kimapenzi na binti wa kiarabu ambaye anamfanya Manyika kushindwa kufanya mazoezi Mara kwa Mara.

Jul 6, 2016

KIUNGO WA SEVILLA ASAINI MILAN

Na Haji balou
Timu ya Inter Milan imekalilisha usajili wa kiungo wa Sevila Na timu ya taifa ya Argentina Ever banega kwa mkataba wa miaka mitatu.

Banega aliisaidia Sevilla kuchukua mataji mawili mfululizo ya kombe la Europe league Na sasa ameamua kwenda Italy kwa uhamisho huru ili kitafuta changamoto mpya.

SIMBA YAMWEKA NJIA PANDA ISIHAKA

NA Haji Balou
Beki wa kati wa timu ya simba Hassan Isihaka amesema bado hajajua mustakabali wake Na timu yake ya simba katika msimu ujao.

“Wao bado hawajanifuata na mimi niko
njia panda kwani sifahamu lolote juu ya
maisha yangu ya Simba kama nitakuwepo
kwenye timu katika msimu ujao ama la,
lakini ni bora waniambie mapema nijue
nachukua maamuzi gani.

“Nasikia tu tetesi kuwa wanataka
kunipelekea Mbao FC ya Mwanza, lakini
kwangu sidhani kama nitaenda huko kwa
sababu mchezaji ndiye anayechagua wapi
aende sasa kama wao wamepanga
kunipeleka huko wataenda kucheza
wenyewe,” alisema Isihaka.

SOURCE: CHAMPIONI

Jul 5, 2016

20% AKUBALI YAISHE ASAINI MIAKA MITANO KWA MAN WATER

Na Haji balou
Msanii mkongwe wa muziki, Abbas Hamisi
Kinzasa ‘20%’ amerudi katika label yake ya
zamani ‘Combination Sound’ inayosimamiwa na
mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Man
Water.

Muimbaji huyo ambaye mwaka 2011 alitwaa
tuzo saba za Kilimanjaro Music Award (KTMA)
kwa mara moja, huku producer wake Man Water
akichukua tuzo mara mbili mfululizo za producer
bora (mwaka 2013 na 2014), tayari
amesharekodi ngoma kadhaa chini ya producer
huyo.

Kupitia instagram, Man Water ameandika:
Twenty Percent is back 2016, kaa mkao wa kula
ngoma zenye jumbe nzito na za kusisimua, kila
kitu kiko sawa sasa, new page.
20% kwa sasa anajipanga kuachia wimbo wake
mpya utaotoka Julai 18 mwaka huu huku
akijapanga kuandaa albamu yake iitwayo ‘Sauti
ya Gharama’.

Jul 4, 2016

SUAREZ MWINGINE ASAINI BARCELONA

Na Haji balou
FC BARCELONA imesibitisha kumsajili kiungo wa timu ya Villarreal Denis Suarez Na kesho anatarajiwa kupimwa afya.

Suarez mwenye umri wa miaka 22 alicheza Barcelona B kabla ya kuondoka kuamia Sevilla Na baadae kujiunga Na Villarreal ambayo aliisaidia mpaka kufika hatua ya nusu fainali Na  sasa amerudi tena  Barcelona.

Denis Suarez hana udugu wowote Na staa wa timu hiyo Luis Suarez ambaye alijiunga Barcelona misimu miwili iliyo pita.

STAA MWINGINE TOTENHAM KUJIUNGA REAL MADRID

Na Haji balou
Klabu ya Real madrid  tayari Kutoa euro million 35 ili kumnasa kipa namba moja wa Totenham Na Timu ya taifa ya Ufaransa  Hugo Lloris.

Kama Hugo Lloris  atajiunga Na Real Madrid atakuwa mchezaji watatu kujiunga Na Real Madrid akitokea Totenham kwa kipindi cha hivi karibuni  wachezaji wengine ni Gareth Bale, Luka Modric Na Emmanuel aliye enda kwa mkopo.