SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 23, 2015

MECKY MEXIME ATAJA KIKOSI CHAKE BORA VPL2014/2015

mtibwa-picha
TUNAENDELEA  kuangalia vikosi bora vya makocha wa timu za ligi kuu soka Tanzania bara, makocha wasiokuwa na timu na wachambuzi wa soka kwa msimu wa 2014/2015.
Jana tulikuwekea kikosi bora kilichopendekezwa na kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi na tukaahidi kukupatia kikosi bora cha kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime….
Hiki ndicho kikosi bora cha ligi kuu soka Tanzania bara msimu 2014/2015, kwa mujibu wa Mexime;
  1. Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
  2. Hassan Ramadhan Kessy (Simba)
  3. David Charles Luhende (Mtibwa Sugar)
  4. Salim Mbonde (Mtibwa Sugar)
  5. Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ (Yanga)
  6. Mudathir Yahya (Azam fc)
  7. Simon Msuva (Yanga)
  8. Haruna Niyonzima (Yanga)
  9. Amissi Tambwe (Yanga)
  10. Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
  11. Emmanuel Okwi (Simba)

NDANDA FC KUMUIBUKIA ALIKO DANGOTE

Aliko Dangote, President and CEO of Nigeria's Dangote Group speaks during the final session of the World Economic Forum
Bilionea Aliko Dangote
Uongozi wa Ndanda FC unajipanga kukutana na bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kwa ajili ya kumuomba kuwa mmoja wa wadhamini wa juu katika timu hiyo kabla msimu ujao haujaanza.
Salehjembe ameripoti kwamba  mwenyekiti wa Ndanda FC, Hamad Omari alisema licha ya kuwa na udhamini wa Kampuni ya Binslum na Big Tanzania, lakini wanajipanga kumuona tajiri huyo anayemiliki kiwanda cha saruji kwenye mkoa wao.
“Tunafikiria kufanya mikakati ya kuweza kukutana naye ili aweze kuwa mdhamini mkuu kwenye timu yetu ambayo imenusurika kushuka daraja.
“Unajua tangu ligi imemalizika bado hatujakaa kuweza kujadili hayo mambo na kama ataweza kukubali basi litakuwa ni jambo jema kwa sababu fedha zinazotolewa na wadhamini wa ligi hazikidhi mahitaji ya timu kwa msimu wote, sasa lazima njia nyingine zitumike kuhakikisha tunakuwa vizuri zaidi msimu ujao,” alisema Omari.

Dangote, raia wa Nigeria, kwa sasa ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara ambako timu hiyo inatokea, anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4 (shilingi trilioni 2.7) na hivi karibuni alitangaza nia ya kuinunua Klabu ya Arsenal ya England.

MWAMBUSI AICHOMOLEA NJE AZAM FC


 IMG_5671
WAKATI Azam fc wakidai idadi ya wachezaji wa kigeni ligi kuu soka Tanzania bara iongezwe kutoka idadi ya sasa ya watano, kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi amepinga mtazamo huo.
Hoja ya Azam kutaka idadi iongezeke ni kupata wachezaji wengi wa kigeni watakaowasaidia katika michuano ya kimataifa pamoja na kuwapa changamoto wachezaji wazawa ndani ya timu hiyo.
Makamu bingwa hao wa ligi kuu msimu wa 2014/2015 wanadai wamejifunza kwa TP Mazembe na El Merreikh ambao wamesheheni wanasoka wengi kutoka nje ya nchi zao.
Azam wakitoa hoja hizo, Mwambusi amesema haoni haja ya kuongeza wachezaji wa kigeni bali vipaji vya ndani viangaliwe zaidi.
“Siungi mkono kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni katika soka letu la Tanzania kwasababu sisi tuna wachezaji wengi wenye vipaji. Muhimu ni wachezaji wetu kujitambua kwanza, halafu viongozi wa klabu zetu wanawachukuliaje wachezaji wetu?” Amesema Mwambusi na koungeza: “Saa nyingine watu wanataka kusajili kwa fasheni, vilabu vikubwa vinashindana kusajili wachezaji wa nje, tusichukue wachezaji kwasababu tu tunataka kushindana na fulani, tuwachukue wachezaji wa nje kwasababu wana kiwango cha juu ili waje kuleta changamoto hapa kwetu”.
“Kwa idadi iliyopo inatosha kwasababu tumeshaona hata hao watano kuna wengine wanakaa nje kwa kushindwa na wazawa. Mimi nasema wachezaji wetu wanatakiwa kujitambua tu ili wajue kuwa mpira ni kazi, wajitoe na kucheza kwa juhudi zote uwanjani ili kuweza kuendeleza soka letu”.
“Wanaweza kuja hata wachezaji 11 wa kigeni, sijui kama itatusaidia, kikubwa tuangalie tulipojikwaa, tusiangalie tulipoangukia. Viongozi wanaweza kusema vijana wetu hawajitambui, sawa!, watajitambuaje? Kila mtu kwa nafasi yake katika mpira afanye kazi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na kwa umakini mkubwa, viongozi wanaotawala soka katika nchi yetu wana nia kweli ya kuendeleza soka letu?. Tunaweza tukakubali kuleta wachezaji wengi, lakini tusipopita kwenye mfumo sahihi hatuwezi kufika kokote”.