SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 9, 2015

WENGER HAJUI WILSHERE ATARUDI LINI

 
Wilshere hajacheza tangu Novemba alipoumia kifundo cha mguu katika mechi ya Ligi Kuu ya England ambapo Arsenal ilifungwa mabao 2-1 na Manchester United.
Alikua arejee mazoezini lakini kabla ya mechi ya Jumanne dhidi ya Leicester City, Wenger alisema: "Lazima tumchunguze kila siku. Sijui lini ataweza kurejea uwanjani."

Kuhusu mchezaji mwingine Alexis Sanchez ambaye tayari amefunga mabao 18 msimu huu, Wenger alisema, “ Atajiunga na kikosi “ kitakachocheza na Leicester na kwamba hakukuwepo majeruhi wowote katika mchezo wa Jumamosi ambapo Arsenal walishindwa na watani wao wa jadi Tottenham. Kwa kupoteza mechi hiyo Arsenal sasa inashiikilia nafasi ya sita katika Ligi Kuu.


Mbali na Wilshere na Sanchez Arsenal pia inamkosa Alex Oxlade-Chamberlain ambaye aliumia wakati Arsenal ilipopambana na Manchester City mnamo mwezi uliopita.

SERIKALI YA MISRI YATOA ADHABU KUTOKANA NA VURUGU ZA JANA

misri
Mashabiki wa soka Misri huenda safari hii wakasahau kwa muda ligi kuu ya nchini kwao baada ya Serikali kutangaza kuisimamisha ligi hiyo kwa muda usiojulikana baada ya kuzuka vurugu zilizotokea jana na kusababisha watu zaidi ya 20 kufariki.
Wengi wa waliofariki ni mashabiki wa timu ya Zamalek ambao walifariki kutokana na msongamano mkubwa wa watu waliokuwa wakijaru kuingia kwa nguvu uwanjani ambapo Polisi waliwafyatua mabomu ya machozi wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.fan
Taarifa ya Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalekwalikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu bila tiketi, Polisi walijikuta wakitumia nguvu ya ziada kuwazuia ili wasifanye uharibifu uwanjani.
Tukio hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu itokee ishu kama hiyo ambapo wapenzi wa soka zaidi ya 70 walifariki wakati vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege wa Port Said.

NDOA YAMBADILI EMMANUEL OKWI KAMBINI SIMBA

Mshambuliaji nyota wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, anadaiwa kubadili mfumo wake wa maisha ndani ya klabu hiyo tangu aliporejea kutoka katika likizo ya ndoa aliyokuwa amepewa na uongozi wa timu hiyo baada ya kuoa.


Okwi ambaye hapo awali alikuwa akidaiwa kuwa na tabia ya usumbufu, hivi sasa ni mtoto mwema kutokana na kuwa msitari wa mbele kuzingatia kila jambo analoagizwa kufanya na kocha mkuu wa timu hiyo, Mserbia, Goran Kopunovic.

Hali hiyo, Pia imewafanya viongozi wa timu hiyo kutoyaamini macho yao kwani walizoea kumwona akiwa tofauti kabisa na alivyo hivi sasa ikiwa ni baada ya kuoa.

Kopunovic ambaye amejiunga na Simba akichukua mikoba ya Mzambia, Patrick Phiri, alisema kuwa kila siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo Okwi anavyozidi kubadilika kwani tabia yake ya sasa ni ya kuigwa na wachezaji wote katika kikosi hicho.

“Hakika najivunia kuwa na mchezaji kama Okwi katika kikosi changu kwani ni mfano wa kuigwa na wenzake kuanzia ndani na nje ya uwanja, japokuwa hapo awali nilisikia kuwa ni msumbufu lakini binafsi usumbufu huo sijauona.

“Hata hivyo nimekuwa nikisikia baadhi ya wachezaji wenzake wakimtania kuwa tangu alipooa amebadilika sana, labda hiyo ndiyo sababu,” alisema Kopunovic.

Okwi amejiunga na Simba msimu huu akitokea Yanga ambako alikuwa akisumbuana vilivyo na viongozi wa klabu hiyo na mpaka sasa bado ana kesi nao baada ya kudai kuwa wanataka kwenda kumshtaki kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutokana na kukiuka masharti ya kimkataba.

RATIBA YA MECHI ZINAZO FUATA LIGI KUU BARA

 
 
Feb 11- Azam vs Mtibwa Sugar

Feb 14- Ndanda vs Mtibwa Sugar
             Coastal Union vs Mbeya City
             Stand United vs Mgambo Shooting
            
Feb 15- Polisi Morogoro vs Simba
             Kagera Sugar vs JKT Ruvu
Feb 21- Mbeya City vs Yanga
             Kagera Sugar vs JKT Ruvu
             Ndanda vs Coastal Union
             Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar
Feb 22- Stand United vs Simba
              Azam vs Tanzania Prisons
Feb 25- Mbeya City vs Ruvu Shooting 

NGASSA AWAOMBA MSAMAHA SIMBA SC



Mara mbili jana Mrisho Ngassa alionyesha ishara ya kuwaomba msamaha mashabiki wa Simba SC baada ya kufunga mabao yote mawili, Yanga SC ikishinda 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Alikuwa anamanisha nini? 

WAAMUZI MECHI YA AZAM , YANGA HAWA HAPA

MAREFA kutoka nchi jirani za Burundi na Somalia, ndio watachezesha mechi za kwanza za Raundi ya Awali ya michuano ya Afrika za timu za Tanzania mwishoni mwa wiki.
Yanga SC itamenyana na BDF XI Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Azam FC watakuwa wenyeji wa El Merreikh ya Sudan Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji.
Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Azam na El Merreikh refa atakuwa Hassan Mohamed Hagi, wasaidizi wake namba moja Bashir Sh Abdi Sule na namba mbili Salah Omar Abubakar wakati mezani atakuwa Kidane Melles Terfe, wote wa Somalia.
Kikosi cha Azam FC kilichotolewa mapema Kombe la Shirikisho mwaka jana na Ferroviario mwaka jana

Kamisaa wa mchezo huo atakuwa M.CHaileyesus Bazezew Beleti kutoka Ethiopia.
Mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga SC na BDF XI, refa atakuwa Thierry Nkurunziza, wasaidizi wake Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili na mezani George Gatogato, wote wa Burundi wakati Kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.

ALICHOSEMA YAYA TOURE KUHUSU MAN CITY

NAHODHA wa Ivory Coast, Yaya Toure amesema kwamba klabu yake, Manchester City inatakiwa kushinda mechi zote zilizobaki ikiwa inataka kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Akizungumza baada ya kuwaongoza Tembo kushinda taji la Kombe la Mataifa ya Afrika, Toure ambaye alikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango kwenye baadhi ya mechi za AFCON alisema yuko tayari kurudi kazini Man City.
Lakini klabu yake ikiwa inazidiwa pointi saba na vinara Chelsea, nyota huyo wa Ivory Coast amesema hiyo si kazi rahisi.
Yaya Toure, pictured after winning the Africa Cup of Nations, insists Manchester City can win the league
Yaya Toure akipokea Kombe la Afrika jana mjini Bata, Equatorial Guinea baada ya kuiongoza Ivory Coast kushinda kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120

"Kwa kujiamini kwangu, najua soka si kuhusu mchezo mmoja, au miwili hususan katika Ligi Kuu ya England,"amesema.
"Tuna mechi 38 na ikiwa tunataka kushinda (kutetea ubingwa) tunatakiwa kushinda mechi zote. "Nafahamu ni vigumu, lakini nafahamu natakiwa kurejea na kufanya kazi yangu tena,".
 
Toure alifunga mkwaju wake wa penalti wakati matuta jana Ivory Coast ikiibwaga Ghana 9-8 na kutwaa Kombe- na sasa anarejea England kuisaiedia Man Citu viya ya kutetes taji baada ya kukosekana tangu mwezi uliopita.
Na Manchester City haijashinda mechi hata moija tangu Mwanasoka huyo Bora wa Afrika aende kwenye AFCON.

MAGWIJI WA BARCELONA KUKIPIGA DAR

KIKOSI cha magwiji wa Barcelona kitazuru Dar es Salaa Machi 28 mwaka huu kwa ajili ya mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya wachezaji nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, maarufu Tanzania Eleven.
Almasi Kasongo, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam, wanaoandaa ziara hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya Prime Time Promotions amesema hayo leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari ukumbi wa City Sports Lounge, Dar es Salaam.
 
Mkutano huo, ulihudhuriwa na mkali wa zamani wa mabao wa Barcelona, Mholanzi Patrick Kluviert ambaye amethibitisha ujio wa nyota waliotaka Camp Nou miaka ya nyuma kidogo.
Ziara hiyo ni matunda ya ziara ya magwiji wa wapinzani wa Barcelona, Real Madrid Agosti mwaka jana, ambao pia walicheza na magwiji wa Tanzania na kushinda 3-1 Dar es Salaam.
Patrick Kluivert katikati akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam leo

Mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23, mwaka jana na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Reuben de La Red alifunga mabao matatu peke yake, magwiji.
 
De la Red alimfunga bao moja Mwameja Mohamed kipindi cha kwanza na kipindi cha pil akamtungua mara mbili Manyika Peter, wakati bao pekee la Stars, Real walijifunga wenyewe kupitia kwa Roberto Rojas.
Siku hiyo, Rais Kikwete alimkabidhi mpira De La Red baada ya mechi kabla ya kuwakabidhi Kombe Real Madird kwa ushindi huo.
 
Katika mchezo huo, ambao wachezaji waliingia na kutoka, Real Madird walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, De La Red akimalizia pasi ya Luis Figo.
Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa kiungo Christian Karembeu, aliyezuia shambulizi la Tanzania na kuanzisha shambuizi zuri lililozaa matunda, akiuvuka msitu wa wachezaji wa wenyeji kwa umahiri mkubwa.
 
Tanzania Eleven ilisawazisha dakika ya 45 baada ya kona ya Mecky Mexime kuzua kizaa langoni mwa Real na Roberto Rojas akajifunga katika harakati za kuokoa baada ya Kali Ongala kuuparaza kwa kichwa. 
Kipindi cha pili, De la Red alifunga bao kwa pili kwa penalti dakika ya 81 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Habib Kondo kwenye eneo la hatari.
Awali ya hapo, Figo alimtoka vizuri beki Mecky Mexime na kuingia hadi kwenye eneo la hatari akiwa 

kwenye nafasi ya kufunga akampasia De La Red ambaye alipiga nje.
De la Red alikamilisha hat trick yake dakika ya 88 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Tanzania Eeleven na baada ya hapo, wachezaji wa timu zote mbili wakajumuika katika hafla ya chakula cha usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu.

KWA RATIBA HII SISHANGAI BURNLEY IKISHUKA DARAJA

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMATATU

.
.
 
.
.
.
.
.
.
.
.

YAMOTO BAND KAMILI KWA KWENDA KUFANYA SHOW LONDON

 Kutoka kushoto Enock, Maromboso, Beka na Aslay wakiwa wameshikilia ticket zao za ndege  ambazo walikabidhiwa rasmi na mkurugenzi wa Zurii house of Beauty Jestina George Meru.
Yamoto Band wanatarijiwa kufanya Live show kwenye jiji London siku ya tarehe 21.02.2015 katika ukumbi wa Royal Regency Banguet Hall 
 Zuri House of Beauty CEO Jestina George Meru akiwa kwenye picha ya pamoja na timu nzima ya Yamoto Band 
Kama kawaida Ukitembelea Zurii House of Beauty huondoki mkono mtupu
UK na Europe yote Siku ya Jumamosi tarehe 21 Feb 2015 tukutane pale kwenye ukumbi wa Royal Regency Manor Park London Kwani Hiyo ndio sehemu pekee kwenye jiji la London utapopata Burudani ya kukata na shoka kutoka kwa No1 band ya Tanzania Hakuna wengine ni wale wale vijana wetu wanne machachari wanaoitikisha East Africa sasa hivi YAMOTO BAND aka MKUBWA na WANAWE.

IVORY COAST MABINGWA WAPYA AFRIKA

TIMU ya Taifa ya Ivory Coast imetwaa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Bata, Equatorial Guinea.
Historia imejirudia, baada ya Tembo kuwaunga ten Black Stars kwa penalti katika fainali kama ilivyokuwa 1992 walipotwaa taji lao la kwanza.
 
Shujaa wa Ivory Coast usiku huu alikuwa ni kipa Boubacar Barry aliyefunga penalti ya mwisho, akitoka kuokoa ya kipa mwenzake, Razak Braimah na kumaliza kiu ya miaka 23 ya taifa lake kusubiri taji hilo.
Penalti za Ivory Coast zilifungwa na Aurier, Doumbia, Yaya Toure, Soomon Kalou, Kolo Toure, Kanon, Bailly Serey Die na Barry, wakati Wlifried Bony na Tallo walikosa mbili za kwanza.
 
Penalti za Ghana zilifungwa na Mubarak Wakaso, Joedan Ayew, Andre Ayew, Mensah, Agyemang-Badu, Afful, Baba na Boye wakati Acquah, Achwampong na Brimah walikosa.  
 
Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang, Rais wa FIFA, Sepp Blatter na Rais wa CAF, Issa Hayatou walikuwepo uwanani na awali walikagua vikosimkabla ya kukabidhi Medali na taji kwa washindi baada ya mechi 
 
Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa; Barry, Bailly, Aurier, Kanon, Toure, Tiene/Kalou dk114, Die, Toure, Gradel/Doumbia, dk66, Bony na Gervinho/Tallo, sk120. 
 
Ghana; Razak, Boye, Rahman, Mensah, Afful, Mubarak, Acquah, Ayew, Atsu/Acheampong dk115, Gyan/Agyemang-Badu dk120 na Appiah/Ayew dk98.
The Ivory Coast team and staff pose with their Africa Cup of Nations trophy having defeated Ghana 9-8 on penalties on Sunday night
Wachezaji wa Ivory Coast na viongozi wao wakifurahia na Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa penalti 9-8 dhidi ya Ghana usiku huu
Manchester City striker Wilfried Bony holds up hero Boubacar Barry (centre), who scored the winning penalty in the final in Bata 
Mshambuliaji wa Manchester City, Wilfried Bony akiwa amembeba kipa Boubacar Barry baada ya kufunga penalti ya mwisho mjini Bata 

BARCELONA YAFANYA MAUAJI LA LIGA SASA YAIKARIBIA KABISA REAL MADRID

TIMU ya Bercelona, imeichapa mabao 5-2 Athletic Bilbao katika mchezo wa La Liga na kupunguza pengo la pointi wanazozidiwa na vinara, Real Madrid hadi kubaki moja. 
Lionel Messi alifunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu dakika ya 15 kabla ya Luis Suarez kufunga la pili dakika ya 26, De Marcos akajifunga kuipatia Barca bao la tatu dakika ya 62, Neymar akafunga la nne dakika ya 64 na Pedro la tano dakika ya 86.
 
Mabao ya Athletic Bilbao yalifungwa na Mikel Rico dakika ya 59 na Aduriz dakika ya 66, wakati timu hiyo ilipata pigo dakika ya 75, baada ya mchezaji wake, Etxeita kutolewa kwa kadi nyekundu 75. 
 
Kikosi cha Athletic Bilbao kilikuwa: Iraizoz, De Marcos, Etxeita, Laporte, Balenziaga/Aurtenetxe dk52, San Jose, Mikel Rico, Susaeta/Benat dk69, Lopez, Muniain/Gurpegui dk78 na Aduriz.
 
Barcelona: Bravo, Alves/Adriano dk69, Mathieu, Pique, Alba, Xavi/Rafinha dk74, Busquets, Rakitic, Messi, Suarez/Pedro dk80 na Neymar.
Xavi (right) goes approaches Messi (centre) after the latter helped take Barcelona one point off top
Xavi (kulia) akishangilia na Messi (katikati) na Suarez kushoto baada ya ushindi wao 
 Barcelona forward Lionel Messi celebrates after scoring his side's opening goal against Athletic BilbaoMshambuliaji Leonel Messi akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Barcelona
Luis Suarez (left) doubled Barcelona's lead, ensuring three points for Luis Enrique's team at San MamesMchezaji Luis Suarez akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Barcelona.
Neymar controls the ball, as Barcelona beat Athletic Bilbao to go within touching distance of Real Madrid



Ivan Rakitic (left), Messi and Neymar celebrate at San Mames as Barcelona beat Athletic Bilbao
 Pedro wheels away in celebration after coming on as a substitute to score Barcelona's fifth goal of the game