SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jul 16, 2015

KIBURI CHAMUONDOA VALDEZ MAN UNITED

Victor-Valdes-training
Hatimaye kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amefumbua kile kilichokua kimejificha baada ya kushuhudia golikipa Victor Valdez akiachwa katika safari ya ‘Pre-season’ nchini Marekani.

Akiongea kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari katika ‘tour’ hiyo ya nchini Marekani, pamoja na mambo mengine, Van Gaal alithibitisha kuwa klabu inajiandaa kumuuza mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona.

Van Gaal akatoboa kwamba, Valdez aligoma kucheza katika mechi za U21 ikiwa ni utaratibu wa kujijenga kurudi katika fomu yako ya kawaida.

Van Gaal amesema, Valdez alienda kinyume na aliichoita ‘philosophy’ yake. Van Gaal huwamuru wachezaji kujiunga na timu ya vijana ya U21 katika hali ya kuwafanya warudishe fitness zao, lakini Valdez alikataa imefahamika.

Pamoja na sintofahamu ya golikipa David de Gea, lakini Van Gaal anasema hawawezi kumvumilia mchezaji kama Valdez na kumshangaa kwamba walimsaidia kurudi katika hali yake, ikiwa ni pamoja na kumpa mkataba lakini amekiuka masharti.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wa De Gea, kocha huyo alisema ni upuuzi kuuliza swali hilo kwani De Gea anaonesha ‘commitment’ na ueledi mkubwa kikosini hapo.

Kuhusu DiMaria, Van Gaal alisema, mchezaji huyo ni mali yao lakini akasisitiza kuwa soka ni mchezo usiotabirika na kwamba mashabiki wasubiri kuona hadi mwisho itakuwaje.

Aidha katika mkutano huo na waandishi wa habari, wachezaji wapya walitambulishwa huku wakiulizwa pia maswali na waandishi katika utaratibu wa kawaida kabisa wa media.

Kwingineko tetesi zinasema kuwa Manchester United inamuwinda golikipa Romero wa timu ya taifa ya Argentina huku Real Madrid nao wakiingilia dili hilo.

STEWART ASEMA MESSI,TCHETCHE, AME, WAWA WOTE ‘WAPO UNGA’

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
NYOTA wa Azam FC, Serge Wawa Pascal Kipre, Miachel Balou, Kipre Herman Tchetche wote raia wa Ivory Coast pamoja wazalendo Ramadhani Singano ‘Messi’ na Ame Ali ‘Zungu’ wote hawako fiti.
Hayo yamesemwa na kocha Mkuu wa timu hiyo Muingereza, Stewart John Hall katika mahojiano na BIN ZUNBEIRY SPORTS- ONLINE jana jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Pamoja na hao, Stewart amesema wachezaji wawili pia waliokuja majaribio kipa Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast na kiungo Ryan Burge kutoka England, pia hawako fiti.
Na wakati michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inaanza Jumamosi Dar es Salaam, Stewart amesema kwamba wachezaji wake kadhaa tegemeo hawako tayari. 
Hawako fiti; Kipre Tchetche (kulia) na Ramadhani Singano 'Messi' kushoto wakifanya mazoezi maalum baada ya kumaliza programu ya timu jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Stewart amevutiwa na Burge na amempa programu maalum ya kumuweka fiti pamoja na Wawa, Balou, Tchetche, Messi na Ame ambao wote wamekuwa wakifanya mazoezi ya ziada kabla na bada ya mazoezi ya timu kwa ujumla.
“Siku chache zimebaki kabla ya Kagame, lakini wachezaji wengi tegemeo katika kikosi cha kwanza hawako fiti. Messi, Kipre Tchetche, Balou, Ame, Serge Wawa na Ryan wote hawako fiti kwa sababu walichelewa kujiunga na wenzao kwa maandalizi ya mwanzo wa msimu,”amesema.
Hata hivyo, mtaalamu huyo amesema atafanya jitihada zinazowezekana kuhakikisha kwa siku chache zilizobaki wachezaji hao wanakuwa fiti angalau kwa asilimia 50.
Stewart Hall (katikati) akijadiliana na Meneja wa Azam FC, Luckson Kakolaki na kipa wa timu ya vijana, Metacha Boniphace
Kipre Michael Balou hayuko fiti
Serge Wawa Pascal pia hayuko fiti

“Napambana kupata angalau asilimia 50, kama wakizidi hapo itakuwa vizuri. Lakini lengo ni kufanya vizuri katika haya mashindano, ikibidi kuchukua Kombe,”amesema. 
Aidha, Stewart amepongeza usajili wa kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ kutoka APR ya kwao, akisema ni mchezaji mzuri kwa ujumla.
Migi anakuwa mchezaji wa sita wa kigeni wa Azam kati ya saba wanaotakiwa- na wa kwanza kabisa mpya kusajiliwa msimu huu. Wachezaji wa kigeni waliopo Azam FC ni beki Serge Wawa Pascal, kiungo Kipre Michael Balou, mshambuliaji Kipre Tchetche wote kutoka Ivory Coast, winga Brian Majwega kutoka Uganda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi ambao wote walikuwepo msimu uliopita.
Jean Baptiste Mugiraneza amefikisha idadi ya wachezaji sita wa kigeni waliosajiliwa Azam FC

Lakini pia, kuna wachezaji wengine wanne wa kigeni wanawania kusajiliwa Azam FC katika nafasi moja iliyobaki, ambao ni makipa Nelson Lukong kutoka Cameroon, Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast, kiungo Ryan Burge kutoka England na mshambuliaji Allan Wetende Wanga kutoka Kenya.
Lukong na Wanga wamegoma kufanya majaribio na kocha Muingereza Stewart Hall amesema hatasajili mchezaji ambaye hajamuona mazoezini- hivyo nafasi hiyo inaweza kuchukuliwa na Burge anayaendelea na majaribio, kwani hata kipe mwingine Angban anaonekana wa kawaida.
Awali, Azam FC ilisajili wazalendo tu wawili ambao ni kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Simba SC na Ame Ali ‘Zungu’ kutoka Mtibwa Sugar.
Azam imepangwa Kundi C pamoja na Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda, wakati Kundi A kuna wenyeji wengine, Yanga SC, Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan na Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan FC ya Somalia.

SIMBA WATUMIA MUDA WAO KUWALIWAZA WATOTO YATIMA WA LUSHOTO


Pamoja na maandalizi ya kambi mjini Lushoto, Simba wametumia muda wao mchache kutembelea kituo cha watoto yatima cha Irente.


Wakiongozwa na Kocha Dylan Kerr, Simba na kikosi chao kizima walitua katika kituo hicho kilichopo Lushoto pia na kuzungumza na watoto hao ikiwa ni pamoja na kuwaliwaza.
Kerr alionekana kufurahishwa na suala hilo na kusema lilikuwa jambo zuri.


“Kama watu wanaoaminika au wanaotazamwa na jamii, ni jambo jema kuungana na wanajamii wengine kama tulivyofanya,” alisema Kerr raia wa Uingereza.

CHELSEA WALIVYOTUA NCHINI CANADA TAYARI KWA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA

CHELSEA WAMETUA JIJINI MONTREAL NCHINI CANADA KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU ENGLAND. CHEKI WALIVYOWASILI.










SIRI YA DILUNGA KUSUSA YANGA SC HII HAPA…

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIUNGO Hassan Dilunga (pichani) amegoma kuhudhuria mazoezi Yanga SC, kwa sababu ameambiwa atatolewa kwa mkopo Stand United.
Dilunga ameamua ‘kujifungia’ nyumbani kwao na kutokwenda mazoezini Yanga SC, huku uongozi wa klabu hiyo ukipanga kumchukulia hatua za kinidhamu.
BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE imeambiwa na rafiki wa karibu wa Dilunga kwamba ameamua kususa mazoezi kwa sababu haoni sababu ya kufanya mazoezi na timu ambayo hataichezea.
“Amegoma kwa sababu wamemuambia watamtoa kwa mkopo, naye amesema haoni sababu ya kufanya mazoezi na timu ambayo hataichezea,”amesema rafiki huyo wa Dilunga.
Mwenyewe Dilunga alikua mkali alipotafutwa na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE na kusema hataki kuzungumza chochote kuhusu mambo yake na Yanga SC.
“Sitaki uandike chochote kutoka kwangu kuhusu mimi na Yanga SC, wewe iache kama ilivyo,”alisema jana Dilunga.
Yanga SC imeingia kambini jana katika hosteli za Chuo Cha Maaskofu, Kurasini mjini Dar es Salaam kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Yanga SC ambayo imepangwa Kundi A pamoja na Gor Mahia ya Kenya, Telecom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khartoum-N ya Sudan, itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini.
Mabingwa mara tano wa michuano hiyo, 1975, 1993, 1999, 2011 na 2012, watafungua dimba na Gor Mahia Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo itatanguliwa na mchezo kati ya APR ya Rwanda dhidi ya Al Shandy ya Sudan Saa 8:00 mchana.