SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 13, 2015

MAGAZETI YA MICHEZO LEO FEB 13

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

WAZAMBIA KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI DAR

Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
KLABU ya Red Arrow FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia inatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam-Tanzania Jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuweka kambi ya mafunzo ya wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 2015.
Uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Col Nolacso K Chilando ulifika leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF sambamba na Ofisa Habari wa klabu, Luteni Kanali Melody Siisii, Alex Chila Ofisa ubalozi wa Zambia nchini Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini.

Kutoka kushoto ni Ofisa habari wa Red Arrows  Lt Melody Siisii, Mwenyekiti wa Red Arrows Col Nolasco Chilando, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na Ofisa Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania Alex Chila, wakiwa ofisi za TFF - PPF Tower leo.

Wakiongea na katibu  mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mweisgwa, uongozi wa timu hiyo umesema maandalizi ya kambi yameshakamilika na kikubwa walikua wanaliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kutambua uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya kufanyia mazoezi.
 
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF Bw.Mwesigwa  alisema wameyapokea maombi hayo ya Red Arrow FC  na kuwakaribisha nchini kwa ajili ya kambi yao na kusema ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine pia kuja kuweka kambi nchini.
 
Timu ya Red Arrow FC inayomilikiwa na jeshi la Anga nchini Zambia ikiwa nchini kwa mafunzo, inatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini kuwatafutia timu moja ya kucheza nayo.

KLUIVERT KUISAIDIA STAND UNITED

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Ajax Amsterdam, Barcelona ya Hispania na Newecastle ya England, Patrick Kluivert amewasili Shinyanga kwa shughuli mbalimbali za kimichezo ikiwemo kufugua kituo cha michezo katika shule ya sekondari Com mjini hapa.
Kluveirt ambaye ameambatana na mchezaji wa zamani Real Madrid na Barcerona za Hispania, Marco Garcia walikuwa wageni wa Mbuge wa jimbo la Shinyanga, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Steven Masele wakati wa kufunga kituo cha michezo katika shule ya sekondari com kwa lengo la kutengeneza vijana wazuri wenye uwezo wa  kucheza mpira kwa ufundi zaidi.



Akifungua kituo hicho, Steven Masele alisema kituo hicho cha michezo kitatumika kuinua vipaji kwa wachezaji na pia kuwaomba wazazi pamoja na wadau wengine wa soka mkoani shinyanga kushikamana katika michezo.
“jengo hili ni kwa ajili ya kuweka vifaa vya michezo pamoja na kutoa mafunzo kwa watoto watakao jiunga na kituo hiki ambapo moja ya vifaa hivyo ni gym na vifaa vingine vya mazoezi”alisema Masele.
Kwa upande wake, Kluveirt alisema kuwepo kwa kituo hicho ni njia pekee ya kuibua vipaji na kutengeneza wachezaji ambao wataweza kucheza mpira vizuri ndani ya nchi na hata nnje ya nchi pia na hivyo kuwataka watoto wanaocheza mpira mjini Shinyanga kutumia fursa hiyo.
“Mimi nilianza kucheza mpira nikiwa mdogo sana, lakini nilijituma hivyo ukianza mpira ukiwa mdogo utakapo kua utaweza kucheza mpira vizuri sana”alisema  Kluivert.
Kabla ya zoezi hilo kufanyika Patric Kluivet alianza kwa kuzungumza na kutoa mafunzo kwa wachezaji wa timu ya Stand United ya mjini Shinyanga inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage.
“Katika kucheza mpira mchezaji yeyote anatakiwa kuwa na vitu vitatu muhimu kwanza awe na nidhamu, awe msikivu kwa mwalimu wake halikadhalika kujituma katika mazoezi, akifanya hivyo, lazima atafanya vizuri. Hivyo nawaomba msikilize sana mwalimu wenu anawafundisha nini, pia ni lazima mjitambue kuwa mnafanya nini” alisema Kluivert.

KESI YA KASEJA YA AHIRISHWA

ALIYEKUWA kipa wa Yanga SC, Juma Kaseja leo asubuhi amepandishwa Baraza la Usuluhishi katika mahakama ya Kazi, Dar es Salaam kuhusu mashataka ya kuvunja mkataba na klabu hiyo, lakini tukio la moto limeahirisha shauri hilo.
Akizungumza mara baada ya kusikilizwa kwa awali kwa shauri hilo Mwanasheria wa Yanga SC, Frank Chacha amesema shauri hilo limeahirishwa kufuatia maombi ya upande wa Kaseja ambao ofisi zao za Kampuni ya Kisheria ya Mbamba Advocate zimeungua moto.


Chacha amesema Kaseja ambaye alikuwepo na mwanasheria wake, Nestory Mwenda waliwasilisha maombi hayo mbele ya Mheshimiwa Fimbo kuwa nyaraka zao mbalimbali za shauri hilo kuungua na moto katika ofisi zao zilizoungua na moto hivi karibuni katika jengo la Consolidated Investments lililopo mtaa wa Libya Mnazi mmoja.
"Tumelazimika kuwakubalia maombi yao hayo kwa kuwa hata sisi tunafahamu kwamba wenzetu wamekumbana na hilo tatizo sasa tnasububiri wajikamilishe ili turudi tena katika tarehe ambayo kesi imepangwa kuendelea,"alisema Chacha.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Machi 10 ambapo kila upande umekubaliana kuwa utakuwa tayari kuendelea kwa shauri hilo.
Yanga imemfikisha Kaseja katika kesi hiyo kwa madai kwamba kipa huyo mkongwe alivunja mkataba wake kwa kitendo cha kugoma kendelea kukipiga na klabu hiyo ambapo katika madai hayo klabu hiyo imemtaka Kaseja kulipa fidia ya shilingi 340 milioni.

CANNAVARO HATARINI KUIKOSA BDFXI

KOCHA mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm amesema kwamba Nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro' yuko kwenye hatihati ya kucheza mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana Jumamosi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo Dar es Salaam, Pluijm amesema ukiacha shaka hiyo juu ya Cannavaro, kila kitu kuhusu timu yake kipo sawa ambapo anazidi kufurahia umoja, mshikamano na utulivu waliokuwa nao vijana wake.
Pluijm amesema wapo tayari kwa kila kitu kuhusu wapinzani wao hao, lakini hofu yao ni maumivu aliyokuwa nayo Cannavaro ambaye goti lake la kulia.


"Hatujajua kama atakuwa sawa mpaka siku ya mchezo ni jambo la kusubiria leo na kesho kuangalia maendeleo yake lakini tunaimani atakuwa sawa, mbali na hapo naweza kusema tupo tayari kuingia vitani kupambana na hao Wanajeshi,"amesema Pluijm.
 
Wakati huo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga Jerry Muro amesema tayari wameanza kuuza tiketi za mchezo huo dhidi ya BDF ambao wanatua leo jioni na ndege maalum ya jeshi la Botswana.
"Wapinzani wetu wanaingia leo na ndege maalum ya jeshi la kwao na waankuja na msafara qwa wachezaji 25 pamoja na viongozi wao tunaomba wale wote wanaoipenda Yanga kununua tiketi mapema kuanzia leo ili kupunguza msongamano siku ya mchezo na siku hiyo milango ya Uwanja itafunguliwa mapema kuanzia saa saba mchana,"alisema Murro.