SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 29, 2016

HUU NDIO MWONEKANO MPYA WA HASSAN ISIHAKA WA SIMBA

Picha ya nahodha wa zamani wa Simba, Hassan Isihaka akiwa amenyoa rasta zake imekuwa gumzo zaidi mitandaoni kuanzia
jana.

Picha hiyo kwa mara ya kwanza
ilitundikwa na SALEHJEMBE, lakini
ikasambaa kwenye mitandao mingi na kuwa gumzo.

Isihaka alikuwa akipasha na kikosi cha Simba, awali alizoeleka kuonekana akiwa na rasta lakini sasa amezinyoa na kubaki
na afro.

Mar 27, 2016

JOSE MOURINHO AMEYASEMA HAYA KUHUSU MESSI

Na Haji balou
Kocha Jose Mourinho hivi karibuni amefanya mahojiano na kituo cha BT Sport na kutoa maoni yake juu ya tofauti ya kuwa na Lionel Messi
katika kikosi na kucheza dhidi yake, hasa katika Champions League.

“Messi ameshinda Champions League na makocha tofauti. Nadhani ni rahisi kushinda ukiwa nae kuliko ukicheza dhidi yake,” alisema.

Kocha huyo Mreno bado anaamini kwamba kucheza kitimu – teamwork ni muhimu.
“Mimi ni kocha wa timu ya soka Najua kwamba wakati mwingine watu wanadhani kwamba mchezaji mmoja mmoja ni muhimu kuliko timu.

Bado nafikiri kwamba timu ni muhimu zaidi kuliko chochote. Lakini ni ukweli dhahiri kwamba kuna baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kufanya tofauti,” alisema.

Mar 17, 2016

MAAMUZI MENGINE YA SIMBA KUHUSU HASSAN ISIHAKA


Na Haji balou
SIMBA SC imemfungia kwa mwezi mmoja pamoja na kumvua Unahodha, beki wake wa kati chipukizi, Hassan Isihaka baada ya kukutwa na hatia ya utovu wa nidhamu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara amewaambia Waandisji wa Habari leo kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezaji huyo kukutwa na hatia ya kumtolea 'maneno machafu' kocha wa klabu, Mganda Jackson Mayanja.
Manara amesema adhabu hiyo kwa Isihaka ambaye pia ni beki wa kati wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni onyo kwa wachezaji wengine wa klabu hiyo wasifikirie kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu katika timu.
Isihaka anadaiwa 'kumjibu utumbo' kocha Mayanja kabla ya mechi ya jana ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwezi uliopita.
Inadaiwa Isihaka alimtukana Mayanja kwenye chumba cha kubadilishia nguo Uwanja wa Taifa kabla ya mchezo huo wa michuano ya Kombe la Azam Sports Federation ambao SImba ilishinda 5-1. 
Siku moja baada ya kudaiwa kufanya kitendo hicho, Isihaka alisimamishwa kwa muda usiojulikana kabla ya mchezaji huyo kuomba radhi siku mbili baadaye.

SIMBA WAMETOA MAAMUZI YAO KUHUSU VIPORO VYA YANGA NA AZAM FC

Image result for haji manara


Na Haji balou

Klabu ya Simba imeweka msisitizo kwamba mechi ya Jumamosi dhidi ya Coastal Union ni ya mwisho kwao hawatacheza tena hadi Yanga na Azam FC wacheze mechi zao za viporo.

Simba itakuwa Tanga Jumamosi kuivaa Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mkuu wa kitengo cha habari cha Simba, Haji Manara ambaye jana alilizungumza hilo, leo amesisitiza kwamba watakuwa na msimamo huo kwa sababu kuu tatu.

“Moja, hakuna sababu ya timu nyingine kuwa na viporo hata baada ya kucheza mechi za kimataifa,” alisema Manara.

“Mbili, hakukuwa na sababu Yanga isicheze Jumatano. Baada ya sisi kucheza Tanga wao watakuwa na viporo vitatu, unafikiri tunaweza kumaliza ligi kugombea ubingwa kwa timu nyingine kuwa na michezo mitatu mkononi. Umewahi kuona kwenye ligi ipi makini duniani?”

“Tatu, kama zitabaki na viporo vitatu, timu nyingine zimeishacheza. Maana yake zipo ambazo zitakuwa zimeteremka daraja. Ushindani utakuwa hakuna tena, wakikutana nazo inakuwa ni rahisi sana kwao kushinda.”


Simba ndiyo ipo kileleni ikiwa na pointi 54, wakati Yanga na Azam FC ziko katika nafasi ya pili na tatu, kila moja ikiwa na pointi 50 na kila moja ina mechi mbili mkononi.

Mar 15, 2016

HASSAN KESY MAMBO SAFI SIMBA SC

Uongozi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umesema umefika mbali katika suala lake na beki wake, Hassan Kessy na una imani kubwa ataendelea kubaki na kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.

Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wameanza mazungumzo na Kessy na yako katika hatua nzuri sana.

“Tuko katika hatua nzuri sana ya mazungumzo. Tumeanza mazungumzo kipindi sasa na tuna matumaini makubwa Kessy ataendelea kubaki Simba,” alisema Kaburu katika mahojiano na SALEHJEMBE.

KESSY
“Tunaamini Kessy tunamhitaji, naye ni kijana anayeipenda Simba. Hivyo tukifikia makubaliano, tutaingia mkataba na kuwataarifu.”

Kumekuwa na taarifa huenda Kessy ana mpango wa kujiunga na Yanga hali iliyoonyesha kuwaudhi baadhi ya mashabiki wa Simba.


Hata hivyo kumekuwa na mgawanyiko kuhusiana na beki huyo wa kulia mwenye uwezo wa kupiga krosi nyingi. Wengine wakisema abaki na wengine wakikubali aende zake.

FA WAMEAMUA HIVI KUHUSU DIEGO COSTA

costa

Licha ya Barry kusema kwamba Diego Costa hakumng’ata kwenye mechi ya weekend iliypita, FA imemkuta Costa na makosa na wamempa hadi Alhamisi akatoe maelezo.
Diego Costa ameonekana aking’ata Barry kwenye mechi yao ambapo hadi alama za meno zilionekana kwenye picha video. FA imetoa statement kwamba, “Ni tabia isiyokubalika, baada kuonyeshwa kati ya pili ya njano na bado anaonyesha tabio isiyokubalika uwanjani. Hadi Alhamisi saa 12 jioni ndio muda aliopewa kutoa maeleozo”
Kwa hiyo hadi Alhamisi ambapo Costa atatoa maelezo kuhusu hili tatizo na chama cha soka cha England kitatoa hukumu yake juu ya Costa.

TFF YASOGEZA MBELE MECHI MBILI ZA YANGA NA AZAM FC

MECHI mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinazozihusu timu za Azam na Yanga zilizopangwa kufanyika mapema wki ijayo, zimeahirishwa.
Mechi hizo ni kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC Jumanne ya Machi 22 Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Yanga SC dhidi ya Mwadui FC Jumatano ya Machi 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwaka huu.
Sababu za kufutwa kwa mechi hizo ni kupisha ratiba ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
Kiungo wa Yanga, Deus Kaseke akipasua katikati ya wachezaji wa Azam FC, Serge Wawa (kulia) na Farid Mussa (kushoto)

taifa Stars itakuwa na mchezo wa kufuzu AFCON Kundi G dhidi ya Chad mjini N’jamena Machi 25, kabla ya timu hizo kurudiana Machi 28, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na baada ya mechi za mwishoni mwa wiki za michuano ya klabu barani, Afrika wachezaji wa Stars wanatarajiwa kukusanywa Jumapili kabla ya safari Jumanne kuelekea Chad.
Yanga SC baada ya ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya APR Jumamosi mjini Kigali, watarudiana na timu hiyo ya jeshi la Rwanda Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na Azam FC baada ya kushinda 3-0 mjini Johannesburg, Afrika Kusini dhidi ya wenyeji Bidvest Wits katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika, watarudiana na timu hiyo Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Pamoja na hayo, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kesho na mwishoni mwa wiki.
Azam FC wataikaribisha Stand United kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa Stand United ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 22 haina nafasi ya ubingwa na wala haimo kwenye hatari ya kushuka daraja, hivyo huo ni mchezo ambao hauwatii ‘presha’ hata kidogo.
Lakini Azam FC ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi zake 47 za mechi 20 katika mbio za ubingwa dhidi ya Yanga yenye pointi 50 za mechi 21 na Simba iliyo kileleni kwa pointi zake 54 za mechi 23 – inahitaji ushindi ili kujiimarisha.  
Simba itashuka tena dimbani Jumamosi kucheza na Coastal Union Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mar 12, 2016

HIKI NDIO KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHO IVAA BIDVEST

NA Haji balou
Kikosi cha timu ya Azam FC kitakachocheza dhidi ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Bidvest jijini Johannesburg leo kuanzia saa 1.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

28 Aishi Manula
  4 Shomari Kapombe
14 Ramadhan Singano
  6 Erasto Nyoni
  5 Pascal Wawa
13 Aggrey Morris
23 Himid Mao
29 Michael Bolou
  8 Salum Abubakar
19 John Bocco (C)
11 Didier Kavumbagu

AKIBA
1   Mwadini Ally
26 Wazir Salum
18 Frank Domayo
22 Khamis Mcha
12 David Mwantika
20 Mudathir Yahya
17 Farid Mussa

#VivaAzamFC

Mar 10, 2016

SIMBA KURUDI KILELENI LEO

NA Haji balou
SIMBA SC ina nafasi ya kurejea
kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara leo iwapo itashinda
dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Simba wanaikaribisha Ndanda leo
katika mfululizo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam wakihitaji
ushindi ili kuongoza ligi.

Na kocha wa Wekundu hao wa
Msimbazi, Mganda Jackson Mayanja amesema kwamba timu yake ipo vizuri baada ya maandalizi ya tangu Jumatatu wakiwa kambini nje kidogo ya mji ili wachezaji wapate utulivu.

Mar 9, 2016

PLUIJM APR NI WAZURI LAKINI TUTAPAMBANA

Na Haji balou
KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi
Hans van der Pluijm amesema
kwamba wanakwenda kwenye
mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya
APR, lakini watapambana wasipoteze.

Pluijm amesema kwamba mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, utakuwa mgumu kwa sababu APR ni timu nzuri.
“APR ni timu nzuri na watakuwa
wamejiandaa vizuri, lakini sisi tuko
vizuri, tutakwenda kupambana
tusipoteze mchezo, ili tumalizie vizuri
mchezo wa nyumbani,”amesema.
Yanga SC inatarajiwa kuondoka kesho nchini kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo huo, unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.

Mar 8, 2016

ULIMWENGU YUPO FITI KUCHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA CHAD

NA Haji balou
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa
Tanzania, Thomas Emmanuel
Ulimwengu (pichani) yuko fiti kabisa sasa na atakuja nchini
kuichezea nchi yake mechi mbili za
Kundi G kufuzu Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika mwakani.

Na klabu yake, Tout Puissant
Mazembe imemruhusu kuja Dar es
Salaam kuugana na Taifa Stars kwa
ajili ya michezo miwili ya nyumbani
na ugenini dhidi ya Chad.

TPM imemuambia Ulimwengu,
maarufu kama Rambo mbele ya
mashabiki wa Lubumbashi kwamba
atakwenda Dar es Salaam mara tu
baada ya mchezo wa marudiano wa
Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa
Afrika dhidi ya St George ya Ethiopia
Jumapili ya Machi 20 mjini Lubumbashi.

Taifa Stars watakuwa wageni wa
Chad Jumatano ya Machi 23 mjini
N'Djamena, kabla ya timu hizo
kurudiana Machi 28 mjini Dar es
Salaam.

Ulimwengu aliumia mguu akiichezea
Mazembe dhidi ya St Eloi Lupopo
Februari 17, mwaka huu katika Ligi
Kuu ya DRC timu hizo zikitoka sare
ya 0-0 na akacheza kwa dakika 12 za
mwisho huku akichechemea Februari 20 katika mchezo wa Super Cup ya CAF dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Lubumbashi, wenyeji
wakishinda 2-1.

MAHREZ ANAWEZA KUJIUNGA NA TIMU HII MSIMU UJAO

NA Haji balou
Leicester City wanaweza kuwa wamebakiwa na mechi 9 tu za kumuona star wao Riyad Mahrez
akifanya mazuri kwenye club hiyo. Ikifika muda wa usajili kutakua na vita kubwa kwa club mbalimbali kubwa kutaka kuchukua wachezaji
kutoka Leicester City ambao wanakikosi kizuri kwa ushirikiano na hata mchezaji kwa mmoja mmoja.

Boss wa Barcelona Luis Enrique amemuweka kwenye wish list yake mchezaji wa Leicester City ambapo angependa kumuona anajiunga na
club yake msimu ujao.

Hakuna mchezaji asiyependa kucheza na kikosi kinachoshinda makombe kama Barecelona.
Hivyo basi kutakua na hamu kubwa kwa Mahrez kutaka kujiunga na kikosi hicho ambapo atafaidika kiuchumi na kimchezo pia.

Taarifa zinasema kwamba Enrique
amemuangalia sana mchezaji huyu mwenye miaka 25 na kuvutiwa sana na style yake ya kufunga. Kipindi kijacho cha usajili kinategemewa kuwa na movement kubwa sana
ya wachezaji na makocha kwenda club mbali mbali.

Mar 7, 2016

AZAM KUIFUATA BIDVEST SAUZI

NA Haji balou
Azam FC inatarajia kuondoka nchini
Jumatano ya keshokutwa kuelekea Afrika Kusini ‘Sauz’ kupambana na Bidvest Wits lakini kocha wa timu hiyo, Muingereza, Stewart Hall ametamba kuwa anaondoka akiwa ameshanasa siri nyingi za kiufundi
za wapinzani wake hao.

Pamoja na hayo, Stewart amesema kuwa anafahamu ubora wa timu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili kwa sasa katika Ligi Kuu ya Sauz lakini amegundua silaha pekee ya kuwapunguza nguvu na pengine
kuwashinda kabisa ni kupata mabao ya ugenini kabla ya mchezo wao wa hapa nyumbani.

Azam itavaana na Wits Jumamosi hii huko Sauz katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili baadaye nchini Tanzania.

“Tutakwenda kule nikiwa tayari
nimeshaisoma Wits, nafahamu ni timu nzuri ikiwa ndani ya moja ya ligi bora za Afrika lakini nimefanikiwa kuona DVD zao tano pamoja na kutuma mtu akawaangalie kwenye mechi zao za ligi hivi karibuni,
kwa hiyo nimeshawasoma vizuri tu,”
alisema Stewart.

Mar 5, 2016

HIKI NDIO KIKOSI CHA AZAM KITAKACHOANZA MECHI YA LEO DHIDI YA YANGA

NA Haji balou
Kikosi cha Azam FC kitakakabiliana na Yanga dakika chache zijazo ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

28 Aishi Manula
  4 Shomari Kapombe
17 Farid Mussa
15 Said Morad
  5 Pascal Wawa
12 David Mwantika
16 Jean Mugiraneza
23 Himid Mao
14 Ramadhan Singano
18 John Bocco
10 Kipre Tchetche

AKIBA

  1 Mwadin Ally
26 Wazir Salum
29 Michael Bolou
18 Frank Domayo
20 Mudathir Yahya
  9 Allan Wanga
11 Didier Kavumbagu

#VivaAzamFC

VAN DER SAR AMEYASEMA HAYA KUHUSU VAN GAAL

NA Haji balou
Mchezaji  wa zamani wa Manchester united Edwin van der sar amesema kuwa kocha Luis van gaal ni mmoja kati ya makocha bora ambao yeye amewahi kufanya nao kazi hivyo anawataka mashabiki wa United kumwamini mholanzi huyo.

Van der sar alicheza chini ya Van gaal katika timu ya Ajax ya kwao uholanzi ambapo wote walishinda ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 1995 kabla ya kukaa miaka sita katika klabu ya Manchester united chini ya kocha Sir Alex Ferguson.

Van der sir aliongeza kuwa kwangu Van gaal ni kocha bora milele kwani alikuwa njia ya Mimi kupata mafanikio alitufunza mengi sana tukiwa kama wachezaji vijana.

Mar 4, 2016

HIVI NDIO VIWANGO VIPYA VYA SOKA MWEZI MARCH

Na Haji balou

List ya viwango vipya vya soka ulimwenguni imetangazwa March 3 2016, FIFA imetangaza viwango hivyo vya FIFA na nchi ya Ubelgiji
ambayo anacheza soka la kulipwa mtanzania Mbwana Samatta ipo nafasi ya kwanza ikufuatiwa na Argentina.

Tanzania ipo nafasi ya 125 ukilinganisha na miezi miwili nyuma ilikuwa 126 huku kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki Uganda imeendelea kuongoza kwa kushika nafasi ya 67 , Rwanda ipo nafasi ya 85 na Kenya ipo 103 ambapo kwa
Afrika nzima Ivory Coast ndio wanaongoza huku kwenye list ya dunia wakishika nafasi ya 36.
Hii hapa ndiyo orodha ya Fifa ya mataifa bora Afrika Machi 3 2016:

1. Visiwa vya Cape Verde
2. Ivory Coast
3. Algeria
4. Ghana
5. Tunisia
6. Senegal
7. Misri
8. DR Congo
9. Congo
10. Cameroon

MESSI APIGA TATU BARCA YAUWA 5-1 LA LIGA

NA Haji balou
BARCELONA imezidi kukimbia kivuli
chake katika Ligi Kuu ya Hispania,
maarufu kama La Liga baada ya
ushindi wa mabao 5-1 usiku huu dhidi ya wenyeji Rayo Vallecano Uwanja wa Rayo Vallecano mjini Madrid.

Mwanasoka bora kabisa kuwahi
kutokea duniani, Lionel Messi
amefunga mabao matatu peke yake
usiku huu katika dakika za 23, 53 na
72, huku mabao mengine ya Barca
yakifungwa na Ivan Rakitic dakika ya
22 na Arda Turan dakika ya 86.
Lionel Messi akishangilia baada ya
kuifungia mabao matatu peke yake
barceloma ikishinda 5-1 dhidi ya Rayo Vallecano katika La Liga.

Bao pekee Rayo Vallecano
limefungwa na mshambuliaji wa
kimataifa wa Angola, Manucho
Goncalves dakika ya 57 na sasa
Barca inafikisha pointi 66 baada ya
kucheza mechi 26 na kuendelea
kujinafasi kileleni mwa La Liga,
ikifuatiwa na Atletico Madrid yenye
pointi 61 za mechi 27 na Real Madrid
yenye pointi 57 za mechi 27 pia.
Rayo Vallecano inabaki na pointi zake 26 za mechi 26 na kuendelea kushika nafasi ya 16 katika ligi ya timu za 20.

Katika mchezo huo, Rayo
iliwapoteza wachezaji wake wawili
waliotolewa kwa kadi nyekundu, Diego Llorente aliyemchezea vibaya Rakitic dakika ya na Manuel Iturra
aliyemuangusha Luis Suarez kwenye
boksi. Lakini Suarez alikosa penalti
iliyotolewa baada ya kuangushwa
kwake.

Mar 3, 2016

BAADA YA ISIHAKA KUFUNGIWA SIMBA HAYA NDIO ALIYOSEMA HAMISI KIIZA

Na Haji balou


Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza naye yuko katika wakati mgumu baada ya kuandika mambo mtandaoni akionyesha kuupinga uongozi wa Simnba kumsimamisha nahodha wake, Hassan Isihaka.

Simba ilitangaza kumfungia Isihaka kwa muda usiojulikana kutokana na kitendo chake cha kumtolea mwalimu wake, Jackson Mayanja maneno yasiyo ya kiungwana.


Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza, Kiiza ameanza kujitetea akitupia lawama magazeti. Kwamba yaliandika na kumchafua Isihaka.

Lakini hali halisi inaonyesha haikuwa hivyo kwani yeye alianza kutupia mtandaoni hata kabla ya magazeti kuandika.

Presha imekuwa kubwa kwa Kiiza baada ya uongozi kumtaka aombe radhi. 

Lakini presha ikawa kubwa zaidi baada ya mhusika mwenyewe, Isihaka kuona amefanya kosa na kuamua kumuomba radhi kocha wake na uongozi.


Kiiza alitupia maneno kwenye mtandao wa Instagram akidai Isihaka anachafuliwa. Jambo lililoonyesha wazi alikuwa akiupinga uongozi. Lakini hakueleza kama alikuwa akiunga mkono nahodha huyo kinda amjibu kocha wake hovyohovyo.

ALICHOSEMA MANEGER WA HASSAN KESSY KUHUSU MKATABA MPYA SIMBA

Na Haji balou
Meneja wa Hassan Kessy amesema bado anahitaji mchezaji huyo aendelee kuitumikia Simba.
Athuman Tippo amesema Kessy hadi sasa ni mchezaji wa Simba ingawa mkataba wake unaendea ukingoni.

Lakini wanatoa nafasi kubwa kwa Simba kuingia naye tena mkataba kama wanamhitaji. “Ni suala la kukubaliana. Kama Simba watakuwa tayari, mimi naona ni vizuri  Kessy abaki Simba.

Hata hivyo itategemea tutafikiaje makubaliano,” alisema Tippo
mchezaji wa zamani wa Coastal Union na Milambo ya Tabora.
Kauli hiyo ya Tippo maarufu kama Zizzou Fashion inakuja siku moja baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja kusema Kessy kama ataendelea kusumbua kuhusiana na suala la kusaini,
basi anaweza akaenda zake.

MATOKEO YA MECHI ZA JANA LIGI KUU ENGLAND

TIMU ya Liverpool imeichapa mabao
3-0 Manchester City katika mchezo
wa Ligi Kuu ya England usiku huu
Uwanja wa Anfiled.

Ushindi huo ni sawa na kisasi cha
kufungwa kwa penalti 3-1 katika
fainali ya Kombe la Ligi, maarufu
kama Capital One Cup Februari 28,
Uwanja wa Wembley baada ya sare
ya 1-1.

Katika mchezo wa leo, mabao ya
Liverpool yamefungwa na Adam
Lallana dakika ya 34, James Milner
dakika ya 41 na Roberto Firmino
dakika ya 57.

Nyota wa Manchester United, Juan
Mata akidjangilia baada ya kuifungi
timu yake pekee katika ushindi wa 1-0 victory over Watford
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya
England usiku huu, Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga 1-0 Watford, bao pekee la Juan Mata dakika ya 83 Uwanja wa Old Trafford.

Arsenal imefungwa 2-1 nyumbani na
Swansea City Uwanja wa Emirates
katika mchezo mwigine wa ligi hiyo.
Mabao ya Swansea yamefungwa
na Wayne Routledge dakika ya 32
na Ashley Williams dakika ya 74,
wakati la Gunners limefungwa na Joel Campbell dakika ya 15.
Nahodha wa Swansea City
akimtungua kipa wa Arsenal, Petr
Cech katika mchezo wa Ligi ya
England baada ya krosi ya Gylfi
Sigurdsson Uwanja wa
Emirates.

Stoke City imeilaza 1-0 Newcastle
United, bao pekee la Xherdan Shaqiri
dakika y 80 Uwanja wa Britannia.

West Ham United imeilaza 1-0 Tottenham Hotspur, bao pekee la Michail Antonio dakika ya saba.