SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 6, 2015

Kurasa za #Magazeti leo MAY 6 2015 zimeamka na hizi kubwa

DSC02205 DSC02206 DSC02207 DSC02208 DSC02209 DSC02210

KAMARA ATUA DAR, JE ATAKWENDA TIMU GANI?

Kiungo Lansana Kamara (kushoto) akiwa na Meneja wake, Gibby Kalule baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa KImataifa wa Julius Nyerere (JKNI), Dar es Salaam jana. Mchezaji huyo raia wa Sierra Leone aliyekuwa anacheza Sweden, amekuja Tanzania kutafuta timu ya kuchezea na yuko tayari kwa majaribio.

MANNY PACQUIAO HATARINI KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA, AWEZA TUPWA JELA HADI MIAKA MINNE

BONDIA Manny Pacquiao anaweza kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa kutoorodhesha maumivu yake ya bega kwenye fomu maalum ya taarifa za bondia kabla ya pambano lake na Floyd Mayweather alilopoteza kwa pointi.
Pacquiao anaweza kuwa nje ya ulingo hadi mwaka mmoja wakati anajiandaa kwenda kufanyiwa upasuaji wa bega baada ya kuumia mazoezi akijiandaa na pambano hilo.
Lakini nyota huyo wa Ufilipino anaweza kuchukuliwa hatua kwa kusaini fomu ya maelezo muhimu ya bondia kabla ya pambano, bila kuorodhesha maumivu ya bega lake.
Manny Pacquiao pictured on Monday with his arm in a sling as he prepares to undergo surgery
Manny Pacquiao pichani jana akiwa amefungwa mkono wakati akijiandaa kwenda kufanyiwa upasuaji
Pacquiao's pre-fight questionnaire which shows he did not disclose his shoulder injury
Fomu ya maelezo muhimu ya Pacquiao kabla ya pambano haikuorodhesha maumivu ya bega lake

BIN ZUBEIRY imeipata nakala ya fomu ya maelezo muhimu ya bondia kabla ya pambano, ambayo inaonyesha kwamba Pacquiao alitumia dawa kadhaa za maumivu.
Aidha, neno hapa likiwa linafuatia limepigiwa mstari baada ya swali; ‘Ulikuwa una maumivu yoyote kwenye mabega yako, chini ya mabega, au mikononi ambayo yanahitaji vipimo vya uthibitisho wa kupona?’
Kwa kusaini fomu hiyo, wote Pacquiao na mshauri wake Michael Koncz wanaweza kuchukuliwa hatua kwa sababu, mwishoni kuna maelezo yasemamo; "Maelezo ya hapo juu ni kweli na sahihi nikiwa na akili zangu timamu,".
Adhabu ya kosa hilo kwa kawaida huwa ni kufungwa jela kati ya mwaka mmoja na minne na kutozwa faini hadi dola za Kimarekani 5,000 (Sh. Milioni 20). Pacquiao anaweza pia kutozwa faini na kufungiwa na Kamisheni ya Michezo Nevada.
Mwenyekiti wa Kamisheni, Francisco Aguilar amesema kwamba ofisi ya Mwanasheria Mkuu itachunguza kwa nini maumivu hayo hayakuorodheshwa.
"Na tutafanya majadiliano fulani. Kwa sababu Kamisheni inapaswa kupata maelezo ya kila wakati ya bondia. Tiba aliyopata iliorodheshwa kwenye fomu, lakini si ya maumivu halisi. Hili si pambano letu la kwanza. Hii ni biashara yetu. Kuna utaratibu, na unapojaribu kukiuka utaratibu, hatuwezi kufanya kazi na wewe,"amesema.
It was a boxing masterclass from Floyd Mayweather as he beat his great pound-for-pound rival in Las Vegas
Floyd Mayweather alipigana kwa ustadi wa hali ya juu dhidi ya mpinzani wake huyo mjini Las Vegas

TEVEZ AWAONDOA ‘VICHWA CHINI’ REAL TURIN, JUVE YANG’ARA NYUMBANI 2-1

REAL Madrid wameanza vibaya Nusu Fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji Juventus Uwanja wa Juventus mjini Turin usiku wa jana.
Real sasa itahitaji ushindi wa 1-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Madrid ili kuking’oa ‘Kibibi Kizee cha Turin’ katika michuano hiyo na kwenda kutetea taji lake.
Alvaro Morata alianza kuwafungia Juventus dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 27.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amefikisha mabao 76 na sasa ndiye anayeongoza kwa kufunga katika historia ya mashindano hayo.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester zote, United na City, Muargentina Carlos Tevez aliifungia bao la ushindi Juve kwa penalti dakika ya 57 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Dani Carvajal.
Tevez wheels away in celebration after restoring the Old Lady's lead from the penalty spot against the current Champions League holders
Tevez akishangilia baada ya kuifungia bao la uishindi Juventus dhidi ya mabingwa watetezi, Real Madrid usiku wa jana