SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 20, 2015

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA LEO 20 FEB

.
DSC09703
.
.
.
.
.
.
.
.
.

BALOTELLI AING’ARISHA LIVERPOOL DAKIKA ZA MWISHO

BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Italia, 
Mario Balotelli limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Besiktas katika mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora Europa League Uwanja wa Anfield usiku wa jana.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City, Inter Milan na AC Milan, alifunga bao hilo kwa penalti dakika ya 85, kufuatia winga Jordon Ibe kuchezewa faulo kwenye eneo la hatari.
Mtaliano huyo alimpokonya mpira Nahodha Jordan Henderson na ‘akazinguana’ na Daniel Sturridge kabla ya kwenda kupiga.
Mapema, Demba Ba na Adam Lallana walipoteza nafasi nzuri za kufunga kwa kila timu na baada ya ushindi huo mwembamba Anfield, Liverpool inajiweka katika mazingira magumu kuelekea mchezo wa marudiano nchini Uturuki Alhamisi ijayo.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Ibe, Henderson, Allen/Lovren dk63, Moreno, Lallana/Sterling dk77, Sturridge na Coutinho/Balotelli dk63.
Besiktas: Gonen, Kurtulus, Franco, Gulum, Ramon, Hutchinson, Kavlak, Tore, Sosa/Ozyakup dk60, Sahan/Frei dk72 na Ba.
Balotelli celebrates in front of the Liverpool fans after converting from the spot to give his side a narrow victory
Balotelli akishangilia 'kigumu' mbele ya mashabiki wa Liverpool baada ya kufunga 
 Balotelli took the ball off Liverpool captain Jordan Henderson and fellow striker Daniel Sturridge to take the penalty
 Liverpool midfielder Lallana (centre) watches his effort go wide as Daniel Sturridge (right) watches on


ALICHOSEMA MSUVA BAADA KUIFUNGA PRISONS


Msuva..Na. Richard Bakana, Dar Es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans, Simon Msuvu baada ya kufanikiwa kuipandisha timu yake katika kilele cha ligi hiyo kwa kuifungia mabao mawili kati ya matatu katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, mshambuliaji huyo amefunguka na kudai kuwa anajisikia vizuri anapopangwa kucheza na Ngassa au Sherman.
Akizungumza na Shaffihdauda.com baada ya mchezo huo, Alipoulizw nani kati ya nyota hao wawili anawakubali akicheza nao, Msuva amesema kuwa yeye ni mchezaji hivyo haweze kuchagua nani wa kucheza naye lakini akipangwa na yoyote kati ya Mrisho Ngassa na Khap Sherman lazima atekeleze majukumu yake kama mchezaji.
“ Ah hiyo ni kazi ya mwalimu, yeye ndio anajua amuanzishe nani asimuanzishe nani, hayo ni majukumu yake, Mimi mtu yoyote nitakayepewa nicheze naye nacheza naye” Amesema Simon Msuva amabye ameibuku shujaa kwa kifumania nyavu mara mbili akiiteketeza Prisons katika uwanja wao wa Nyumbani Sokoine, Jijini Mbeya.
Akizungumzia mchezo huo kwa ujumla Msva amewasifia Prisons kwa kusema kuwa ni timu nzuri lakini baadhi ya makosa madogo madogo ndio yaliyowagharimu hadi wao kuibuka na pointi tatu na mabao matatu.
“Prisons ni timu nzuri sio kwamba ni timu mbovu, sema makosa ambayo wao wliyateda sisi ndio tuliyatumia na ndio maana tumeweza kutoka na ushindi” Amemalizia Msuva.
Katika mchezo huo Yanga ilipata bao la kwanza katika dakika ya 3 kupitia kwa Simon Msuva ambaye aliunganisha kona safi kutoka kwa Mbrazil Andrey Coutinho, Dakika nane baadaye Beki wa Prisons Lugano Mwagama, akaiandikia Yanga bao lapili akiwa katika harakati za kuokoa shuti kali lililopigwa na Coutinho na kumbabatiza na kuingia langoni, hadi dakia 45 za kwanza zinamalizika Yanga walikuwa wakiongoza kwa bao 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Prisons wakitengeneza nafasi za mapema lakini wakashindwa kuzitumia, Kunako dakika ya 62 kwa mara nyingine Msuva akaiandikia Yanga bao la tatu baada ya kuunganisha kona iliyochongwa na Andrey Coutinho na kufanya hadi dakika 90 zinakatika Yanga 3 Prisons 0.