SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 4, 2015

STEPHEN KESHI KUTUA AZAM FC

keshi1Na, Richard Bakana, Dar Es Salaam
Baada ya kumfungashia vilango vyake aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Azama FC, Mcameroon, Joseph Omog, Sasa wanalambalamba hao wapo kwenye mpango wa kumpatia mikoba hiyo Stephen Keshi aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Nigeria.
Akizungumza  na Shaffihdauda.com Katibu mkuu wa Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara, Idrissa Nasoro, Amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na Keshi, ikiwezekana kuchukua nafasi ya Omog aliyetundikiwa daruga wiki hii.
“Tunatafuta kocha wa kusaidiana na George Best Nsimbe, Stephen Keshi tunawasiliana naye vizuri tu, lakini sio kwamba ndio atakuwa kocha wetu, bado tunaendelea kutafuta kocha atakae tufaa, Hapo badaye tutaweka wazi” Amesema Idrissa Nasorro.
Juzi uongozi wa klabu ya Azam FC, ulitangaza kuachana na kocha wake mkuu, Joseph Omog ambaye ameweka historia ya kuwa kocha wa kwanza kuipatia timu hiyo kikombe cha Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiwa ni siku  moja tu, baada ya kutua nchini wakitokea Sudan, kucheza na El Marreikh na kutolewa kwenye michuano ya klabu Bingwa kwa jumla ya Mabao 3-2.
Katika Mkataba wa Joseph Omog na Azam FC kulikuwa na kipengere kilichokuwa kinasema kuwa, Omog lazima ahakikishe anaifikisha timu hiyo katika hatua ya Makundi ya michuano ya Klabu Bingwa zaidi ya hapo atakuwa amejivunjia Mkataba wake.

VAN GAAL AWAZUIA MABEKI KUMRUDISHIA MIPIRA DE GEA

BAADA ya mashabiki wa Manchester United kuwazomea wachezaji wa timu hiyo katika mechi ya jumamosi iliyopita dhidi paka weusi Sunderland, kocha Louis Van Gaal amekuja juu na kuwataka wachezaji wake kutorudisha mpira mara kwa mara kwa kipa David de gea.
Mashabiki hao waliokuwepo katika mechi hiyo iliyopigwa katika uwanja wa Old Trafford, waliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuonekana kukasirishwa na kuchoshwa na wachezaji wao kutofanya mashambulizi na kurudisha mpira mara kwa mara kwa kipa wa timu hiyo.

"Ninakubaliana na mashabiki, hatutakiwi kumtumia kipa mara kwa mara. Kuna muda tunapata nafasi ya kushambulia lakini hatufanyi hivyo, tunamchosha De gea " alisema Van Gaal.
Kocha huyo raia wa uholanzi,leo anakibarua kizito kukiongoza kikosi chake kitakaposhuka dimbani katika uwanja wa St.James Park kuwavaa Newcastle United ambao wamekuwa katika kiwango kizuri kwa mechi za hivi karibuni.
Manchester United inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ikiwa  imejikusanyia pointi 50 katika michezo 27 waliyocheza mpaka sasa kunako ligi hiyo.

AZAM FC YAANZA KUSAKA KOCHA MSAIDIZI, BEST AWE BOSI MKUU


Uongozi wa Azam FC, umeanza juhudi za kusaka kocha msaidizi kwa ajili ya kikosi chao.

George ‘Best’ Nsimbe amepewa nafasi ya kuendelea kama kocha mkuu, huku kocha msaidizi akitafutwa.

Habari za uhakika kutoka Azam FC zimeeleza kuwa tayari juhudi za kumsaka kocha msaidizi zimeanza.

"Kweli kuna makocha kadhaa ambao tunafanya nao mazungumzo, Best ndiye atakuwa kocha mkuu," kilieleza chanzo cha uhakika.
Best raia wa Uganda amechukua nafasi ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Joseph Omog raia wa Cameroon.
Uongozi wa Azam FC, umeonekana kuwa na nafasi nzuri ya kumuachia Best achukue jahazi hilo.

Omog ametimuliwa kibarua baada ya Azam FC kung’olewa na El Merreikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 3-2.

MTIBWA SUGAR IMEAMKA NA KUFANIKIWA KUITWANGA POLISI

Baada ya wakati mgumu wa kufungwa mfululizo hatimaye Mtibwa Sugar imerejea katika listi ya ushindi.


Mtibwa Sugar imeifunga Polisi Moro kwa mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Manungu mjini Turiani.

Polisi ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia Said Bahanuzi katika dakika ya 41 likadumu hadi mapumziko.

Lakini kipindi cha pili kilikuwa cha Mtibwa Sugar ambayo ilifunga mabao yake kupitia Ali Shomari katika dakika ya 53 na Said Mkopi akamaliza kazi katika dakika ya 79.

Kwa ushindi huo, sasa Mtibwa Sugar imefanikiwa kufikisha pointi 22.

MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI SIMBA ASEMA JERRY MURO MGENI KATIKA SOKA

TULLY (KULIA) AKIZUNGUMZA NA KOCHA WA ORLANDO PIRATES WAKATI SIMBA ILIPOKUWA KAMBINI NCHINI AFRIKA KUSINI, MWISHONI MWA MWAKA JANA.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully amesema mpira umeingiliwa kwa kuwa wanacholalamika Yanga ni sawa na kichekesho.



Ingawa hajawaweka wazi, Tully ameonyesha kulenga maneno yaliyozungumzwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro aliyesema kuwa Simba ilimchezesha mshambuliaji Ibrahim Ajibu 'Kadra' katika mechi dhidi  ya Prisons.

"Nashangazwa sana na kauli, watu wanazungumza, hawajui lolote. Ili mradi tu wanasema, suala la Ajibu lilipitia taratibu zote viongozi wa Yanga wanajua.

"Sasa unasikia mtu anasema mambo ambayo yanashangaza kabisa kuonyesha hajui lolote kuhusu soka, nasema amevamia huku maana watu wa mpira tunajuana," alisema Tully.

Kabla, Muro alitoa malalamiko kuwa Simba ilimchezesha Ajibu ikijua ana kadi tatu za njano jambo si sahihi.

Lakini Simba ikatoa ufafanuzi kutumia kanuni mpya zinazoruhusu kuchagua mchezaji asicheze katika mechi ipi kutokana na uchaguzi wao.

Naye Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto akalifafanua hilo kwa kusema hakuna kosa lolote kwa kuwa mkutano wa pamoja wa viongozi wa klabu, TFF na Bodi ya Ligi ulipitisha kanuni hizo mpya.


MAKOMBE 15 MIKONONI MWA TERRY, ANASUBIRI LA 16

Na Saleh Ally
OKTOBA 28, 1998 beki John Terry akiwa kinda aliingia uwanjani kuichezea Chelsea mechi yake ya kwanza ikipambana na Aston Villa katika mechi ya Kombe la Ligi.

Miaka 10 baadaye, ilikuwa 2008, Terry akawa adui baada ya kuteleza na kukosa penalti ya mwisho katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Moscow, Urusi dhidi ya Manchester United.
Maisha yanasonga, mengi yanapita lakini kibaya kinaweza kubadilika na kuwa kizuri kama mhusika anajitambua. Hakuna anayeweza kukataa kwamba kweli Terry maarufu kama JT sasa ni shujaa wa Chelsea.
Beki ambaye atakumbukwa, nahodha ambaye atakuwa gumzo kwa kipindi kirefu baada ya kustaafu. Sasa anasonga ukiongoni akiwa na miaka 34, lakini anaendelea kuibebesha Chelsea vikombe na mikono yake ndiyo mpokeaji mkuu.

Alianza kujihakikishia namba katika kikosi cha Chelsea katika msimu wa 2000-01, alipocheza mechi 23 zote akianza. Msimu uliofuata akawa tegemeo akishirikiana na Marcel Desailly na Desemba 5, 2001, rasmi akakabidhiwa unahodha.
Miaka 14 sasa tokea amekuwa nahodha wa kikosi cha Chelsea, tayari JT ana makombe 14 mkononi mwaka aliyoshinda akiwa na klabu yake hiyo ya Chelsea.
Hauwezi ukamzungumzia JT bila ya utukutu na kashfa lukuki, mwaka 2002 akizichapa na baunsa, wakamchangia na mwisho akapandishwa kizimbani. Miezi michache baadaye akakutana na kashfa nyingine ya kumdhalilisha mtalii wa Kimarekani, ikawa kesi nyingine.

Usisahau, JT aliingia katika kashfa ya kutembea na mpenzi wa mshikaji wake kitambo, beki Wayne Bridge. Hiyo haitoshi, akambagua Anton Ferdinand na kusababisha ugomvi mkubwa kati yake na aliyekuwa mshikaji wake, Rio Ferdinand.
Kwa kifupi, JT ni mtukutu hasa lakini unaporudi kazini, JT ni kati ya mabeki bora zaidi England hadi msimu huu kwa kuwa Chelsea inapambana kupata ubingwa wa Ligi Kuu England na kama itashinda, atakuwa amebeba kombe la 16.
Maana yake JT tayari ameweka rekodi mpya katika mikono yake ya unahodha wa miaka 14 na makombe 15 aliyoyashika.

Nani anaweza kusema JT hajitumi, si mbunifu au si makini? Ubora wa kazi zake unafuta makosa na utukutu wake wote na ndivyo binadamu wanavyoishi, kwamba wakati mwingine vizuri kuangalia katika mazuri ya mtu kuliko kujali zaidi makosa.
Makombe la Ligi ya Mabingwa, Europa, Ligi Kuu England, FA, Kombe la Ligi na mengine. Mchezaji yupi wa nyumbani Tanzania anawaza atakuwa amefanya nini wakati soka lake litakapokuwa limefikia ukingoni?
Inawezekana kukawa na tofauti kubwa kati ya Ibrahim Ajibu wa Simba na JT. Kweli kinda huyo wa Simba, ndoto yake kuwa na gari kali ikiwezekana nyumba pia, lakini mafanikio makubwa yanajenga kila kitu na gari na nyumba, zenyewe zinamfuata, tena anachagua.
Mchezaji yupi kinda au anayefanya vizuri wa Yanga, Azam FC, Coastal Union na kwingine anayeamini kama mafanikio hayajakaa vizuri katika timu anayochezea, anaweza kutoka nje ya Tanzania na kubadilisha mambo? Alipo, ndipo alipo na amefika! Vipi atafikia alipofikia JT?
Wachezaji nao ni mashabiki, kazi yao kusifia vinavyofanywa na wenzao wakati wao hawafanyi lolote. JT angeweza kufanya hivyo, lakini hawezi kwa kuwa alikuwa anataka kufanya zaidi ya alivyotaka kufanya. JT tayari ana makombe hayo 15, anatafuta la 16. Wewe je?
MAKOMBE NA KLABU:
3 – Ligi Kuu England: 2004–05, 2005–06, 2009–10
5 - FA Cup: 1999–00, 2006–07, 2008–09, 2009–10, 2011–12
3 – Kombe la Ligi: 2004–05, 2006–07, 2014–15
1 – Ligi ya Mabingwa Ulaya: 2011–12
1 - Europa League: 2012–13
2 – Ngao ya Jamii: 2005, 2009
VIKOMBE BINAFSI:
1 – Mchezaji wa mwaka wa PFA: 2004–05
3 – Mchezaji katika kikosi cha mwaka cha PFA: 2003–04, 2004–05, 2005–06
2 – Mchezaji wa mwaka Chelsea: 2001, 2006
1 – Ndani ya kikosi Bora cha Kombe la Dunia: 2006
5 – Mchezaji bora wa FIFPro World XI: 2005, 2006, 2007, 2008, 2009
3 – Beki bora wa klabu wa UEFA: 2005, 2008, 2009

4 – Timu bora ya mwaka ya UEFA: 2005, 2007, 2008, 2009

MBEYA CITY WAFUNGUKA KUHUSIANA NA VIPIGO VYAO


Licha ya kutokuwa na kasi kama msimu uliopita, klabu ya Mbeya City imefunguka kuwa matokeo wanayopata kwa sasa ni kawaida kwa sababu hakuna timu ambayo inaweza kushinda kila mchezo.

Timu hiyo msimu uliopita ilikuwa moto na kuweza kufanya vyema huku ikimaliza katika nafasi ya tatu na kuweza kuwafunika baadhi ya wakongwe kama Simba, Coastal Union na Kagera Sugar.
Mbeya City kwa sasa inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 168 tu kwenye msimamo wa ligi.
Msemaji wa Mbeya City, Mohammed Kisanda maarufu kama Dismas Ten, alisema kikosi chao kipo vizuri lakini kwa sasa ni upepo tu unapita, mambo yatakuwa mazuri.
“Timu si kama inafanya vibaya sana, ni matokeo ya kawaida, hakuna timu ambayo kila siku inashinda kila mchezo, kuna sare, kufunga na kufungwa, watu walitambue hilo na wawe na subira.


“Tunapambana kuhakikisha tunarudi katika mstari kwa kushirikiana vyema na benchi la ufundi na bado hatujakata tamaa, tunajipanga na tutafanya vyema japo ligi ya msimu huu imekuwa na changamoto tofauti na ile iliyopita,” alisema Dismas.
04 Mar 2015

IVO; BEKI AKIZINGUA ANAKULA NGUMI


Kipa namba moja wa Simba, Ivo Mapunda, amewapa onyo la mwisho mabeki wake na kuwaambia kuwa wawe makini kwa dakika zote 90.

Kipa huyo mzoefu amesema mabeki hao wanatakiwa kuacha kufanya makosa ya kizembe, la sivyo ataenda mbali zaidi kwa kuwaonya kwa kuwapiga ngumi.

Katika mechi dhidi ya Stand, kipa huyo alitaka kuwapiga mabeki wake baada ya kufanya makosa mara kadhaa.
Ivo alisema kuwa katika mechi nyingi, amekuwa akiwaona mabeki wake wakijisahau katika ukabaji na kufanya makosa mengi ya kizembe, kitu ambacho kinaweza kuigharimu timu na kuiweka kwenye nafasi mbaya.

 “Inafikia kipindi namuonya beki aliyefanya makosa kwa kumsukuma ila naona makosa bado yanafanyika, kama wakiendelea hivi hata ngumi nitakuwa nawapiga, makosa wanayoyafanya ni ya hatari, kama wakiyafanya kwenye mechi dhidi ya timu inayojua kuyatumia vyema, basi tunaweza kufungwa kirahisi,” alisema Mapunda.

BEKI MGANDA SIMBA AWATUMIA SALAMU YANGA


Kitasa Mganda wa Simba, Juuko Murshid, ameibuka na kuitahadharisha safu ya ushambuliaji ya Yanga na kusema hawapati kitu.

Beki huyo ametoa onyo hilo zikiwa ni siku chache zimebaki kabla timu hizo hazijaumana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Jumapili hii.
Murshid amesema anajua mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na timu zinazokutana lakini akasisitiza kuwa, siku hiyo kazi yake ni kucheza na mafowadi wa Yanga pekee kuhakikisha hawaleti usumbufu hata kidogo.

“Mchezo utakuwa mgumu ila nikuhakikishie kwamba tutashinda, lakini kama nitacheza hiyo mechi kazi yangu kubwa siku hiyo nitahakikisha hakuna fowadi wa Yanga anayeleta usumbufu wa kufunga bao hata moja.


“Nafahamu kuwa wana rekodi na mwenendo mzuri wa kufunga katika mechi za hivi karibuni lakini hilo halinisumbui kwa kuwa safu yetu ya ulinzi ipo vizuri na tumejiandaa vya kutosha katika kupambana kuhakikisha tunaendeleza ushindi,” alisema Murshi

SIMBA YAMFUKUZIA NDUGU YAKE TWITE

MBUYU (KUSHOTO) NA KABANGE WAKATI WAKIICHEZEA APR YA RWANDA.
Jina la nahodha na kiungo mkabaji wa FC Lupopo ya Kongo, Kabange Twite, limetajwa kwenye orodha ya wachezaji anaowataka Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic, kwenye usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.


Awali, kiungo huyo ambaye ni pacha wa kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, alitakiwa kutua Jangwani misimu miwili iliyopita ya Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya kamati ya usajili ya timu hiyo, kocha huyo Mserbia ndiye ametoa mapendekezo ya  uongozi kuhakikisha wanamsajili kiungo huyo msimu ujao.

Chanzo hicho kilisema, kocha huyo hivi sasa yupo kwenye mazungumzo ya awali na Kabange anayemudu kucheza namba sita inayochezwa na Jonas Mkude ndani ya uwanja.

“Kocha ametoa mapendekezo ya kumsajili Kabange kutokana na kumjua akiwa anaifundisha Polisi Rwanda na kiungo akiwa anaichezea APR ya inayoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda.

“Hivyo kocha huyo anaendelea na mazungumzo na kiungo huyo kwa ajili ya kumsajili katika msimu ujao, atamsajili Kabange baada ya kuona upungufu kwenye kikosi chake kwenye safu hiyo ya kiungo,”kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa pacha wa mchezaji huyo Mbuyu kuzungumzia hilo alisema kuwa “Ni kweli kabisa yapo mazungumzo ya awali yanayoendelea kati ya Kabange na kocha wa Simba kwa ajili ya kuja kuichezea timu hiyo.


“Asilimia ni kubwa ya Kabange kutua kuichezea Simba, kwa sababu huyo kocha mpya wa Simba anamjua vizuri Kabange, aliwahi kuifundisha Polisi Rwanda, hivyo anaujua vizuri uwezo wa Kabange,”alisema Twite.

YANGA YAWEKA KAMBI BAGAMOYO KUSAKA POINTI TATU DHIDI YA SIMBA


Katika kuhakikisha timu yao inafanya mazoezi kwenye hali tulivu na salama, Yanga wamejificha kwenye eneo lenye msitu mkubwa huku kukiwa na siafu wengi.

Yanga wanajiwinda na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili ijayo.

Yanga yenyewe iliyoweka kambi yake kwenye hoteli moja Bagamoyo huko Pwani, inatoka umbali mrefu kuufuata uwanja ambao umezungukwa na pori kubwa huku kukiwa na milio ya ndege tu.
Kufika kwenye uwanja huo ni shughuli pevu kwani hakuna gari lolote linaloweza kufika huko zaidi ya pikipiki, hali iliyosababisha kuwa na mashabiki wachache sana.

Katika mazoezi ya jana asubuhi yaliyofanyika kwenye uwanja huo, watazamaji wakubwa waliokuwa wakifuatilia mazoezi hayo yaliyoongozwa na kocha msaidizi Charles Mkwasa ni wanafunzi pekee wa chuo hicho wanaofikia 15.

Kubwa kuliko yote, uwanja huo umezungukwa na wadudu aina ya siafu ambao kama ukisimama au kukaa, lazima watakutambaa kutokana na mazingira ya msitu uliouzunguka uwanja huo.

ZIPO HAPA KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO LEO MARCH 4

.
.
.
.
.
.
.