SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 21, 2015

BONGO MOVIE WAANZISHA TAWI LA YANGA

UWOYA
Hili ni tawi jipya linaloisapoti klabu ya Yanga  mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015. Tawi hili kwa sasa ndio limeanzishwa na tayari lina viongozi wa muda ambao wataliongoza  kwa muda pia ili liweze kufikia malengo yake na ya klabu ya Yanga kufika mbali zaidi.
Kundi ili linaongozwa na viongozi wa muda ambao ni
Mwenyekiti wa tawi…..Mike Sangu
Makamu mwenyekiti…….Catty Lupia
Katibu mkuu…………….Jimmy Mafufu
Mtunza fedha…………..Mayasa Mrisho
Kundi hili lina wanachama wengi sana ambao ni wafanyakazi wa kiwanda cha filamu kwa namna moja au nyingine yaani na wadau wa filamu wamo pia. Hadi sasa wanachama ni Vincent kigosi ‘Ray’,  Irene Uwoya,  Mariamu Ismail,  Barafu Suleiman , Saguda George, Haji Mboto, Haji Adam, Chopamchopanga, Jimmy mafufu (katibu mkuu),Lissa Stella , Issa Mussa (Claud), Dullu Mngullu, Idrissa Makupa…Mr. Kupa, Catthy Lupia (makamu mwenyekiti), Mayasa Mrisho (Mtunza fedha),Stanley msungu, Mr Mo, Mike Sangu (mwenyekiti), Stella Nadya , Jini Kabula, Steve Nyerere , Marry Mawigi , Zahoro China  na Badra
Orodha  ni kubwa sana na hata baadhi ya wanamuziki wa dansi wamo pamoja na bongoflevar.Mengi tutawajuza kadili mambo yatakavyokuwa yanakwenda na lini kikao cha pamoja kitakaa.

MFUNGAJI BORA KAGERA ASAINI MWADUI

Mandawa zawadi
Mandawa (wa pili kushoto) alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu soka Tanzania bara mwezi Novemba mwaka jana
MWADUI FC imetia chumvi kwenye kidonda cha Kagera Sugar baada ya kuinasa saini ya mfungaji hatari wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015, Rashid Mandawa.
Mandawa aliyefunga magoli 10 msimu wa ligi kuu uliomalizika mei 9 mwaka huu,  leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia matajiri wa madini mkoani Shinyanga, Mwadui fc.
Wakati huo huo, kocha mkuu wa klabu hiyo ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Coastal Union, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ ameongeza mkataba wa miaka mitatu (3) kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Julio pia alikuwa anawania na Wagosi wa Kaya baada ya kufaniikiwa kuwanusuru kushuka daraja.
Siku za karibuni, Mwadui ilimsajili Malegesi Mwanga kutoka Kagera Sugar, hivyo ni pigo lingine kubwa kwa ‘Wanankurukumbi’ wenye maskani yao uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Kabla ya kujiunga na Mwadui, Mandawa alikuwa anaripotiwa kuwindwa na Simba.
Pia alikuwa na mpango wa kwenda kufanya majaribo katika klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
                   CLICK   HOME KWA HABARI ZAIDI ZA KIMICHEZO

JUMA MWAMBUSI ATAJA KIKOSI BORA LIGI KUU VPL 2014/2015


mwambutsi-jumaKocha mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi
TUNAENDELEA na zoezi letu la kuangalia vikosi bora vya makocha wa timu za ligi kuu soka Tanzania bara, makocha wasiokuwa na timu na wachambuzi wa soka kwa msimu wa ligi kuu wa 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu,  Yanga wakiibuka mabingwa, Azam nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu na Mbeya City nafasi ya nne.
Siku mbili zilizopita tumeweza kukuletea kikosi bora cha kocha wa Yanga , Hans van der Pluijm na Coastal Union, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, lakini leo tunakuletea kikosi bora cha msimu kilichopendekezwa na kocha bora wa msimu wa 2013/2014, Juma Mwambusi.
Kwanza Mwambusi amesema: “Ligi ilikuwa ngumu, kama unavyojua mwaka jana tuliingia na changamoto mpya na msimu uliomalizika (2014/2015) timu zilijidhatiti sana. Lakini kama mwalimu pamoja na kucheza mechi ngumu, mtazamo wangu ulikuwa kuangalia wachezaji ambao ninaweza kuwapendekeza katika kikosi ambacho kinaweza kucheza timu yoyote na  kuleta mafanikio”.
HIKI NDICHO KIKOSI BORA CHA VPL 2014/2015 KILICHOPENDEKEZWA NA JUMA MWAMBUSI
  1. Hanington Kalisebula (Mbeya City)
  2. Hassan Ramadhan Kessy (Simba)
  3. Hassan Mwasapili (Mbeya City)
  4. Serge Paschal Wawa (Azam fc)
  5. Salim Mbonde (Mtibwa Sugar)
  6. Steven Mazanda (Mbeya City)
  7. Simon Msuva (Yanga)
  8. Haruna Niyonzima (Yanga)
  9. Paul Nonga (Mbeya City)
  10. Amissi Tambwe (Yanga)
  11. Emmanuel Okwi (Simba)

PART 3 : ADEBAYOR KATUPA TENA STORY YA FAMILIA YAKE…WALITAKA KUMUUA KISA PESA.

kola
Hii ni sehemu kidogo ya status ya Adebayor kuhusu kaka yake Kola
Leo nimeamua kuleta part 3 ya story yangu. Hii ni kwasababu kaka yangu Kola Adebayor na ndugu zangu wameamua kuzungumzia mambo ya familia kwenye social media, kutuma baria kwenda kwenye club na radio. Ningeweza kuandika kitabu na kuuza lakini nimeamua ku-share na wewe hapa.
Miaka 25 iliyopita kaka yangu mkubwa Kola alienda ujerumani na kuwa tumaini kubwa kwa familia yetu. Wote tuliamini angeweza kubadilisha maisha ya familia yetu. Miaka baada ya yeye kuondoka Togo bado hatukua na umeme wala simu, Kama angetaka kuongea na sisi alikua anapiga simu kwenye hotel inaitwa Atlantic Hotel ambayo ilikua karibu na nyumbani kwetu.
Nilivyopata nafasi ya kwenda kucheza mpira France kwa mara ya kwanza, tuliitaji pesa kwa ajili ya ticket ya ndege na gharama nyingine. Kaka yangu hakupatikana kusaidia katika hili, mungu pekee anajua alichokua anakifanya huko Ujerumani.
Nilivyofika Ujerumani nilijaza makaratasi yote na timu ikaniruhusu kukaa kwenye academy. Baada ya miezi michache Kola akataka kunitembelea, nilikua nakaribia kuishiwa na pesa na nilikua naishi kwenye academy. Kwa hiyo nikaamua kuazima pesa ili kulipia hotel yake. Wakati huo mchezaji mwenzangu Sega N’diaye kutoka Cameroon alikua na pesa za kutosha akaniazima pesa. Pia ikabidi niazime pesa zaidi ili niweze kumpa Kola atumie kwenye safari yake ya kurudi Ujerumani.
Baada ya miaka michache mambo yakaanza kwenda vizuri, nashukuru mungu nikasaini mkataba na Mets.Tangu siku hiyo kaka yangu alikua anawasiliana na mimi muda wote ukifika muda wa kulipia bili zake za mwezi.Kuna muda alikua anasema kwamba mwanae anaumwa, so ikabidi nizoee tu
Nikawa na bahati zaidi ya kupata ofa kutoka Monaco na nikasaini mkataba nao. SIku moja Kola na marehemu Peter walikuja kunitembelea Monaco. Kaka zangu hawa wawili hawakuniambia kama walikua wanakuja. Lakini damu nzito kuliko maji nikawapokea. Walifika asubui sana mimi nikiwa naelekea kwenye mazoezi.Nilivyorudi tulikua na mazungumzo na walisema wanataka kuanzisha biashara ya magari. Ki ukweli biashara hiyo inahusisha pesa nyingi sana lakini niliwambia nitawasaidia nikipata malipo yanayofuata.
Wakati huo Thierry Mangwa alikua anaishi kwenye nyumba yangu kwasababu alikua ana matatizo binafsi so ikabidi tukae wote.Siku moja narudi kutoka mazoezini nikamkuta analina na hajawai kuniambia kwamba hata kaka zangu hawakuniambia.Siku nyingine rafiki yangu Padjoe alikuja kunitembelea na wakati anaondoka nikampa €500. Kaka yangu Kola alivyojua hivto alikasirika sana. Alikua hajaelewa kwanini nimpe rafiki pesa na sio yeye. Sababu ilikua ni simple, pesa aliyokua anataka Kola ilikua ni nyingi.
Siku moja nilikua nimechoka sana baada ya mazoezi nikaamua kulala, nilivyoamka nikakuta kisu shingoni mwangu na kaka zangu walikua wanapiga kelele kwamba nawapotezea muda.Nikawauliza hii ndio njia ya ku-solve tatizo, basi niueni na mchukue pesa. Basi wakaniacha na kuweka kisu chini.
Mama akanishauri niite polisi na nikafanya hivyo lakini damu nzito kuliko maji nikaacha yapite.
Baada ya mwezi nikarudi Togo nikashangaa mama yangu akibwatukia kwanini nimewaita polisi kisa kaka zangu wakati yeye ndie aliyenishauri hivyo. Akasema mimi ni mtu mbaya kwenye familia.
Kila muda nikirudi Togo watu wananiuliza kwanini kaka yangu Kola harudi kutembelea nyumbani baada ya miaka yote aliyoenda Ujerumani.Nikamnunulia ticket ya ndege na kumsafirisha hadi nyumbani kwa gharama zangu mwenyewe.
April 22, 2005 baba yetu alifariki na kabla ya hapo aliniambia nihakikishe msiba wake usiwe sehemu ya masikitiko bali tufurahie na kujivunia maisha yake hapa duniani. Mimi nikanunua ticket kwa ajili ya kaka zangu wote na tukaenda Togo na nikafanya kama baba alivyoseama.Kola anaejiita baba wa familia alifanya nini kwenye huo msiba licha ya kukaa ujerumani miaka yote.