SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Mar 16, 2015

YANGA SC NA FC PLATINUM KATIKA PICHA JANA TAIFA

Kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima akimtoka beki wa FC Platinum ya Zimbabwe jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza, Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga SC ilishinda 5-1.
Kiungo wa Yanga SC, Salum Telela akipambana na mchezaji wa Platinum
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa akimgeuza beki wa Platinum, Elvis Moyo
Beki wa Yanga SC, Oscar Joshua akimpiga chenga mshambuliaji wa Platinum

Mshambuliaji wa Yanga SC, Amisi Tambwe akimtoka beki wa Platinum

SABABU ZA MRISHO NGASSA KULIA BADALA YA KUSHANGILIA MABAO YAKE JANA DHIDII YA PLATUMN

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MRISHO Khalfan Ngassa jana amefunga mabao mawili Yanga SC ikishinda 5-1 dhidi ya Platinum FC katika mchezo wa kwanza, Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika, lakini hakushangilia badala yake akaanza kulia.
Kisa nini? Ngassa ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba alishindwa kuzuia hisia zake juu ya majonzi aliyonayo kufuatia kifo cha kocha Sylvester Marsh.
Marsh, kocha wa zamani wa timu za taifa, kuanzia za vijana, hadi ya wakubwa, Taifa Stars alifariki dunia juzi katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa ya saratani ya koo.
Mwili wa Marsh uliagwa jana katika hospitali ya Muhimbili kabla ya kusafirishwa kwa basi dogo aina ya Coaster kupelekwa Mwanza kwa mazishi na Ngassa amesema msiba huo umemuumiza mno.
Mrisho Ngassa kulia akilia baada ya kufunga bao la nne katika ushindi wa Yanga SC wa 5-1
Ngassa kulia akilia baada ya kufunga bao la tano 

“Marsh amenifundisha mpira Kagera Sugar,lakini pia ndiye ambaye alinichukua kwa mara ya kwanza U17 (timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17,”.
Baada ya kufanya vizuri Serengeti ndipo milango ya mafanikio yangu kisoka ikafunguka, kwa hivyo unaweza kuona huyu ni mtu muhimu kiasi gani katika maisha yangu,”alisema Ngassa.
Nyota huyo wa timu ya Jangwani amesema kwamba baada ya kupata taarifa kwamba mwili wa Marsh utasifirishwa kwa basi, alijaribu kufanya jitihada za kuwezesha usafirishwe kwa ndege, lakini akakosa ushirikiano.
“Nilijaribu kuwatafuta ndugu za marehemu, lakini sikuwapata na bahati mbaya tulikua katika maandalizi ya mchezo wetu, hivyo nikakosa njia nyingine ya kufsnya. Ila msiba huu umeniumiza sana na nimeshindwa,”amesema.   
Ili Yanga isisonge mbele, inabidi ifungwe mabao 4-0 na Platinum katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Bulawayo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Djamaladen Aden Abdi, aliyesaidiwa na Hassan Eguech Yacin na Abdallah Mahamoud Iltireh wote wa Djibouti, hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Mabao ya Yanga SC yalifungwa na viungo Salum Abdul Telela ‘Master’ dakika ya 32 na Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ dakika ya 43, wakati bao la Platinum lilifungwa na Walter Musoma dakika ya 45.
Kipindi cha pili, Yanga waliongeza makali na kufanikiwa kupata mabao matatu zaidi, ambayo yanawafanya waende Bulawayo kwenye mchezo wa marudiano, wakiwa wana kazi ndogo tu.
Mabao hayo yalifungwa na Amisi Tambwe dakika ya 47 na Mrisho Ngassa mawili dakika ya 55 na 90.

NOOIJ AMUITA DIDA STARS JAPO HAJADAKA MIEZI MITATU YANGA

Na Baraka Kizuguto, MOROGORO
LICHA ya kwamba hajacheza mechi yoyote tangu Desemba 13, mwaka jana alipodaka Yanga SC ikifungwa mabao 2-0 na watani SImba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, lakini kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ ameitwa Taifa Stars.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooj, ametaja kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Machi 29, 2015 na Dida yumo kikosini.
Tangu atunguliwe mabao mawili, Yanga ikilala 2-0 mbele ya Simba mechi ya Mtani Jembe, Dida amekuwa akimuangalia Ally Mustafa ‘Barthez’ akifanya kazi kwenye lango wana Jangwani hao.
Dida aliyeruka juu akiwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars. Ameitwa Stars japokuwa hajadaka tangu Desemba 13, mwaka jana 

Taifa Stars inayotarajia kucheza na The Flames mwishoni mwa mwezi huu, itaingia kambini machi 22 machi  katika hotel ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea jijini Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo.
Mbali na Dida, wachezaji wengine walioitwa ni makipa Aishi Manula na Mwadini Ali, wote wa Azam FC, wakati mabeki ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United).
Washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar), Simon Msuva, Mrisho Ngassa (Yanga), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta (TP Mazembe - DRC), John Bocco (Azam FC), na Juma Luizio (Zesco United - Zambia)
Timu ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.

YANGA SC WAFANYA MAUAJI AFRIKA, YAWATANDIKA WAZIMBABWE 5-1, NGASSA APIGA MBILI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imetanguliza mguu mmoja hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Platinum FC ya Zimbabwe jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ili Yanga isisonge mbele, inabidi ifungwe mabao 4-0 na Platinum katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Bulawayo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Djamaladen Aden Abdi, aliyesaidiwa na Hassan Eguech Yacin na Abdallah Mahamoud Iltireh wote wa Djibouti, hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Mrisho Ngassa kulia akifurahia na Haruna Niyonzima baada ya kufunga bao la nne leo

Mabao ya Yanga SC yalifungwa na viungo Salum Abdul Telela ‘Master’ dakika ya 32 na Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ dakika ya 43, wakati bao la Platinum lilifungwa na Walter Musoma dakika ya 45.
Kipindi cha pili, Yanga waliongeza makali na kufanikiwa kupata mabao matatu zaidi, ambayo yanawafanya waende Bulawayo kwenye mchezo wa marudiano, wakiwa wana kazi ndogo tu.
Mabao hayo yalifungwa na Amisi Tambwe dakika ya 47 na Mrisho Ngassa mawili dakika ya 55 na 90.
Mshambuliaji Mliberia, Kpah Sherman aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Simon Msuva alimsetia krosi nzuri Ngassa kufunga bao la tano. 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Hassan Dilunga, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Salum Telela, Simon Msuva/Kpah Sherman, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe na Said Juma ‘Kizota’.
Platinum FC; Petros Mhari, Raphael Muduviana, Kelvin Moyo, Gift Bello, Thabit Kamusuko, Wellington Kamudyariwa/Simon Shoko, Wisdom Mtasa/Aaron Katege, Brian Muzondiwa, Obrey Ufiwa/Emmanuel Mandiranga, Walter Musoma na Elvis Moyo. 

HUU NDIO MSIMAMO LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MECHI ZA WIKIEND HII

ANGALIA MAN UNITED ILIVYOITUNGUA TOTTENHAM 3-0, ROONEY, FELLAINI, CARRICK WAKING'ARA

 
MANCHESTER UNITED 4-1-4-1: De Gea 6, Valencia 6, Jones 6.5, Smalling 7, Blind 7, Carrick 8.5 (Rafael 87'), Herrera 6.5, Mata 6.5 (Pereira 79mins), Fellaini 7.5 (Falcao 83'), Young 7.5, Rooney 8
Subs not used: Lindegaard, Blackett, Januzaj, Wilson
Manager: Van Gaal 7 
Goals: Fellaini (9), Carrick (19), Rooney (34) 
Booked: Mata 

TOTTENHAM 4-2-3-1: Lloris 6, Walker 4, Dier 4.5, Vertonghen 6, Rose 5.5; Bentaleb 5, Mason 5 (Lamela 64', 4); Chadli 5.5 (Adebayor 79'), Eriksen 5, Townsend 4 (Dembele 31mins, 5); Kane 5.
Subs not used: Vorm, Chiriches, Davies, Paulinho.
Manager: Pochettino 5
Goals: Nil Booked: Rose 
MOM: Michael Carrick. 


`