SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Apr 10, 2015

ARSENAL WATUA ARGENTINA KUKAMILISHA USAJILI WA 'MESSI'

KIONGOZI wa Arsenal, Dick Law amesafiri kwenda Argentina kukamilisha usajili wa kinda Maxi Romero.
Mkuu wa mijadala ya klabu hiyo, amepaa hadi Amerika Kusini kumalizia mpango wa kumsajili mshambuliaji kinda wa miaka 16, ambaye tayari ameanza kufananishwa na Lionel Messi.
The Gunners wamepiga hatua katika mazungumzo na Velez Sarsfield juu ya usajili wa Pauni Milioni 4.5 wa kinda huyo.
Arsenal are close to signing 16-year-old Maxi Romero from Velez Sarsfield for £4.5million
Arsenal ipo karibu kumsajili kinda wa miaka 16, Maxi Romero kutoka Velez Sarsfield kwa Pauni 4.5

Lakini dili hilo limekuwa likitiwa ugumu na haki za umilikinwa Romero- hivyo amelazimika kusafiri hadi Argentina kukamilisha mipango hiyo.
wakala wa Romero na klabu yake, Velez wote wana hisa katika kummiliki mchezaji huyo,ambayo inalketa mkanganyiko kwa Arsenal.
Ligi Kuu ya England hairuhusu mmiliki wa tatu katika sheria za usajill na suala hilo lazima limalizwe kama ya mchezaji kwenda kuanza kazi The Gunners.
Romero anatarajiwa kubaki na Velez, kwa mkopo, kwa angalau misimu miwili zaidi kabla ya kwenda England kuanza maisha mapya Arsenal. Nyota huyo kinda hajawahi kuchezea kikosi cha wakubwa cha Velez, bali amekuwa akifanya nacho mazoezi kama mchezaji wa kikosi hicho.

ALVES AFUNGASHA, AWAAGA BARCELONA, ANAKWENDA MAN UNITED AU MAN CITY

BEKI wa pembeni, Dani Alves anatazamiwa kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu baada ya mwakilishi wake kuthibitisha mlinzi huyo wa kulia wa Kibrazil amekataa ofa ya kuongeza Mkataba.
Alves amefurahia mafanikio kwa miaka saba Barcelona, akishinda mataji manne ya Hispania na mawili ya Ligi ya Mabingwa.
Lakini mkonhwe huyo mwenye umri wa miaka 31, hajawa tayari kungeza Mkataba na klabu hiyo ya Nou Camp.
Alves has enjoyed seven successful years at Barcelona, winning four Spanish titles
Beki wa kulia wa Brazil, Dani Alves anajiandaa kuondoka Barcelona msimu huu

Wakala wa mchezaji huyo, Dinorah Santana, ambaye pia ni mke wa zamani wa Alves, amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana kwamba mteja wake amekataa ofa ya kuongeza Mkataba.
"Majadiliano yamekwisha," amesema mwanamama huyo.
"Ikiwa wamesema hii ni ofa ya mwisho, kisha (majadiliano yamekwisha).
Habari hizo zinatoa fursa kwa klabu ambazo zimekuwa zikimtaka beki huyo hodari kuanza kumfuatilia kuwania saini yake.
Beki huyo wa zamani wa Sevilla pia ya Hispania, amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United na Manchester City zote za England, pamoja na Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
Brazilian right-back Dani Alves (right) looks set to leave Barcelona this summer
Alves amekuwa na miaka saba ya mafanikio Barcelona, akishinda mataji manne ya Hispania na mawili ya Ulaya