SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 3, 2015

HARRY REDKNAPP AFYA MGOGORO, AACHIA NGAZI QPR

Harry Redknapp ameachia ngazi Queens Park Rangers kufuatia maumivu ya magoti lakini ameweka wazi kuwa bado huo hautakuwa mwisho wake wa kufundisha soka.
Redknapp, 67, amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuambiwa kuwa atahitajika kufanyiwa upasuaji wa magoti yake yote mawili. Hawezi kutembea hata hatua 100, akakiri kuwa kwa sasa yeye si mtu sahihi wa kuiongoza QPR katika vita vya kushuka daraja. Akampigia mmiliki wa timu saa 11.30 alfajiri na kumjulisha habari hizo.
Harry Redknapp quit QPR with the club second bottom of the Premier League
Kocha huyo mkongwe anasema: “Sikupata usingizi usiku mzima, nawaza kuhusu hilo. Siwezi kutembea, nimekuwa kwenye maumivu muda wote. Nimejitahidi sana lakini inafika hatua nakuwa siwezi kufanya kazi yangu.
“Siwezi kwenda uwanjani, hata kama gari litaniingiza mpaka ndani lakini bado nitapaswa kutembea kidogo.
“Nilikwenda uwanjani kumtazama mjukuu wangu akicheza soka wikiendi iliyopita lakini baada ya dakika tano tu nililazimika kurudi kwenye gari. Sikuweza hata kusimama. Ni maisha gani haya kama huwezi hata kutazama watoto wakicheza? Nikafikiria usiku kucha, baadae nikaamua kumipigia Tony Fernandes.


JACKLINE WOLPER AMKUBALI AY

Acctress Jacquline Wolper kutoka katika kiwanda cha filamu bongo amewataka watanzania kupenda kazi za wasanii wa nyumbani na kuwapa support katika kazi zao wanazofanya ili kuwatia nguvu na kuwapa moyo wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi kwa
Msanii Jacqueline Wolper
watanzania,Wolper amesema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Instragram alipokuwa akionyesha jinsi gani ameguswa na kazi mpya ya msanii Ambwene Yesaya (AY).
Wolper alisema kuwa katika maisha ya kila siku ni vizuri raha na burudani kupata na watu waliokuzunguka maana hao ndio msaada wako hata pale utapatwa na matatizo
"Jioni yangu ya leo(Jana) imekua nzuri sana nimemaliza kazi,mapema mbio nyumbani kuburudika na nyimbo mpya ya msanii ninayemkubali kaka Ay jamani tupende vya nyumbani na Raha pata nawalokuzunguka mimi na familia tuko happy nazigo tumeliewa sema nini nina kazi hii week nzima Radio itapasuka maana dada hata akiwa jikon atakua na usemi wa zigo zigo hahaha big up my broo we love u Ay"
Mwanadada Jackline Wolper ameungana na msanii Ommy Dimpoz kutibitisha kuwa Ay amefanya kazi nzuri na kali ambayo kwa matazamo wao wanaamini kuwa itafanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari na hiki ndicho Ommy Dimpoz amefunguka
"Zigo jipyaa kotoka kwa Yesayaaaaa Ay hatariii sana naona kaamua kuchukua hela zake sasa"
Ay jana ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Zigo ambao umefanywa na Produza Narheel na kufanyiwa Mixing katika studio za Mj Records lakini pia mkali huyo jana ameachia Video ya wimbo wake wa It's going down.

BAADA YA KUFUNGWA JIONI YA LEO AZAM FC ITARUDI KESHO

10502243_903983952975295_7904939974675269474_n
MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara, Azam fc wamemaliza ziara yao nchini Congo DR ambako wameshiriki michuano ya Mazembe inayoendelea mjini Lubumbashi.
Azam walianza kwa kufungwa goli 1-0 na TP Mazembe, wakatoka sare ya 2-2 na Zesco United ya Zambia na leo wamefungwa 1-0 na Don Bosco.
Katibu Mkuu wa Azam fc, Idrissa Nassor ‘Father’ amesema kikosi cha Azam kitatua kesho jijini Dar es salaam tayari kwa maandalizi ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Polisi Morogoro itayopigwa uwanja wa Jamhuri mwishoni mwa wiki hii.
“Tutarudi kesho saa mbili asubuhi, tutarudi Chamazi na kuendelea na mazoezi kuelekea mechi ya jumamosi Morogoro dhidi ya Polisi Morogoro. Baada ya hapo tutacheza na Mtibwa Sugar”. Amesema ‘Father’ na kusisitiza: “Mazoezi ya Congo yalikuwa maalumu kwa mechi za ligi ya mabingwa, tumejifunza mengi na tunatarajia kufanya vizuri”.

HII INAIHUSU KLABU YA BARCELONA

073014-Soccer-FC-Barcelonas-Brazilian-Neymar-J2-PI.vadapt.620.high.0
Ni siku nyingine ngumu kwa Raisi wa FC Barcelona Josep Maria Bartomeu.
Huku uchaguzi mkuu ukiwa umekaribia ndani ya Nou Camp, nafasi ya Bartomeu kurejea madarakani imeingia shakani leo jumanne baada ya kutoka kwa tuhuma zinazomhusisha raisi huyo wa sasa na mambo ya kukwepa kodi.
Sakata hilo la kukwepa kodi linahusisha kesi ya usajili wa Neymar kutoka Santos mwaka 2013.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na utata juu fedha iliyolipwa kwenye usajili wa Neymar na Barcelona – mwendesha mashtaka wa kesi dhidi ya Barca anadai Barca waliwalipa Santos kiasi cha €94.8m kwa jumla (€82.7m za ada ya usajili huku €12.1m za kodi), wakati Barcelona wakisema walilipa kiasi cha €57.1m tu.
Screen-Shot-2015-02-03-at-11.16.57-AM
Bartomeu, pamoja na rasi aliyejiuzulu Sandro Rosell, wanatuhumiwa kwa kupika taarifa za uongo katika uhamisho huo wa Neymar – na matokeo yake Bartomeu anashatakiwa kwa kuhusika na kukwepa inayofikia kiasi cha €2.8m.
Bartomeu anatarajiwa kwenda mahakamani baadae mwaka huu kujitetea dhidi ya mashtaka haya, kwa pamoja na raisi aliyejiuzulu mwezi uliopita kutokana na tuhuma hizo Sandro Rosell.

20 PERCENT AIBUKA MORO APIGA SHOW YA NGUVU


Mkali wa Bongo Fleva, Abbas Kinzasa a.k.a 20 Percent akitoa burudani.
Mkali wa Bongo Fleva, Abbas Kinzasa a.k.a 20 Percent akiwa na bendi yake ya Mwakaulwi Sound.
...Akiendelea kuimba.
Mkali wa Bongo Fleva ambaye mwaka 2012 alitwaa Tuzo Tano za Kili, Abbas Kinzasa a.k.a 20 Percent ameibuka kivingine baada ya kutoka kwenye Bongo Fleva na kutumbukia dansi akiwa na bendi yake ya Mwakaulwi Sound.
Jumapili iliyopita 20 Percent aliyewahi kutamba na Ngoma Tamaa Mbaya ambayo ni miongoni mwa nyimbo zilizompatia tuzo alinaswa na kamera yet ndani ya Ukumbi wa Black Point wa mkoani hapa akikamua vilivyo na kuwakonga mashabiki wake.
Aliposhuka stejini mwanahabari wetu alifanikiwa kufanya mahojiano juu ya kubadili aina ya muziki wake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli kwa sasa nimeachana na Bongo Fleva. Nimeingia rasmi kwenye dansi.
“Kwa sasa namiliki bendi yangu ya Mwakaulwi Sound ambayo kwa sasa nafanya matamasha mjini Bagamoyo.
“Lengo la kuja Moro, nataka bendi yangu niihamishie hapa kwani hapa nina kampani kubwa ya akina Afande

YANGA, AZAM KUCHEZA FAINALI ZA MASHINDANO MAPYA YA EBOLA


Kwa ufupi
Maombi hayo yalisomwa kwenye kikao cha 24 cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia na ikapitishwa kwa kuundwa kamati maalumu ya kusimamia mashindano hayo.

Dar es Salaam. Wakongwe wa soka nchini ambao pia ni mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu, Yanga na pia Azam watashiriki mashindano mapya ya soka yanayoitwa Ebola yatafanyika baadaye mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tibohora alisema jana kuwa klabu hiyo imejitolea kuchangia matibabu ya ugonjwa huo katika nchi zilizoathirika.

Alisema mwenyekiti wake, Yusuf Manji atayadhamini mashindano kwa Dola 500,000 na kwamba yatajulikana kama, ‘Mashindano Huru ya Bara’.“Mwenyekiti wetu (Yusuf Manji) aliwasilisha dodoso kwenye Umoja wa Afrika (AU) kwa kushirikisha Serikali, kuandaa mchakato wa kuchangisha fedha kwa wafanyabiashara wakubwa kwa nchi wanachama wa umoja huo, lengo likiwa ni kuzisaidia nchi zilizoathirika na ugonjwa wa ebola. “Ni kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa Yanga, ambayo ni klabu kubwa na wenye mashabiki wengi Tanzania, mpira pia ni biashara, ikapendekezwa kupitia mpira pia kuwe na mashindano ambayo yatachangia waathirika wa ebola. Maombi hayo yalisomwa kwenye kikao cha 24 cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia na ikapitishwa kwa kuundwa kamati maalumu ya kusimamia mashindano hayo. Tibohora alisema mashindano haya yatashirikisha timu 108 kutoka kila nchi mwanachama wa AU, ambaye pia ni mwanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zitaingiza timu mbili, mshindi wa kwanza na wa pili hapa nchini timu watashiri

HII INA MUHUSU FRANCIS CHEKA

Mke wa Cheka aangua kilio kortini

Bondia Francis Cheka akipanda kwenye gari ya polisi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela. Picha na Mpigapicha Wetu 
Na Hamida Shariff na Imani Makongoro, Mwananchi

Posted  Jumanne,Februari3  2015  saa 14:15 PM
Kwa ufupi
Mumewe atupwa jela miaka mitatu, mashabiki, mabondia washikwa butwaa.
Morogoro/Dar . Wakati mke wa bondia maarufu nchini, Francis Cheka (32), Toshi Asenga akimwaga machozi mahakamani mumewe alipohukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa fidia ya Sh1 milioni, mabondia wa zamani, wadau wengine wameshikwa butwaa.
Katika hali ya kushangaza pamoja na umarufu wake, mashabiki wengi wa ngumi mjini Morogoro na vitongoji vyake hawakuwa na taarifa kuhusu kesi hiyo.

Cheka alitiwa hatiani kwa kosa la kumshambuliaji meneja wa baa yake, Bahati Kibanda.
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mke wa bondia huyo aliangua kilio akilalamika kuwa mumewe ameonewa na kwamba hakustahili kupewa adhabu hiyo kubwa.
Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Cheka alitenda kosa hilo Julai 2 mwaka jana kwenye eneo la Ukumbi wa Vijana Social mjini Morogoro.

Ilidaiwa kuwa bondia huyo alimpiga ngumi na mateke maeneo ya tumboni na kichwani na hivyo kumsababishia Kibanda maumivu makali, wakati akijua kutenda hivyo ni kosa kisheria.
Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao haukuacha shaka yoyote katika kuthibitisha shtaka hilo.

“Adhabu hii itakuwa fundisho kwa mshtakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao na mshtakiwa anatakiwa kumlipa fidia ya Sh1 milioni kwa mlalamikaji.”
Hata hivyo, Cheka alipopewa nafasi ya kujitetea aliieleza Mahakama kuwa hana maelezo yoyote zaidi ya kuiachia Mahakama iamue adhabu itakayompa.

Awali, mwendesha mashtaka wa Polisi, Anganile Nsiyani alidai mahakamani hapo na kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 2 mwaka 2014 katika baa ya Vijana Social Hall iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mwendesha mashtaka huyo alidai akijua kufanya hivyo ni kosa Cheka alimshambulia meneja wake wa baa (Bahati Kibanda) kwa kumpiga ngumi usoni na tumboni na hivyo kumsababishia maumivu makali.
Alipofikishwa Mahamani hapo kwa mara ya kwanza Cheka alikana shtaka hilo na hivyo upande wa mashtaka uliahidi kupeleka mashahidi wanne kati ya saba walioithibitisha mahakamani hapo bila ya shaka kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo na hivyo mahakama ikamtia hatiani.

YANGA YATUA SALAMA TANGA


Kikosi cha Yanga, kimetua salama mjini Tanga kujiandaa na mchezo wake wa kesho dhidi ya Coastal Union.

Lakini Yanga wamekataa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambao walitakiwa kufanya mazoezi leo na kuamua kufanya mazoezi kwenye uwanja wa jeshi.
Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema walipanga kufanya mazoezi kwenye uwanja huo na si Mkwakwani.
“Nafikiri hakuna tatizo, kilichotakiwa pale ni suala la mazoezi na tumefanya, hivyo hakuna tatizo lolote,” alisema Muro.

Yanga ina kibarua cha kuivaa Coastal Union kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.

KOPUNOVIC AMLILIA JEAN MARIE, ASEMA ALIMFUATILIA WIKI ILIYOPITA


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic ameonyesha wazi masikitiko yake kutokana na kifo cha ghafla ya Kocha Jean Marie Ntagwabila.

Kopunovic amesema amesikitishwa na taarifa hizo kwa kuwa kocha huyo raia wa Rwanda alikuwa kati ya rafiki na wapinzani wake kikazi.

“Wiki iliyopita nilikuwa nafuatilia habari zake mtandaoni, kwa kweli imenisikitisha sana.

“Wakati nikiwa Polisi Rwanda, alikuwa mpinzani wangu mkubwa akiwa na Kiyovu. Aliwahi pia kufundisha timu nyingine za Rwanda kwa mafanikio makubwa,” alisema raia huyo wa Serbia.
Ntagwabila amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kukimbizwa kwenye hospitali ya kijeshi ya Kanombe jijini Kigali kutokana na matatizo ya mapafu yaliyosababisha ashindwe kupumua.

Simba iliamua kumchukua Kopunovic baada ya kuona wanamhitaji zaidi ya Ntagwabila ambaye pia alikuwa na nafasi ya kuchukua mikoba ya Patrick Phiri raia wa Zambia aliyetimuliwa Simba.

Marehemu aliwahi kuwa mchezaji wa APR na baadaye kocha, pia alizifundisha Rayon na Atraco na kuzipa makombe.

Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic ameonyesha wazi masikitiko yake kutokana na kifo cha ghafla ya Kocha Jean Marie Ntagwabila.

Kopunovic amesema amesikitishwa na taarifa hizo kwa kuwa kocha huyo raia wa Rwanda alikuwa kati ya rafiki na wapinzani wake kikazi.

“Wiki iliyopita nilikuwa nafuatilia habari zake mtandaoni, kwa kweli imenisikitisha sana.

“Wakati nikiwa Polisi Rwanda, alikuwa mpinzani wangu mkubwa akiwa na Kiyovu. Aliwahi pia kufundisha timu nyingine za Rwanda kwa mafanikio makubwa,” alisema raia huyo wa Serbia.
Ntagwabila amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kukimbizwa kwenye hospitali ya kijeshi ya Kanombe jijini Kigali kutokana na matatizo ya mapafu yaliyosababisha ashindwe kupumua.

Simba iliamua kumchukua Kopunovic baada ya kuona wanamhitaji zaidi ya Ntagwabila ambaye pia alikuwa na nafasi ya kuchukua mikoba ya Patrick Phiri raia wa Zambia aliyetimuliwa Simba.

Marehemu aliwahi kuwa mchezaji wa APR na baadaye kocha, pia alizifundisha Rayon na Atraco na kuzipa makombe.

HANS POPPE AMPASHA KISIGA, AMWAMBIA ANAJISUMBUA MWENYEWE

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemwambia kiungo mkongwe wa Simba, Shabani Kisiga asidhani anausumbua uongozi wa klabu hiyo kwa kuondoka kambini.

Kisiga ameondoka kambini Simba kwa madai amekuwa hachezeshwi, lakini Hans Poppe amesema anajipotezea muda wake.
Image result for kisiga
“Hawezi kutusumbua sisi, aliwahi kutusumbua lakini alirudi na kusema kwamba sasa yuko vizuri.
“Kisiga alisema amekuwa tofauti, lakini sasa ameamua kuondoka jambo ambalo halitusumbui na ingekuwa vizuri afanye utaratibu aende tu kwa amani kuliko kufanya hivyo,” alisema.
Hans Poppe alisisitiza suala la nidhamu huku akisema Kisiga alipaswa kuwa mfano katika suala la nidhamu.
Pia alisema mwenye uwezo wa kuona nani anapaswa acheze ni kocha na kama Kisiga angekuwa anafaa, kamwe Goran Kopunovic asingemuacha nje.


Pia alisema mwenye uwezo wa kuona nani anapaswa acheze ni kocha na kama Kisiga angekuwa anafaa, kamwe Goran Kopunovic asingemuacha nje.

HII NDIO THAMANI YA RONALDO KAMA UNATAKA KUMSAJILI

 
Jorge Mendes wakala wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo amesema mchezaji huyo ana thamani ya pauni milioni 300 ikiwa ataamua kuihama klabu yake ya Real Madrid.
Wakala huyo amesema ikiwa timu yake itataka kuuza kwa sababu yoyote ile ni lazima timu inayomtaka itoe kiasi hicho cha fedha.

Ronaldo, mwenye wa miaka 29, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Dunia Mwezi uliopita alikua akihusishwa kurudi katika klabu yake zamani ya Manchester United.
Mendez akasisitiza kuwa nyota huyo atasalia katika timu ya Real Madrid pamoja na kupendwa na mashabiki wa Manchester United.

Wakala huyo aliyewahi kuwa Dj na mmiliki wa Klabu za usiku, ni mwakilishi wa nyota wengine katika soka kama Radamel Falcao, Angel Di Maria, James Rodriguez, David De Gea, Victor Valdes na Diego Costa. Pamoja na makocha Jose Mourinho, Luiz Felipe Scolari.

AZAM FC KUMALIZA ZIARA LEO DRC

 
Timu ya soka ya Azam ya Tanzania leo itamaliza ziara yake nchi Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa kucheza mchezo wa mwisho na klabu ya Don Bosco .

Mchezo utapigwa majira ya saa tisa kwa saa Afrika Mashariki itafuatiwa na mechi kati ya Mabingwa wa DRC TP Mazembe dhidi ya Mabingwa wa Zambia Zesco United.
Ziara ya Azam ni maandalizi katika kujiandaa na michuano ya klabu bigwa barani Afrika pamoja na ligi kuu ya Tanzania inayoendelea .

Azam walianza ziara yao kwa kupoteza mchezo mbele ya TP Mazembe kwa kichapo cha bao 1-0.
Kisha wakakubali suluhu ya mabao 2-2 dhidi ya mabigwa wa Zambia katika mchezo wao wa pili.

MAN UNITED KUIVAA CAMBRIDGE UNITED



 

Manchester United itashuka dimbani kuikabili timu ya Cambridge United katika mchezo wa marudio kombe la FA.
baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa Abbey Stadium Nyumbani kwa Timu hiyo ya Daraja la Chini, Ligi daraja la 2.

Hii ni Mechi ya raundi ya 4 ya FA Cup na Mshindi atatinga Raundi ya 5 na kucheza na Mshindi kati ya Preston au Sheffield United ambao nao wanarudiana leo Jumanne.

Mechi za Raundi ya 5 zitachezwa Wikiendi ya Februari 14 na 15.
Michezo mingine inayochezwa leo ni Fulham dhidi ya Sunderland, huku Sheffield United wakiwakabili Preston

Jumatano kutakua na mchezo mmoja ambapo majogoo wa jiji Liverpool watakua wakichuana na Bolton Wanderers

KOCHA YANGA KUNA TATIZO LAKINI HAKUNA KUKATA TAMAA

  Image result for HANS PLUIJM
Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema hali ya kikosi chake kushindwa kutumia nafasi inachanganya, lakini hawataka tamaa.


Pluijm amekuwa akilia na nafasi nyingi wanazopoteza katika kila mechi.

"Kweli bado ni tatizo, si dogo kwa kuwa kila mmoja anaweza akaliona sasa. Tunahitaji kuendelea kulifanyia kazi, tunahitaji kutulia na hatuwezi kukata tamaa.

"Ukisema tukubali kuchanganyikiwa, tunaweza kujichanganya zaidi. Lakini ni lazima tukubali kuna tatizo na lazima tulitatue," alisema Pluijm.

Wachezaji wa Yanga wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi katika kila mechi, hivyo kuifanya timu yao itoke bila mabao.

Mara ya mwisho, Yanga imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ndanda FC huku washambuliaji wake wakipoteza nafasi takribani saba za wazi za kufunga.

FLETCHER ATU WEST BROM


Kiungo wa Manchester United, Darren Fletcher ametua West Bromwich Albion kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Fletcher ,30, amekuwa kati ya wachezaji waliohama timu moja kwenda nyingine katika hatua za mwisho za dirisha la usajili.

Kiungo huyo mkongwe ametua Wes Brom likiwa limebaki saa moja kabla ya dirisha kufungwa.

USAJILI MZIMA DIRISHA DOGO ENGLAND, NANI KAINGIA WAPI, NANI KATOKA TIMU ZOTE LIGI KUU


Arsenal imesajili kinda wa miaka 17, Krystian Bielik na beki wa kati, Gabriel Paulista kwa Pauni Milioni 11.2, wakati Manchester United imemsajili kipa mkongwe Victor Valdes, huku vigogo wengine,
Liverpool wakiwa hawajasajili mchezaji yeyote.

ARSENAL: 
WALIOINGIA: Gabriel Paulista (Villarreal, Pauni Milioni 11.2) na Krystian Bielik (Legia Warsaw, Pauni Milioni 2.5).  
WALIOTOKA: Benik Afobe (Wolves), Lukas Podolski (Inter Milan, mkopo), Yaya Sanogo (Crystal Palace, mkopo), Joel Campbell (Villarreal, mkopo).  

ASTON VILLA  
WALIOINGIA: Carles Gil (Valencia, Pauni Milioni 3.25), Scott Sinclair (Manchester City, mkopo). 
WALIOTOKA: Darren Bent (Derby, mkopo), Gary Gardner (Nottingham Forest, mkopo), 
Chris Herd (Wigan, mkopo), Callum Robinson (Preston, mkopo).

BURNLEY: 
WALIOINGIA: Michael Keane (Manchester United).
WALIOTOKA: Hakuna.

CHELSEA: 
WALIOINGIA: Juan Cuadrado (Fiorentina, Pauni Milioni 27). 
WALIOTOKA: Andre Schurrle (Wolfsburg, Pauni Milioni 24), Ryan Bertrand (Southampton, Pauni Milioni 10), Mark Schwarzer (Leicester, bure), 
Thomas Kalas (Middlesbrough, mkopo), John Swift (Swindon, mkopo), Lewis Baker (Sheffield Wednesday, mkopo), Marko Marin (Anderlecht, mkopo), Mohamed Salah (Fiorentina, mkopo).

CRYSTAL PALACE: 
WALIOINGIA: Wilfried Zaha (Manchester United Pauni Milioni 6), Jordon Mutch (QPR, Pauni Milioni 5.75), Lee Chung-yong (Bolton), Keshi Anderson (Barton Rovers, Pauni 35,000), Shola Ameobi (Gaziantep), Pape Souare (Lille), Yaya Sanogo (Arsenal, mkopo). 
WALIOTOKA: Stuart O'Keefe (Cardiff), Alex Wynter (Colchester), Zeki Fryers (Rotherham, mkopo), Lewis Price (Crawley, mkopo), Jake Gray Cheltenham, mkopo), Barry Bannan (Bolton, mkopo), Jimmy Kebe (ametemwa).

EVERTON: 
WALIOINGIA: Aaron Lennon (Tottenham, mkopo). 
WALIOTOKA: Samuel Eto'o (Sampdoria, bure), 
Chris Long (Brentford, mkopo), Conor McAleny (Cardiff, mkopo).

HULL CITY:
WALIOINGIA: Dame N'Doye (Lokomotov Moscow, Pauni Milioni 3).
WALIOINGIA: Tom Ince (Derby County, mkopo).

LEICESTER CITY: 
WALIOINGIA: Andrej Kramaric (Rijeka, Pauni Milioni 9.5), Mark Schwarzer (Chelsea, bure), Robert Huth (Stoke City, mkopo). 
WALIOTOKA: Tom Hopper (Scunthorpe, mkopo). 

LIVERPOOL: 
WALIOINGIA: Hakuna 
WALIOTOKA: Oussama Assaidi (Al Ahli, Pauni Milioni 4.7), Suso (AC Milan, Pauni Milioni 1).
  
MANCHESTER CITY: 
WALIOINGIA: Wilfried Bony (Swansea, Pauni Milioni 28). 
WALIOTOKA: Matija Nastasic (Schalke, mkopo), Scott Sinclair (Aston Villa, mkopo).

MANCHESTER UNITED: 
WALIOINGIA: Victor Valdes, Sadiq El Fitouri (Salford City, bure), Andy Kellett (Bolton, mkopo). 
WALIOTOKA: Wilfried Zaha (Manchester United, Pauni Milioni 6), Michael Keane (Burnley, Pauni Milioni 3), Darren Fletcher (West Brom, bure), 
Will Keane (Sheffield Wednesday, mkopo), Ben Amos (Bolton, mkopo), Jesse Lingard (Derby County, mkopo). 

NEWCASTLE UNITED 
WALIOINGIA: Hakuna
WALIOTOKA: Mapou Yanga-Mbiwa (Roma, Pauni Milioni 5.2), Hatem Ben Arfa (ametemwa), Gael Bigirimana (Rangers, mkopo), Haris Vuckic (Rangers, mkopo), Shane Ferguson (Rangers, mkopo), Davide Santon (Inter Milan, mkopo).
QUEENS PARK RANGERS: 
WALIOINGIA: Mauro Zarate (West Ham, mkopo), Ryan Manning (Galway United, bure).
WALIOTOKA: Jordon Mutch (Crystal Palace, Pauni Milioni 5.75), Bruno Andrade (Stevenage, mkopo).

SOUTHAMPTON: 
WALIOINGIA: Ryan Bertrand (Chelsea, Pauni Milioni 10), Eljero Elia (Werder Bremen, mkopo),
Filip Djuricic (Benfica, mkopo). 
WALIOTOKA: Jack Cork (Swansea, Pauni Milioni 3), 
Jos Hooiveld (Millwall, mkopo), Artur Boruc (Bournemouth, muendelezo wa mkopo).

STOKE CITY: 
WALIOINGIA: Philipp Wollscheid (Bayer Leverkusen, mkopo).
WALIOTOKA: Ryan Shotton (Derby), Maurice Edu (Philadelphia), Robert Huth (Leicester City, mkopo).

SUNDERLAND: 
WALIOINGIA: Jermain Defoe (Toronto).
WALIOTOKA: Jozy Altidore (Toronto), Mikael Mandron (Shrewsbury, mkopo), Charis Mavrias (Panathinaikos, mkopo), Cabral (ametemwa).
SWANSEA CITY: 
WALIOINGIA: Kyle Naughton (Tottenham, Pauni Milioni 5), Jack Cork (Southampton, Pauni Milioni 3), Matt Grimes (Exeter City, Pauni Milioni 1.75), Nelson Oliveira (Benfica, mkopo).  
WALIOTOKA: Wilfried Bony (Manchester City, Pauni Milioni 28), Rory Donnelly (Tranmere, mkopo), Jazz Richards (Fulham, mkopo).

TOTTENHAM HOTSPUR:  
WALIOINGIA: Dele Alli (MK Dons, Pauni Milioni 5).
WALIOTOKA: Kyle Naughton (Swansea, Pauni Milioni 5), Aaron Lennon (Everton, mkopo), Milos Veljkovic (Charlton, mkopo), Benoit Assou-Ekotto (ametemwa), Dele Alli (MK Dons, mkopo.

WEST BROMWICH ALBION: 
WALIOINGIA: Callum McManaman (Wigan, Pauni Milioni 4.75), Darren Fletcher (Manchester United, bure). 
WALIOTOKA: Luke Daniels (Scunthorpe).

WEST HAM UNITED: 
WALIOINGIA: Doneil Henry (Apollon Limassol)
WALIOTOKA: Mauro Zarate (QPR, mkopo), Ricardo Vaz Te (ametemwa) .
CHANZO BINZUBERY

KOCHA SIMBA AFRIKI DUNIA RWANDA


 
Na Mwandishi Wetu, KIGALI
KOCHA Jean Marie Ntagwabila aliyekuwa atue Simba SC Januari mwaka huu kuwa Msaidizi wa Mserbia, Goran Kopunovic katika klabu ya Simba SC amefariki dunia leo nchini Rwanda.
Ntagwabila amefariki ghafla katika hospitali ya Jeshi, Kanombe baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.
Simba SC ilikuwa kwenye mchakato wa kumleta marehemu afanye kazi na Goran, lakini Mserbia huyo alimkataa na akapendekeza aletwe Mnyarwanda mwingine, Alphonse Gatera aliyekuwa Msaidizi wake wakati anafundisha Polisi ya Rwanda.
Marehemu atakumbukwa nchini Rwanda kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uhai wake, ikiwemo kuifanya APR iwe tishio mno kiasi cha kufikia kuifunga Zamalek ya Misri mabao 4-1 mwaka 2004 katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikitoka kufungwa 3-2 katika mchezo wa kwanza Cairo.
APR ilisonga mbele hatua ya 16 Bora, ambako ilikwenda kutolewa kwa mbinde na Africa Sports ya Ivory Coast kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake. Bwana ametoa, bwana ametwaa. Pumzika kwa amani Jean Marie Ntagwabila.

ALICHOSEMA NATURE KUHUSU WASANII WA ZAMANI


Nyota na msanii mkongwe wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Juma Nature amesema kuwa wasanii wakongwe wa muziki huo watapotea kabisa katika ramani ya muziki kama wadau wa muziki pamoja na vyombo vya habari havitawapa nafasi ya kutosha kama wanavyopewa wasanii wengine wa sasa.

Nature amesema kuwa zamani kipindi yeye yupo Bongo Records wasanii wote walikuwa kitu kimoja na kazi zao walikuwa wanafanya kwa kushirikiana na kwa umoja kitu ambacho kilifanya wote kuwa namafanikio sawa kwani hata maonesho yao walikuwa wanagawana fedha sawa kitu kisichowezekana kwa sasa.

Nature amesema kuwa kwa sasa wasanii kama yeye watapotea kutokana na wadau wa muziki kuwatumia wasanii wachache katika shughuri zao za kila siku huku akitolea mfano jinsi Diamond anavyopewa kipaumbele katika maonesho na kazi nyingine huku wasanii wazuri kama Rich Mavoko na Ali Kiba wakisahaulika kitu kinachosababisha kuwa na matabaka kwani wanaopewa nafasi ndio wanaofanikiwa.

Katika hatua nyingine Juma Nature amewaasa wadau wa muziki kutowasahau wakongwe wa muziki nchini kwani wao ndio walioufikisha muziki huu hapa ulipofika.

HII INAHUSU USAJILI WA DE GEA

 Image result for de gea

Amani ,Furaha imerejea miongoni mwa mashabiki wa Man United baada ya kipa wao namba moja David De Gea kubaki katika timu hiyo yenye maskani yake Mjini Manchester nchini England. Awali viongozi  wa  Real Madrid walikuwa wakimfuatilia ili kumsajili katika klabu yao, Lakini juhudi zao hazikufanikiwa na wanajipanga usajili ujao.