SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 12, 2015

NDUGU WA ADEBAYOR AOMBA MSAMAHA

 

Ndugu ya mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor ameomba msamaha baada ya nyota huyo kumshtumu katika mtandao wa facebook na watu wengine wa familia yake.
Rotimi Adebayor ameiambia BBC kwamba anaomba msamaha kwa makosa aliyofanya,na kwamba angependelea nduguye arudi katika familia.
Emmanuel Adebayor ambaye pia anaichezea Togo alisema wiki iliopita kwamba mzigo wa kifedha wa kuisadia familia yake pamoja na ugomvi katika familia yake umemuahiribia kazi yake.
Amesema kuwa anazitaka familia nyangine barani afrika kupata funzo kutoka kwake.

ABDI KASSIM AZIDI KUKAMUA MALAYSIA, AZIVUTIA TIMU ZA........

  

ABDI KASSIM AKIPAMBANA DHIDI YA EL HADJI DIOUF KATIKA YA MECHI WAKATI TIMU ZAO ZILIPOKUTANA.
Kiungo wa zamani wa Yanga, Abdi Kassim ‘Babi’ sasa amekuwa lulu nchini Malaysia ambako anaichezea timu ya Ligi Kuu Malaysia, University Technology Mara FC (UiTM).

Babi ambaye timu yake sasa iko katika nafasi ya sita, tayari amezivutia kutoka nchini Bahrain na Korea Kusini.

Mtanzania huyo ambaye ni tegemeo katika kiungo cha UiTM amezivutia timu hizo na tayari zimewasiliana na klabu yake kutaka kujua zaidi kuhusiana naye.

“Kweli wametuma maombi ya kutaka watumie video zangu zaidi, pia profile kuhusiana na nilikocheza kabla ya kuja hapa,” alisema Babi alipozungumza na SALEHJEMBE.


“Baada ya hapo, sijajua nini kitakachofuata lakini mimi nimekuwa nikiendelea kupambana vilivyo kuhakikisha timu yangu inafanya vizuri,” alisisitiza.

BAFETIMBI ‘AWALAZA NJAA’ ARSENAL EMIRATES KWA BAO LA UTATA

BAO la utata la Mfaransa Bafetimbi Gomis limeipa Swansea City ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Emirates, London.
Bafetimbi alifunga bao la dakika za lala salama kwa msaada wa teknolojia kwenye mstari wa lango, hicho kikiwa kipigo cha pili mfululizo kwa The Gunners.
Arsenal inabaki nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa pointi zake 70 ilizovuna katika mechi 35, ikiwa nyuma ya Manchester City wenye pointi 73 za mechi 36 na mabingwa, Chelsea wenye pointi 84 za mechi 36 pia.
Manchester United ni ya nne kwa pointi zake 68 za mechi 36 wakati Liverpool yenye pointi 62 za mechi 36 ni ya tano na Tottenham Hotspur yenye pointi 58 za mechi 36 ni ya sita.
Swansea wanaopanda nafasi ya nane sasa kwa kufikisha pointi 56 baada ya mechi 36, wanazidiwa pointi moja tu na Southampton walio nafasi ya saba.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin/Wilshere dk60, Cazorla, Ramsey, Ozil, Sanchez na Giroud/Walcott.
Swansea; Fabianski, Rangel/Richards dk60, Fernandez, Williams, Taylor, Cork, Dyer/Barrow, Shelvey, Ki/Gomis, Montero na Sigurdsson.
The French striker wheels away in celebration as his late header is awarded as a goal by referee Kevin Friend
Befetimbi Gomis akishangilia baada ya bao lake la utata kukubaliwa na refa Kevin Friend

SIMBA SC YAMTUPIA VIRAGO DANI SSERUNKUMA, SIMON NA OWINO NAO…

Dani Sserunkuma ametupiwa virago Simba SC baada ya mechi 17 tangu Desemba aliposajiliwa kutoka Gor Mahia ya Kenya
Na Princess Asia, DARES SALAAM
MABINGWA wa zamani wa Tanzania na Afrika Mashafiki na Kati, Simba SC wamemtupia virago mfungaji bora wa zamani wa Ligi Kuu ya Kenya, Danny Sserunkuma baada ya makubaliano ya pande zote mbili jioni ya leo.
Mshambuliaji huyo raia wa Uganda aliandika katika ukurasa wake wa twitter jana saa 11:22 jioni akisema kuwa amefikia maamuzi ya kusitisha mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu ujao wa ligi bila kuweka wazi sababu zilizomsukuma kufanya hivyo.
Sserunkuma sasa atakuwa huru kujiunga na timu yoyote ambayo itamuhitaji kutumia kipaji chake.
"Simba na mimi (Sserunkuma) kupitia meneja wangu tumefikia maamuzi ya kuvunja mkataba kwa makubaliano yaliyoridhiwa na pande mbili hizi, tumesitisha ajira rasmi", ilisema kwa kifupi taarifa ya taarifa hiyo.
Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally, amethibitisha kuwa ni kweli klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi imevunja mkataba na mganda huyo.
Ally alisema kuwa kufuatia maamuzi hayo, Sserunkuma sasa ni mchezaji huru na Simba haitamlipa kiasi chochote cha fedha.
Sserunkuma alisajiliwa na Simba mwezi Desemba mwaka jana akipewa mkataba wa miezi 12 ambayo ilikuwa inatarajiwa kumalizika mwaka huu.
Hadi anaondoka Simba SC, Sserunkuma aliyetokea Gor Mahia ya Kenya alikuwa amecheza mechi 17 na kuifungia mabao matano katika mashindano yote, matatu kati ya hayo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Bado wachezaji wengine wawili wa kigeni wamekalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo iliyomaliza ya tatu katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ambao ni Simon Sserunkuma na Joseph Owino, wote Waganda.
Wachezaji wengine wa kigeni kikosini Simba SC ni Waganda pia, Juuko Murushid na Emmanuel Okwi waliokuwa wanakamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu.
Simba SC imemaliza katika nafasi ta tatu katika Ligi Kuu msimu huu, nyuma ya Azam FC waliokuwa wa pili na mahasimu, Yanga SC waliotwaa ubingwa.