SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 17, 2015

YANGA WATOA SABABU KWANINI MECHI YAO NA BDF XI HAIKUONYESHWA KWENYE TV


 YANGA imedai kwamba iligoma kuuza haki za matangazo ya Televisheni za mechi yao na BDF XI ya Botswana kwa vile Azam TV haikufika dau.
Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha, ameweka wazi kwamba mechi zao wanaanza kuuza kwa dau la dola 10,000 (Sh 18 milioni) dau ambalo hakuna chombo chochote nchini kilichoweza kulifikia.
Tiboroha amesema Azam TV walitoa ofa ya millioni 8 za kitanzania.kielezi

YANGA imedai kwamba iligoma kuuza haki za matangazo ya Televisheni za mechi yao na BDF XI ya Botswana kwa vile Azam TV haikufika dau.
Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha, ameweka wazi kwamba mechi zao wanaanza kuuza kwa dau la dola 10,000 (Sh 18 milioni) dau ambalo hakuna chombo chochote nchini kilichoweza kulifikia.
Tiboroha amesema Azam TV walitoa ofa ya millioni 8 za kitanzania.

SIMBA NA YANGA KUMENYANA MACHI 8 TAIFA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RATIBA ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea kubadilika badilika kama hali ya hewa, baada ya jana Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutoa ratiba nyingine, inayoonyesha vigogo Simba na Yanga watamenyana Machi 8, mwaka huu.
Tangu kupanguliwa kwa ratiba ya Ligi Kuu kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu visiwani Zanzibar, ratiba ya ligi hiyo imekuwa haieleweki tena kutokana na baadhi ya timu kuwa na mechi za viporo.

Mechi mbili za kila timu ya Azam, Yanga SC, Mtibwa Sugar na Simba zilisimamishwa ili timu hizo ziende Zanzibar na hata baada ya kurudi zimeshindwa kumalizia viporo vyao haraka kutokana na sababu mbalimbali.
TFF ilipanga ichomeke mechi hizo katikati ya wiki ya mechi za timu hizo, ili ndani ya wiki mbili ziwe zimekwishacheza viporo hivyo, lakini ikashindikana.
Wakati mwingine timu ambayo ilitakiwa kucheza na timu iliyokuwa kwenye Kombe la Mapinduzi katika wiki husika ilikuwa ina mechi mkoa wa mbali.
Na ziara ya Azam FC Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikasababisha mechi zao kusogezwa mbele pia.
Lakini inawezekana marekebisho haya ya ratiba ya Ligi Kuu yakawa ya mwisho kwa msimu huu, kutokana na TFF yenyewe kujiridhisha kusimamisha mara kwa mara mechi za michuano hiyo kunapunguza msisimko na ladha ya kimashindano.  
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea keshokutwa kwa mechi kati ya Azam FC na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na Yanga na Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

AFRICAN SPORTS, MWADUI FC KUCHEZA FAINALI JUMAPILI



Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
TIMU za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.
Mwadui imepanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

Nazo timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.

DEWJI AWAOMBA UTULIVU MASHABIKI SIMBA


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema kikosi cha timu yao ni bora lakini kuna mambo kadhaa ya kufanya na wanachama na mashabiki wanahitaji utulivu.



Dewji amesema wakati uongozi wa sasa unaingia madarakani, Simba haikuwa katika kiwango kizuri kwa zaidi ya miaka miwili nyuma.

"Tunalazimika kutengeneza timu, kufanya mabadiliko na wakati huo huo kuna presha ya kutaka kushinda.

"Ninaamini kutakuwa na mabadiliko makubwa katika mzunguko wa pili. Lakini wanachama na mashabiki, wavute subira kidogo.

"Utaona timu inaanza kuimarika, hata uchezaji wake si kama mechi nne tano zilizopita. Pia wakumbuke tuna kocha mpya na ndiyo anaanza kuzoea kwa kuwa hana hata mechi sita za Ligi Kuu Bara," alisema.

Katika siku za hivi karibuni, Dewji amekuwa akionekana kuwa karibu na timu zaidi na alionekana na kikosi hicho mjini Morogoro, kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Moro.

BAHANUZI MCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA

Kiungo wa timu ya Coastal Union, John Mahundi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Disemba 2014 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Mahundi alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Coastal Union mwezi Disemba mwaka jana na kuchaguliwa na jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi.
Aidha mshambuliaji wa timu ya Polisi Morogoro, Said Bahanuzi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari 2015 wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea kutimua vumbi mzunguko wa 15 kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Bahanuzi anayechezea timu ya Polisi Morogoro kwa mkopo akitokea timu ya Young Africans amekua na mchango mkubwa kwa timu yake tangu kujiunga nayo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini.
Kwa kuibuka wachezaji bora, Mahundi na Bahanuzi watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

KURASA ZA MWANZO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMANNE FEB 17

.
.
.
.
.
.


.
.

MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA, SASA KUIVAA ARSENAL


MANCHESTER United imetoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 3-1 hivyo kutinga Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Preston Noth End usiku huu na sasa watakutana na mabingwa watetezi, Arsenal.
Scott Laird alitangulia kuwafungia wenyeji, Preston dakika ya 47 akimtungua kwa shuti la kubabatiza kipa David de Gea, kabla ya Ander Herrera kuisawazishia United dakika ya 65 akifumua shuti lililowapita mabeki wa Preston na kipa wao.
Marouane Fellaini akaifungia bao la pili Manchester United dakika ya 72, kabla ya Wayne Rooney kusababisha penalti dakika za lala salama na kwenda kufunga mwenyewe.
Former Everton man Fellaini celebrates his winning goal in front of the travelling supporters at Deepdale
Fellaini akishangilia baada ya kuifungia Man United bao la pili

RATIBA ROBO FAINALI KOMBE LA FA 

Liverpool vs Blackburn
Bradford vs Reading
Manchester United vs Arsenal
Aston Villa vs West Brom

Mechi zitachezwa Machi 7 na 8.
Sasa Man United itakutana na mabingwa watetezi wa Kombe la FA, Arsenal katika Robo Fainali Uwanja wa Old Trafford.
Mechi nyingine za Robo Fainali zinatarajiwa kuwa kati ya Liverpool na Blackburn, Bradford na Reading na Aston Villa dhidi ya West Brom. Mechi za Robo Fainali Kombe la FA zinatarajiwa kuchezwa Machi 7 na 8, mwaka huu.

Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Herrera, Fellaini, Di Maria/Rooney na Falcao/Young dk60.

Preston; Stuckmann, Humphrey, Huntington, Clarke, Wright/Wiseman dk75, Welsh, Kilkenny/Reid dk75, Gallagher, Laird, Davies/Robinson dk75 na Garner.