SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jan 17, 2016

NIYONZIMA AOMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI YANGA

KIUNGO Haruna Hakizimana Fadhil
Niyonzima ameomba msamaha Yanga
SC na kuahidi kutorudia kuikwaza
klabu kwa namna yoyote.
Mwezi uliopita, Yanga SC ilitangaza
kuvunja Mkataba na Nahodha huyo
wa Rwanda kwa tuhuma za kukiuka
vipengele vya Mkataba wake.
Lakini leo katika Mkutano na
Waandishi wa Habari makao makuu
ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam,
Niyonzima ameomba msamaha ili
arejeshwe kundini.

“Ninapenda kuchukua fursa hii
kuomba msamaha kwa uongozi,
benchi la ufundi na wachezaji
wenzangu pamoja na wanachama na
wapenzi. Ninaipenda timu yangu na
ninapenda kuendelea
kuitumikia,
”amesema.
Aidha, Niyonzima amesema kwamba
kulitokea kutoelewana kimawasiliano
na ofisi ya Katibu Mkuu, Dk Jonas
Tiboroha kiasi cha kulifikisha suala
hilo kwenye hatua hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya
Habari na Mawasiliano ya Yanga SC,
Jerry Muro amesema kwamba suala la
Niyonzima limefika katika uongozi
mkuu wa klabu na lipo katika hatua
nzuri.

Ingawa Muro hakuweza wazi, lakini
inavyoonekana muda si mrefu Yanga
itatangaza kuzika tofauti zake na
mchezaji huyo na kumrejesha kundini
rasmi.

MKUDE ATOA YA MOYONI BAADA YA KUFUKUZWA KERRY

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude,
ameonyesha masikitiko yake kwa mtindo
ulioanza kuzoeleka ndani ya Simba wa
ingia toka ya makocha kila uchao, akidai
inawavuruga, licha ya kwamba
wachezaji ni kama wanajeshi na katu
hawapaswi kuchagua pori la kupigania
vita.

Mkude alisema wachezaji wa Simba
wapo kwenye wakati mgumu, ingawa
jukumu lao ni kusimama imara ili kuona
timu yao inajenga heshima katika soka
la Bongo.
“Ukisikia utu uzima na kujielewa ndiyo
kipindi hiki ambacho tunakipitia
wachezaji wa Simba, kwani
kubadilishiwa makocha katikati ya
mechi ni mtihani kitu cha ziada ni kutoa
ushirikiano wa haraka kwa kocha
anayekabidhiwa kwetu kwa wakati
husika,” alisema.

Mkude alisema utakuwa msimu mgumu
kwao hasa wakiwa na nia ya kutimiza
kiu ya mashabiki wao wanaolilia
ubingwa. Lakini kwa kitendo cha
kuingia na kuondoka kwa makocha
kunawaumiza na kujikuta muda mwingi
wanatumia kuzoea makocha badala ya
kusonga mbele.

“Sisi tutakuwa tunafanya kazi ya
kuwakumbuka makocha wanapoondoka
na kuwazoea wanaoingia kama
binadamu inatugharimu, hata hivyo
tutapambana na tunaamini tutamzoea
Jackson Mayanja kama ambavyo
tuliwazoea makocha kina Patrick Phiri
na wenzake waliopishana Msimbazi,”
alisema. Mkude pia aliwataka
wanachama na kila mdau wa Msimbazi
kushirikiana pamoja ili kuivusha Simba
katika kipindi hiki ikiusaka ubingwa wa
Ligi Kuu baada ya kuukosa kwa misimu
mitatu iliyopita.

NIYONZIMA KUFANYAKIKAO NA WANACHAMA WA YANGA LEO

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima
atazungumza na wanachama na
mashabiki wa Yanga jijini Dar es Salaam,
leo.
Niyonzima anatarajia kufanya hivyo katika
mkutano wa waandishi wa habari
uliopangwa kufanyika jijini Dar.
Mpashaji mmoja amesema huenda
Niyonzima akafanya mkutano huo makao
makuu ya klabu ya Yanga.

"Sina uhakika sana, lakini mkutano huo
unaweza kufanyika palepale klabuni na
Niyonzima ndiye atakuwa mzungumzaji
mkuu," alitoa taarifa hiyo, mpashaji.
Taarifa zinaeleza, Niyonzima ambaye ni
nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda
ameamua kufanya hivyo kwa lengo la
kumaliza mgogoro.

Hadi sasa, klabu ya Yanga imeishatangaza
kuvunja mkataba na Niyonzima kwa madai
ya utovu wa nidhamu.
Lakini taarifa zinaeleza, hadi sasa bado
uongozi wa Yanga haujampa barua ya
kuvunja mkataba huo hadi sasa.