SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 12, 2015

KOCHA SIMBA ANENA

KOCHA Mkuu wa Simba Mserbia, Goran Kopunovic, amewataka wachezaji wa timu hiyo kutojikuza na badala yake wanatakiwa kupambana na kujituma kwa lengo la kushinda mechi za ligi ili wapate mafanikio.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Morogoro Kopunovic alisema juhudi na kila mchezaji kufahamu majukumu yake ndiyo silaha pekee itakayowapa mafanikio na hatimaye kutimiza ndoto.
Alisema kuwa anawakumbusha wachezaji wake kutoidharau timu yoyote katika ligi hiyo ambayo mechi zote wanazocheza zina ushindani.
Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic kushoto akiwa na wachezaji wake

" Ligi ni ngumu na ina ushindani, nawaeleza mara kwa mara wajitume na wajue kwamba wao bado wako chini na hakuna anayepaswa kujiona  ni bora", alisema Kopunovic.
Kocha huyo naye aliungana na Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van der Pluijm, kuuponda Uwanja wa Jamhuri kuwa hauna ubora na unasumbua wachezaji wake kucheza soka la kuburudisha.
Kopunovic pia aliuponda uwanja wa Mkwakwani Tanga kuwa unafanya wachezaji wacheze kulingana na miundombinu ya uwanja huo na si vile walivyofundishwa.
 
Simba iko mkoani Morogoro tangu jana kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Polisi Morogoro ambayo inatarajiwa kufanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani humo.
Wenyeji Polisi Morogoro wanaofundishwa na Adolph Rishard watashuka dimbani wakiwa na pointi 18 wakati Simba wana pointi 17.

YANGA YA PRESHA JUU SASA YATUMIA VIWANJA VIWILI KWA AJILI YA MAZOEZI


Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema watakuwa wakichanganya mazoezi yao katika viwanja vya Karume na Taifa jijini Dar.

Yanga imeanza rasmi kujiwinda kwa ajili ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ya Botswana itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Pluijm amesema wameamua kufanya hivyo kwa malengo tofauti kwa kuwa Taifa ndiyo watakaochezea mechi dhidi ya Waswana nao lakini Karume itawasaidia kumiliki mpira.
“Eneo la kuchezea na Karume ni bora zaidi, tukicheza pale ni lahisi wachezaji kupata mazoezi ya kutosha hasa katika suala la kumiliki mpira.
“Unapocheza nyumbani, lakini uwe na uhakika wa kukaa na mpira muda mwingi. Hauwezi kushambulia kama hauna mpira.
“Nyumbani lazima ushinde, hivyo tumeanza kufanya mazoezi ya aina tofauti,” alisema.

KOPUNOVIC AFURAHIA KURUDI KWA KIUNGO WAKE TEGEMEZI SIMBA


Kocha Goran Kopunovic amesema kiungo wake Saidi Ndemla atakuwa fiti kabla ya kuivaa Polisi Moro.

Simba ina kibarua Jumapili dhidi ya timu hiyo ngumu kutoka mkoani Morogoro.
Kopunovic amesema kwa kuwa Ndemla ameanza mazoezi kwa zaidi ya siku tatu sasa, anaamini atakuwa fiti.
“Atakuwa fiti hasa kama hakutakuwa na tatizo hapa katikati. Kurejea kwake kunafanya kwue na upana wa uchaguzi.

“Timu inapokuwa na majeruhi wengi ni tatizo kwa kocha, uchaguzi wa nani umtumie au fomesheni ipi uchague linakuwa tatizo,” alisema Kopunovic.

LAMBERT AFUNGASHIWA VIRAGO

 
Aston Villa imemtimua kocha wake Paul Lambert baada ya Klabu hiyo kushuka kwenye Msiamo wa ligi kuu England na kuwa hatarini kushuka daraja
Villa ilipoteza mchezo kwa kupigwa Mabao mawili kwa sifuri na Hull city siku ya jumanne, ikiwa ni mechi yao ya 10 bila kuondoka na ushindi
Mskoti huyu aliteuliwa mwaka 2012, na kusaini mkataba ambao utamalizika mwezi June mwaka 2018.
Kocha wa kikosi cha kwanza Scott Marshal na Kocha wa Magolikipa Andy Marshall wanashikilia nafasi ya Lambert kwa sasa

ZIPO HAPA KURASA ZA KWANZA NA ZA MWISHO MAGAZETI YA MICHEZO LEO FEB 12

.
.
.
.
.
.
.
DSC09373
.
.
.
.
.
.
.

HUYU NDIYE HANDSOME EPL

259187B300000578-0-image-a-4_1423658741197

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ametajwa kuwa mchezaji mwenye mvuto kuliko wote wanaocheza kwenye ligi ya England katika utafiti uliofanywa miongoni mwa mashabiki hususan wa kike nchini England .
Utafiti huu ulihusisha jumla ya wanawake 250 raia wa Marekani ambao waliulizwa maswali juu ya wachezaji wanaodhani wana mvuto wa kimapenzi nchini England na utafiti huo ulimuonyesha nyota huyu Mfaransa kuwa na mvuto kuliko wote .
Wakati alipoarifiwa juu ya kutwaa tuzo hii isiyo rasmi ya mchezaji mwenye mvuto wa kimapenzi kuliko wote , Olivier Giroud alipewa zawadi ya kioo cha dhahabu na hakusita kuwashukuru wazazi wake wawili kwa kumzaa na kumfanya kuwa na mvuto huu ambao leo umekubalika kuwa bora kuliko wachezaji wote kwenye ligi ya England .
2591873200000578-0-image-a-5_1423658746412
Giroud pia aliwashukuru watu wengine kama kinyozi wake , mtaalamu wake wa masuala ya make-up, mbunifu wake wa mitindo pamoja na msaidiz wake wa masuala ya picha watu ambao kijumla wanatengeneza timu inayiomfanya aonekane kuwa na mvuto huu alio nao .
Giroud hakuwa mwenyewe kwenye utafiti huu na kuna wachezaji wengine waliotambuliwa kuwa na mvuto akiwemo mchezaji wa Sunderland Santago Vergini ambaye alishika nafasi ya pili  na nyota wa Leicester City Matty James ambaye alishika nafasi ya tatu .

ALICHOSEMA ALI KIBA KUHUSU KUFANYA COLLABO NA WASANII WA AFRIKA

..

Kuna time utakuwa unajiuliza maswali kuwa kuna umuhimu gani kwa  wasanii wa hapa Tanzania kufanya kolabo na mastaa wa Afrika .
Sasa staa wa Bongo Fleva Ali Kiba amejibu swali lako na kusema;‘Katika kutangaza muziki inasaidia kiasi fulani lakini sio sana, muziki unaweza ukautangaza hata wewe mwenyewe, mimi binafsi muziki wangu nimeutangaza mbali sidhani kama Afrika hainijui bali inanifahamu sema tu kiukweli video zangu nilizokuwa nafanya hazikuwa katika quality nzuri huo ni ukweli naujua kwa hiyo sasa hivi tuko vizuri katika kujipanga nahakikisha kila kitu kitakuwa poa, hiyo inasaidia sana vile vile kubadilisha muziki na kuutangaza muziki wako katika msanii yoyote  ambaye umemchukua labda wa Congo, Nigeria, Uganda, sehemu nyingine nyingi  ili watu waweza kukusikiliza kwa urahisi na vile vile  ni support kubwa inaonesha jinsi gani una ushirikiano na watu wengine‘-Alisema.

BARCELONA YAIKALISHA VILLAREAL 3-1

TIMU ya Barcelona imeifunga mabao 3-1 Villarreal katika Nusu Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme, maarufu Copa del Rey usiku huu Uwanja wa Nou Camp.
Ushindi huo wa 10 mfululizo katika mashindano yote kwa vigogo hao wa Hispania ulitokana na mabao ya Lionel Messi, Andres Iniesta na Gerard Pique.
Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Muargentina Messi alifunga bao la kwanza dakika ya 41, kabla ya Villarreal kusawazisha kupitia kwa Manu Trigueros dakika ya 48.
Andres Iniesta akaifungia Barcelona bao la pili dakika tatu baadaye kabla ya Gerard Pique kukamilisha ushindi wa 3-1 dakika ya 65.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Ter Stegen, Alves, Pique, Mathieu, Alba, Rafinha/Rakitic dk69, Mascherano, Iniesta, Messi, Suarez na Neymar.
Villarreal: Asenjo, Mario, Musacchio, Victor Ruiz, Costa, Jonathan dos Santos, Pina, Bruno/Trigueros dk33, Cheryshev/Gomez dk74, Giovani dos Santos/Rukavina dk52 na Vietto.
Barcelona beat Villarreal at the Nou Camp in the Copa del Rey semi-final first leg
Wachezaji wa Barcelona wakifurahia ushindi wao dhidi ya Villarreal Uwanja wa Nou Camp katika Nusu Fainali ya Copa del Rey.
 
 
 Gerard Pique runs away in celebration after scoring at the Nou Camp for Barcelona 
 
 Barcelona's Lionel Messi celebrates scoring against Villarreal with Luis Suarez (right) at the Nou Camp
 
 Andres Iniesta of Barcelona celebrates after scoring during the Copa del Rey semi-final first leg match against Villarreal

CHRIS SMALLING APIGA MBILI MAN UNITED IKIUA 3-1 ENGLAND

TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Old Trafford.
Sifa zimuendee beki Chris Smalling aliyekuwa katika kiwango cha juu leo na kufunga mabao mawili peke yake, dakika za sita na 45, wakati bao la tatu la United lilifungwa na Robin van Persie kwa penalti.
Bao pekee la Burnley katika mchezo huo, lilifungwa na Danny Ings dakka ya 12, ambalo lilikuwa la kusawazisha kabla ya kuongezwa mawili.
Chris Smalling rises above the Burnley defence to score United's second goal on Wednesday night
Chris Smalling akienda hewani kuifungia Man United bao la pili 

Substitute Smalling scored with his first touch of the ball after replacing injured Jones 
 
 Ings peeled away from Smalling to convert a cross from Kieran Trippier in the 12th minute
 Robin van Persie sealed victory from the spot after Angel di Maria had been upended by Scott Arfield
 

WILLIAN AITAKATISHA CHELSEA LIGI KUU ENGLAND

BAO la dakika za lala salama la Willian, limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Everton usiku huu katika mcheo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Toffees walifungwa bao hilo baada ya kumpoteza mchezaji wake, Gareth Barry aliyetolewa kwa kadi nyekundu na sasa The Blues wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi saba zaidi.
Steven Naismith alikuwa mwenye bahati baada ya kuepuka adhabu licha ya kuunawa mpira kwenye boksi la Everton kipindi cha kwanza. 
Kiungo mpya, Juan Cuadrado alianza kwa amra ya kwanza leo tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 27 Chelsea kutoka Fiorentina na akavutia.
Willian is jubilant as he celebrates his late winner with substitute Didier Drogba, sending Stamford Bridge into pandemonium in the process
Willian akishangilia na Didier Drogba baada ya kufunga
 Willian takes a moment to look to the heavens after sealing a precious victory in Chelsea's title charge
 Ivanovic also grabbed the Everton substitute round the neck in an ugly incident which could have repercussions for the Serb

MAN CITY WANG'AA UGENINI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wameibuka leo na kushinda mabao 4-1 dhidi ya Stoke Uwanja wa Britannia huo ukiwa ushindi wa kwanza tangu mwaka mpya. 
Sergio Aguero aliwafungia wageni bao la kwanza dakika ya 33, kabla ya Peter Crouch kuisawazishia timu ya Mark Hughes dakika ya 38, hilo likiwa bao lake la sita msimu huu.
City ikapata bao la pili dakika ya 10 kipindi cha pili kupitia kwa James Milner, kabla ya Aguero kufunga la tatu kwa penalti dakika ya 55 na Samir Nasri la nne dakika ya 76.
Midfeidler Nasri roars towards the crowd after setting up Milner to score as David Silva celebrates behind him
Kiungo, Nasri akishangilia baada ya kuifungia Man City bao la nne
 
Sergio Aguero made it 3-1 to Manchester City from the penalty spot as the visitors opened up a two-goal lead against StokeSamir Nasri scores Manchester City's fourth of the evening at the Britannia as Manuel Pellegrini's side returned to winning ways

 The former Atletico Madrid striker celebrates after netting his second of the match and City's third