SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Apr 28, 2015

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO JUMANNE ZIPO HAPA

DSC01886 DSC01887 DSC01888 DSC01889 DSC01890 DSC01891

TAMBWE AZIDI KUWAUMIZA ROHO SIMBA

Tambwe akipewa mpira
AMISSI Tambwe ameendelea kuonesha thamani yake na kuwadhihirishia Simba kuwa yeye ni mfungaji hatari baada ya jana kupiga magoli matatu ‘hat-trick’ katika ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Polisi Moro.
Yanga walichukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/2015 baada ya ushindi wa jana wakifikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Mwaka jana Simba walimuacha Tambwe katika mazingira ya utata akiwa ndiye mfungaji bora na dakika za mwisho za dirisha dogo la usajili desemba mwaka jana Yanga wakamsajili kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja.
Katika mechi tatu zilizopita, Tambwe amefunga magoli nane na kufikisha magoli 14 katika msimu huu mgumu wa ligi kuu.
Alifunga manne katika ushindi wa 8-0 dhidi ya Coastal, akatia kambani moja kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya Stand United na jana akapiga tatu dhidi ya Polisi Moro.
Baada ya kufanikiwa kwa muda mfupi ndani ya Yanga, Tambwe amesema anafurahia maisha ndani ya Yanga na ataendelea kufanya vizuri.
“Nashukuru nimefunga ‘Hat-trick’ yangu ya pili msimu huu, nikiwa Simba nilifunga ‘hat-trick’ mbili pia, kwangu haya ni mafanikio, nilipochukua kiatu cha dhahabu mwaka jana nilisikitika kuachwa na Simba, kichwa changu hakikuwa sawa”, Amesema Tambwe na kusisitiza: “Leo hii (jana) nachukua ubingwa Yanga nikifunga magoli muhimu, namshukuru Mungu, wachezaji wenzangu, mashabiki na viongozi, wanaonesha upendo mkubwa kwangu”.

MSUVA AZUNGUMZIA GOLI LAKE LINALO FANANA NA LA VAN PERSIE

NgassanaMsuva
SIMON Happygod Msuva amesema anajisikia furaha kuchukua ubingwa huku goli lake alilofunga kwa kichwa dhidi ya Ruvu Shooting likijadiliwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kufananishwa na alilofunga mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi, Robin van Persie kwenye fainali za kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil.
“Watu wanasema nilifunga kama Robin Van Persie, wanajadili sana kwenye mitandao, haya ni mafanikio kwangu, juhudi ndio siri ya mafanikio” Amesema Msuva.
Winga huyo anayeongoza orodha ya wafungaji akiwa amefumania nyavu mara 17 msimu huu akifuatiwa na Amissi Tambwe mwenye magoli 14 ameongeza kuwa ubingwa waliopata anafurahi kuchangia kwa kiasi kikubwa na ataendelea kufanya vizuri.
“Huu ni mwanzo tu, kila siku najifunza na kupunguza makosa, tuna kocha mzuri, tunaamini tutafanya vizuri zaidi siku zijazo tukianzia na mechi ijayo dhidi ya Etoile du sahel”. Amesema Msuva.

SHANGWE ZA UBINGWA YANGA RAHA TUPU WACHEZAJI, MAKOCHA HADI MASHABIKI





JOHN TERRY 'ANAVYOMSUTA' BENITEZ AELEKEA KUCHEZA MECHI 38 ZA MSIMU BILA TATIZO

MIAKA miwili ilitopita, kocha Rafa Benitez alipokuwa wa Chelsea mustakabali wa beki John Terry ulikuwa shakani Stamford Bridge.
Aprili mwaka 2013, kocha huyo Mspanyola alisema kwamba hawezi kuendelea kumchezesha mechi mbili kwa wiki na uamuzi huo wa utata ulitokana na maumivu ya goti ya mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa England. 
Terry alichezeshwa mechi 14 tu katika msimu wa 2012-2013 kwenye klabu hiyo kipenzi. Leo mwaka 2015, Nahodha huyo wa Blues anakarinia kuinua taji la Ligi Kuu ya England akiwa ametoa mchango wake katika mechi kati ya 33 ilizocheza Chelsea hadi sasa.
Na sasa mkongwe huyo anaelekea kucheza mechi zote 38 za msimu wa Ligi Kuu Chelsea. hakika ni jambo la kujivunia kwake.
Chelsea captain John Terry is on course to appear in all 38 Premier League matches for his side this season
Nahodha wa Chelsea, John Terry anaelekea kucheza mechi zote 38 za Ligi Kuu msimu huu