SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 30, 2015

UMAARUFU WA RAMADHANI SINGANO NA MAHALI ANAPOISHI HAVIFANANI

sing8
Chumba anacholala Singano na Kaka yake Hais Ramadhani
UMAARUFU ni kama utumwa! huwezi kuwa huru kama una jina kubwa, halafu maisha yako ni ya kawaida tu.
Kuna idadi kubwa ya wachezaji maarufu wa mpira wa mguu nchini, pia wapo wanamuziki n.k, lakini maisha wanayoishi ni tofauti na majina yao. Ni maisha ya kiwango cha chini.
Katika soka la Bongo, huwezi kutaja wachezaji wenye majina makubwa kwasasa ukaliacha jina la Ramadhani Singano ‘Messi’.
sing 10
Singano akiwa na majirani zake
Uwezo wa kupiga chenga, pasi, kasi na staili yake ya uchezaji ya kutumia mguu wa kushoto akitokea winga ya kulia ni vitu vinavyofanya Singano aonekana mahiri kusakata kabumbu.
Kila mtu kwasasa anajua kwamba Singano ana matatizo ya kimkataba na klabu yake ya Simba na tulieleza kwa undani siku ya jana.(Rejea habari za jana).
Katika stori yetu ‘exclusive’ na Singano jana, tuliahidi kuendelea na sinema ya suala lake na leo tunakuletea sehemu ya pili ya maisha yake binafsi.
Singano anaishi  kwa ndugu yake eneo la Keko, Machungwa jijini Dar es salaam.
Kiukweli; maisha anayoishi Singano yanasikitisha mno, hana nyumba, badala yake ameomba hifadhi kwa kaka yake, Hamis Ramadhani ambaye pia anamsimamia mambo yake (Meneja).
Hamis na Singano ni ndugu wa damu, wamezaliwa na mama mmoja baba tofauti.
sing13
Baadhi ya picha za ukutani chumbani kwa Singano
Moja ya vipengele katika mkataba wa Singano ni kupatiwa kodi ya nyumba, lakini katika maisha yake yote toka asaini mkataba huo Mei 1, 2013 hajawahi kupewa hata shilingi kama anavyothibitisha mwenyewe; 
“Kipengele cha kulipiwa kodi ya nyumba hakijatekelezwa, niliuandikia barua uongozi wa Aden Rage toka mwaka jana, lakini mpaka sasa naona kimya. Nashangaa kitu kimoja; uongozi huu wa Rais Aveva (Evans) baada ya kuingia madarakani unasema ulipokea nyaraka zote, sasa vipi barua yangu ya kudai stahiki zangu hawakupewa au hawajaiona?”
sing 11
SWALI: Singano, mtandao wetu umefika unapoishi hapa Keko -Machungwa na kushuhudia maisha yako halisi, dhahiri mazingira haya hayafanani na umaarufu wako, unaishi chumba kimoja na kaka yako wakati kuna kipengele cha kupewa kodi ya nyumba na hukijatimizwa, una lipi la kuwaambia Wachezaji wa Kitanzania na Watanzania wote?.
Singano: “Mimi kidogo nipo tofauti na wengine, kwanza kabisa wanichukulie mtu wa kawaida, wasiamini kile wanachokiona kwenye magazeti au media. 
Kwa jina langu mimi Ramadhani Singano Messi watu wanaweza kutegemea naishi vizuri, maisha ya hali juu, hapana! siwezi kuigiza, maisha yangu ni ya  chini sana.
Naishi kawaida sana, nikiamka asubuhi naenda kuswali, nikirudi nakaa nyumbani tu. Chumba tunalala chumba kimoja na kaka yangu, wakati kwenye mkataba wamesema nitalipiwa nyumba. Nimeomba hifadhi kwa kaka yangu. Labda watu watahisi kuna watu wananitumia, hapana!, ninadai haki zangu, tuweke sawa mambo ya kimkataba ili niwe huru na kuendelea kuongea na klabu yeyote”.
Kwa mazingira anayoishi Singano na wengine wengi, ni wazi kwamba wachezaji kibao wanajikuta wanashuka kiwango bila sababu. 
Mchezaji hawezi kuwa  huru, hawezi kuwa sawa kisaikolojia , muda wote anawaza namna ya kuikabili presha ya watu.
Kila mtu anamjua na wengine wanahitaji kumtembelea nyumbani kwasababu ni marafiki wa kimpira, wanamheshimu sana, lakini anapoishi hapana hadhi kabisa, hivyo anaogopa kuwakaribisha moja kwa moja. Utacheza vizuri kwa wakati wote?
Mazingira anayoishi Singano
sing5sing4sing 1sing3sing2

SIMBA SC YASAJILI KIPA WA JKU MIAKA MIWILI


Kipa wa JKU ya Zanzibar, Mohammed Abraham Mohammed (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ofisini kwake, Mbezi, Dar es Salaam mara baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo leo.
Abraham wakati anasaini Mkataba mbele ya Hans Poppe leo Mbezi, Dar es Salaam. Tayari Simba SC ina makipa wanne, Ivo Mapunda, Hussein Sharrif 'Casillas', Peter Manyika na Dennis Richard.

May 29, 2015

KURASA ZA MAGAZETI YA MICHEZO LEO MAY 29

DSC03071 DSC03072 DSC03073 DSC03074 DSC03075 DSC03076
MESSI ALIVYOJIVINJARI UFUKWENI NA DEMU WAKE MJAMZITO SAMBAMBA NA MTOTO WAO WA KIUME A+ A- Print Email Wanasoka kadhaa barani Ulaya tayari wameshajitosa ufukweni wakiwa wamemaliza msimu wao, lakini supastaa wa Barcelona, Lionel Messi nae ameamua kupata wasaa wa kupunga upepo 'beach' ingawa bado ana mataji mawili ya kupigania ndani ya siku tisa zijazo. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina - ambaye ameng'ara na kutupia wavuni mabao 56 msimu huu, alikuwa kwenye ufukwe jijini Barcelona yeye na mpenzi wake Antonella Roccuzzo sambamba na mtoto wao wa kiume Thiago. Messi na wachezaji wenzake wa Barcelona wataikabili Athletic Bilbao Jumamosi hii katika fainali ya Copa del Rey itakayopigwa Nou Camp kabla ya kuikabili Juventus kwenye fainali ya Champions League itayochezwa Berlin Ujerumani wiki moja baadae. Lionel Messi and his girlfriend Antonella Roccuzzo enjoyed some time together at the beach in Barcelona Lionel Messi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo wakipunga upepo ufukweni The couple looked on as their son Thiago played in the sand nearby as Messi prepares for two cup finals Hapa wakimtazama mototo wao Thiago akicheza mchangani Pregnant Antonella soaked up the sun on the beach while enjoying a low-key day out on Thursday Antonella akijivinjari beach na kitumbo chake Growing brood: The pair are expecting their second child, reportedly a boy who they will call Benjamin Messi na mpenzi wake wanategemea mtoto ajae ataitwa Benjamin Antonella laid a protective hand on her bump as he reclined on her four-time Ballon d'Or winning partner Antonella na Messi Antonella, Messi na mtoto wao Thiago

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/messi-alivyojivinjari-ufukweni-na-demu.html
Copyright © saluti 5
MESSI ALIVYOJIVINJARI UFUKWENI NA DEMU WAKE MJAMZITO SAMBAMBA NA MTOTO WAO WA KIUME A+ A- Print Email Wanasoka kadhaa barani Ulaya tayari wameshajitosa ufukweni wakiwa wamemaliza msimu wao, lakini supastaa wa Barcelona, Lionel Messi nae ameamua kupata wasaa wa kupunga upepo 'beach' ingawa bado ana mataji mawili ya kupigania ndani ya siku tisa zijazo. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina - ambaye ameng'ara na kutupia wavuni mabao 56 msimu huu, alikuwa kwenye ufukwe jijini Barcelona yeye na mpenzi wake Antonella Roccuzzo sambamba na mtoto wao wa kiume Thiago. Messi na wachezaji wenzake wa Barcelona wataikabili Athletic Bilbao Jumamosi hii katika fainali ya Copa del Rey itakayopigwa Nou Camp kabla ya kuikabili Juventus kwenye fainali ya Champions League itayochezwa Berlin Ujerumani wiki moja baadae. Lionel Messi and his girlfriend Antonella Roccuzzo enjoyed some time together at the beach in Barcelona Lionel Messi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo wakipunga upepo ufukweni The couple looked on as their son Thiago played in the sand nearby as Messi prepares for two cup finals Hapa wakimtazama mototo wao Thiago akicheza mchangani Pregnant Antonella soaked up the sun on the beach while enjoying a low-key day out on Thursday Antonella akijivinjari beach na kitumbo chake Growing brood: The pair are expecting their second child, reportedly a boy who they will call Benjamin Messi na mpenzi wake wanategemea mtoto ajae ataitwa Benjamin Antonella laid a protective hand on her bump as he reclined on her four-time Ballon d'Or winning partner Antonella na Messi Antonella, Messi na mtoto wao Thiago

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/messi-alivyojivinjari-ufukweni-na-demu.html
Copyright © saluti 5
MESSI ALIVYOJIVINJARI UFUKWENI NA DEMU WAKE MJAMZITO SAMBAMBA NA MTOTO WAO WA KIUME A+ A- Print Email Wanasoka kadhaa barani Ulaya tayari wameshajitosa ufukweni wakiwa wamemaliza msimu wao, lakini supastaa wa Barcelona, Lionel Messi nae ameamua kupata wasaa wa kupunga upepo 'beach' ingawa bado ana mataji mawili ya kupigania ndani ya siku tisa zijazo. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina - ambaye ameng'ara na kutupia wavuni mabao 56 msimu huu, alikuwa kwenye ufukwe jijini Barcelona yeye na mpenzi wake Antonella Roccuzzo sambamba na mtoto wao wa kiume Thiago. Messi na wachezaji wenzake wa Barcelona wataikabili Athletic Bilbao Jumamosi hii katika fainali ya Copa del Rey itakayopigwa Nou Camp kabla ya kuikabili Juventus kwenye fainali ya Champions League itayochezwa Berlin Ujerumani wiki moja baadae. Lionel Messi and his girlfriend Antonella Roccuzzo enjoyed some time together at the beach in Barcelona Lionel Messi na mpenzi wake Antonella Roccuzzo wakipunga upepo ufukweni The couple looked on as their son Thiago played in the sand nearby as Messi prepares for two cup finals Hapa wakimtazama mototo wao Thiago akicheza mchangani Pregnant Antonella soaked up the sun on the beach while enjoying a low-key day out on Thursday Antonella akijivinjari beach na kitumbo chake Growing brood: The pair are expecting their second child, reportedly a boy who they will call Benjamin Messi na mpenzi wake wanategemea mtoto ajae ataitwa Benjamin Antonella laid a protective hand on her bump as he reclined on her four-time Ballon d'Or winning partner Antonella na Messi Antonella, Messi na mtoto wao Thiago

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/messi-alivyojivinjari-ufukweni-na-demu.html
Copyright © saluti 5

SASA NI RASMI SIMBA YAMTEMA MESSI


Kikosi cha Simba, rasmi kimetangaza kumtema kiungo wake Ibrahim Twaha ‘Messi’.

Messi alisajili na Simba misimu miwili iliyopita, lakini hakupata nafasi ya kutosha kuonyesha cheche zake.
Ingawa alianza kuonyesha cheche wakati wa Abdallah Kibadeni, baada ya Zdravko Logarusic kutwaa ‘madaraka, mambo yalibadilika.
Tokea hapo, Messi huyo wa Tanga aliendelea kupotea taratibu, hadi Simba ilipomtema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema, tayari wamempa ruksa.
“Kweli, Twaha tumemuacha aende. Unajua kama unaona inafikia unalazimika kufanya jambo fulani, basi ni vizuri kulifanya mapema,” alisema.

Hivi karibuni, Twaha amekuwa akisikika akisema kwambaa ana mpango wa kuachana na Simba, hivyo timu yoyote inaweza kumsajili kulingana na maelewano yao.

AZAM FC YAAJIRI MAKOCHA KUTOKA UINGEREZA

stewart
*Watoka Arsenal, Southampton za Uingereza
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
‘Baada ya muda mrefu wa fununu, Azam wamekata kiu leo na kuanika makocha wao wapya wanaotoka Uingereza.’

HII KUFURU! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya jana uongozi wa Azam FC kumtangaza Muingereza Stewart John Hall kuwa kocha mkuu mpya akisaidia na makocha kutoka klabu kubwa za soka ulimwenguni ikiwamo Arsenal ya Ligi Kuu ya England (EPL).
Baada ya muda mrefu wa kusubiri kitakachojiri, uongozi wa Azam kupitia kwa msemaji wake, Jaffar Idd Maganga, leo umetangaza kumrejesha Hall na mabadiliko mengine makubwa katika benchi la ufundi.

Maganga amesema kuwa Hall aliyewahi kuinoa Azam FC na kuipa mafanikio makubwa ukiwamo ubingwa wa msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (ingawa aliishia mzunguko wa pili na kumpisha Mcameroon Joseph Omog), amepewa mkataba wa miaka miwili na atakuwa akisaidiwa na Mganda George ‘Best’ Nsimbe.

“Kuna ongezeko na punguzo katika benchi la ufundi na idara ya utawala na fedha kutokana na uamuzi uliofanywa na uongozi wa Azam FC leo (jana),” amesema.
Mark Philip raia wa Uingereza aliyewahi kufanya kazi katika klabu ya Bolton Wanderers ya Uingereza na kituo cha kulea vijana wenye vipaji (Academy) cha klabu ya Aston Villa ya Uingereza pia, anakuwa kocha wa makipa wa Azam akisaidiwa na mzawa Idd Abubakar.

Philip mwenye leseni A ya UEFA katika ukocha, amepewa mkataba wa miaka miwili na matajiri hao wa Tanzania.

Aidha, Mromania Mario Mariana ameajiriwa kuwa kocha wa timu ya vijana ya Azam na atasaidiwa na wazawa Dennis Kitambi (aliyekuwa kocha mkuu wa Ndanda FC msimu uliopita kabla ya kutimkia Azam) na Idd Cheche.

Mariana mwenye leseni ya UEFA Pro katika ukocha, pia atakuwa akiionoa timu ya Azam ya wakubwa akiwa kocha wa viungo (Physical Fitness).
Katika idara ya utawala na fedha uongozi wa Azam FC umemwajiri Muingereza mwingine, El Bankya kuwa meneja wa idara hiyo.

Muingereza huyo mwenye asili ya Uganda aliyewahi kufanya kazi katika klabu za Arsenal na Southampton za EPL, amepewa mkataba wa miaka miwili pia.
“Waajiriwa wote wapya wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam Juni 8 na tutaanza rasmi kambi ya michuano ya Kombe la Kagame Juni 15 hapa Dar es Salaam,” amesema zaidi Maganga.

MUSSA MGOSI ‘MABAO’, ASAINI MSIMBAZI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imemsajili tena mshambuiaji wake wa zamani, Mussa Hassan Mgosi (pichani juu) leo hii, baada ya takriban misimu miwili mizuri akiwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo mjini Dar es Salaam kwamba wamemrejesha Mgosi kikosini baada ya kuvutiwa na juhudi zake akiwa Mtibwa.
“Kwa Mgosi, Simba ni nyumbani kwake. Alikuwa hapa, tukamuuza DC Motema Pembe (ya DRC), akarudi, akaenda Mtibwa. Na sisi, baada ya kuona bado ana uwezo wa kuisaidia timu yake, tumemrejesha,”amesema Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mgosi alisajiliwa na Simba SC mwaka 2005 kutoka Mtibwa Sugar na mwaka 2012 akauzwa DC Motema Pembe ya DRC, ambako alicheza kwa misimu miwili.
Mwaka jana, Mgosi alirejea nyumbani baada ya kumaliza Mkataba wake Kongo na kusaini timu yake ya zamani, Mtibwa- lakini baada ya kung’ara Manungu kwa misimu miwili, amerejeshwa kundini.
Mgosi anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Simba SC ndani ya wiki moja, baada ya awali klabu hiyo kuwasajili kiungo Peter Mwalyanzi kutoka Mbeya City, mabeki Samih Hajji Nuhu kutoka Azam FC na Mohammed Fakhi kutoka JKT Ruvu.
Bahati nzuri ilioyoje kwa Wekundu wa Msimbazi, kama ilivyokuwa kwa Mwalyanzi, Nuhu na Fakhi- Mgosi pia anarejea Simba SC kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Manungu. 

May 28, 2015

‘KAPTENI’ HANS POPPE AWASHUKIA MAWAKALA UCHWARA BONGO

Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI kamati ya usajili ya timu ya soka ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amewatolea uvivu wale wanaojiita `mawakala `wa wachezaji hapa nchini waliyoanza kujitokeza Nyakati hizi za Usajili wakipanga bei za Wachezaji bila kufuata utaratibu.
Amesema kuwa wakati huu ambapo baadhi ya wachezaji wanaongezewa mikataba na wengine kusajiliwa katika timu Mbalimbali wamejitokeza watu wanajitambulisha kuwa maajenti wa wachezaji ambao hupanga Bei za wachezaji huku wakiwa hawatambuliki na Shirikisho la Soka Nchini TFF pamoja na Klabu anayochezea Mchezaji.
Amedai kuwa alisikia taarifa kuwa wamemuongezea Mkataba `Kinyemela` Mchezaji Ramadhani Singano `Messi` huku yeye Mwenyewe akiwa hana taarifa jambo ambalo si sahihi na watahakikisha wanachukua hatua za kisheria kwa aliyezusha jambo hilo.
Amedai kuwa wao walimuongeza Mkataba Mchezaji wao ( Singano) na kumuongezea Mshahara lakini anasikitika kusikia walimuongezea mkataba Kinyemela jambo ambalo litaleta taswira mbaya kwa jamii.
``Sisi tulimuongezea Mkataba Mchezaji wetu Singano ikawa ni Maika mitatu na tulifuata taratibu zote,sasa tunashangaa anajitokeza mtu anajiita ajenti anasema mchezaji alimaliza mkataba wake na anasema tulighushi,hilo jambo ni baya sana hatutokubali kuzushiwa uongo wakati mchezaji tulimuongezea mkataba ili kuboresha mshahara wake ``,Alisema Hanspope kwa ukali.
Captain huyo mstaafu wa jeshi ( JWTZ) alitahadharisha kuwa kama TFF na Vilabu havitochukua hatua za haraka basi maajenti bandia wataendelea kujitokeza na kuharibu sura ya mchezo wa Soka Nchini.
Hans Poppe kulia amewajia juu mawakala uchwara nchini

USAJILI SIMBA SC;
KUHUSU usajili unaondelea Mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili amesema kuwa kwasasa wanaendelea kujaza nafasi zinazoonekana kutakiwa kujazwa na wanaangalia namna ya kuwapandisha baadhi ya wachezaji .
Amekiri kuwa ni kweli wapo katika mazungumzo na Mchezaji Balimi Busungu ambaye jana aliitwa katika Timu ya Taifa ambaye wamempa ofa yao na wanasubiri majibu ya mchezaji huyo.
Ameongeza kuwa kwasasa hawana wasiwasi wala haraka ya kusajili mchezaji kwa gharama kubwa sana na kwamba wamempa ofa mchezaji huyo kutoka Mgambo ya Tanga na endapo hatokubaliana nao hawatoangaika kumuongezea fedha kwakuwa wachezaji wenye viwango vikubwa wapo wengi.

TAIFA STARS;
Akitoa mawazo yake juu ya maendeleo ya Timu ya Taifa (TAIFA STARS) Pope amesema kuwa haoni sababu ya kumlaumu kocha mkuu wa timu hiyo Mart Nooj kwakuwa zipo sababu Nyingi zinazofanya Taifa Stars ifanye vibaya.
Amesema kuwa Michuano ya COSAFA siyo kigezo chakupima uwezo wa Mwalimu wa Timu ya Taifa huku akitetea kuachwa kwa baadhi ya wachezaji .
Ameongeza kuwa kuachwa kwa baadhi ya wachezaji katika timu ya Taifa kunategemea na mambo mengi na mojawapo ni tabia za baadhi ya wachezaji kutokuwa na Nidhamu ndani na Nje ya Uwanja.
``Mimi kwa mtazamo wangu sioni sababu ya kumlaumu mwalimu wa Timu ya Taifa eti kwasababu ya Michuano ya COSAFA,zipo sababu nyingi zinazotufanya tukwame ukiangalia huku chini tunapopswa kuanza wa watoto tumepuuza,yani tumepuuza mambo mengi sana ambayo inatupasa turudi nyuma kinyume na hapo tutafukuza makocha wengi sana``. Alisema .

SIMBA SC YASAJILI MABEKI WAWILI KWA MPIGO, MMOJA WA AZAM MWINGINE WA JKT RUVU


Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imesajili mabeki wawili wa Kizanzibari, Samir Hajji Nuhu wa kushoto na Mohammed Fakhi wa kati usiku wa leo.
Nuhu alikuwa mchezaji wa Azam FC kwa misimu miwili hadi msimu wa 2013/2014 kabla ya kuumia goti na kuondolewa katika usajili, wakati Fakhi msimu huu amechezea JKT Ruvu.
Mabeki hao vijana wadogo wamesaini leo mikataba ya kuitumikia Simba SC, Nuhu mwaka mmoja na Fakhi miaka miwili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba wanatarajiwa mambo mazuri kutoka kwa wachezaji hao vijana wadogo.
Fakhi akisaini SImba SC leo mbele ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch 

“Huyu Nuhu kwa wenye kumkumbuka alipokuwa Azam FC kabla ya kuumia. Na yeye ndiye aliyekuwa beki chaguo la kwanza upande wa kushoto. Lakini baada ya kupitia vipimo vyake na kujiridhisha kwamba amepona kabisa, tumempa nafasi nyingine,”amesema Poppe.
Aidha, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema Fakhi alikuwa beki tegemeo wa kati wa JKT Ruvu msimu huu na wengi walivutiwa na ukabaji wake mzuri.
“Mimi binafasi niseme ni mmoja kati ya watu waliopendezewa na ukabaji wa huyu kijana. Lakini si hivyo, kama utakumbuka mechi yetu ya mwisho  ya Ligi tulicheza na JKT Ruvu, hivyo baada ya mechi hata benchi la Ufundi lilimpendekeza huyu mchezaji,”amesema.
Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika watatu baada ya mwanzoni mwa wiki kusajiliwa kiungo wa Mbeya City, Peter Mwalyanzi.
Simba SC imekuwa na bahati ya kuwasajili wachezaji wote hao wote wakiwa huru baada ya kumaliza mikataba yao katika klabu zao. 
Nuhu akisaini Mkataba wa Simba SC leo mbele ya Frisch

May 27, 2015

HANS POPPE AMTOLEA UVIVU MENEJA WA MESSI, AMUAMBIA AWE MAKINI SANA

=

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemvulia uvivu meneja wa kiungo wao, Ramadhani Singano ‘Messi’ kwamba analazimika kuwa makini.

Hans Poppe amesema meneja huyo anapaswa kuwa makini kutokana na maneno aliyoyatoa kwamba mkataba wa mchezaji wake ‘umechezewa’.
“Kwa kweli anapaswa kuwa makini sana, maneno anayoyazungumza hayana ukweli na anapaswa awe na uhakika.
“Anaposema kuna ujanja umefanyika katika mkataba huo wakati uko TFF, maana yake TFF wanahusika kuufanyia ujanja.
“Tumegushi saini, tumegushi na dole gumba. Sidhani kama ni jambo zuri kuzungumza tu hayo mambo.
“Anapaswa kuwa makini, nasema hivi kumuasa lakini bado naweza kusema simtambui kwa kuwa sijui yeye Messi ana meneja na wala hajawahi kuutambulisha uongozi wa Simba,” alisema Hans Poppe.
Meneja huyo amekuwa akilalama kwamba mkataba wa Simba na Messi unapaswa kulazimika msimu huu lakini ulio TFF unaonyesha unamalizika mwakani yaani 2016.
Lakini ajabu Messi, ameshindwa kuonyesha nakala ya mkataba wake ambayo ingeweza kuonyesha kama kweli Simba wamekosea au la.

HARRY KANE ATOA MSIMAMO JUU YA KUSAJILIWA MAN UITED

harry-kane-tottenham-premier-league_3280053
Harry Kane:  aliifungia magoli 21 Tottenham  katika msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu England.
Harry Kane amesisitiza kuwa ataendelea kuichezea  Tottenham baada ya tetesi kuenea kwamba Manchester United wanavutiwa naye.
Mchezaji huyo bora kijana wa mwaka wa PFA amekumbana na swali kuhusu hatima yake ya baadaye mara tu baada ya kuwasili Malaysia kuelekea mechi ya kirafiki ya Spurs dhidi Malaysia XI.
Nyota huyo mwenye miaka 21 ameweka wazi kuwa ana nia ya kuendelea kuichezea Spurs chini ya kocha Mauricio Pochettino ambaye alimnoa vizuri msimu uliopita na kufunga magoli 21 sambamba na kucheza mechi ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.

May 26, 2015

HIVI NDIVYO VITA VYA SIMBA NA YANGA ILIVYO KUWA KUMWANIA PETER MWALYANZI

IMG-20150524-WA0012
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo mshambuliaji, Peter Mwalyanzi kutokea Mbeya City fc.
Mwalyanzi alisaini mkataba huo jana na baada ya hapo alifanya mahojiano maalumu na Sports Xtra ya Clouds fm na hapa chini ni baadhi ya mambo aliyozungumza:
Swali: Kabla hujawa Peter Mwalyanzi wa leo, ulianza kucheza mpira wapi?
Mwalyanzi anaeleza: “Nilianza kucheza mpira nikiwa shule, nilikuwa napenda sana mpira. Nilipomaliza kidato cha nne nikasajiliwa Kijiweni ya Mbeya, baadaye ikaja kuuzwa na kubadilishwa jina kuwa TMK. Minziro (Fred) alikuja Mbeya, kuna baadhi ya wachezaji ikabidi waondoke na ile timu, hawakutakiwa kuondoka watu wote, wakachagua watano na mimi nikiwemo.
Tulicheza TMK, lakini hatukufanikiwa kupanda ligi kuu, wakapanda Manyema , Africa Lyon na Majimaji, ambao tulikuwa tunacheza 9 bora pale uwanja wa Uhuru .
Wale wachezaji watano Mtemvu (Abass), wote   alikuwa anatukalisha Gesti, kwahiyo ikawa gharama, kwake na ikabidi wachujwe, nikabaki peke yangu TMK. Nilipoona ile timu haiangalii mbele zaidi,  nikasajili Pan Africa wakati huo kocha akiwa Juma Pondamali ‘Meansah’.
Kipindi ambacho tulikuwa  tunacheza tisa bora, tulikuwa na Mgambo JKT kabla ya kupanda ligi kuu. Waliniona na kuniita Tanga, hatimaye nikasajili pale.
Swali: Baada ya kusajiliwa Mgambo, msimu wako wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara ulikuwaje?
Mwalyanzi anaeleza: “Msimu wangu wa kwanza haukuwa mzuri pale Mgambo, mechi nne za kwanza zilikuwa ngumu kwangu, mwalimu alikuwa hanielewi kwasababu mpira wangu ulikuwa laini.
Alikuja kunipa nafasi kwenye mechi na Mtibwa Sugar, nikamuonesha kwamba alivyokuwa ananifikiria sivyo, baada ya mechi hiyo, Mgambo wakawa wananihitaji kuwepo  uwanjani kila mechi. Nilicheza misimu miwili Mgambo.
Swali: Baada ya kucheza misimu miwili Mgambo, zilitoka taarifa za Yanga na Simba kukuwinda, ilikuwaje?
Mwalyanzi: “Nilipomaliza msimu wa pili pale Mgambo, Yanga wakawa wananihitaji, nikaja mpaka huku Dar es salaam, nikafanya nao mazungumzo, lakini viongozi wakagawanyika, baadhi  walikuwa wananitaka  mimi wengine wanamtaka Hassan Dilunga, wakaonekana wa Dilunga wameshinda, Bin Kleb akaniambia wewe nenda tutakupigia Simu.
Swali: Baada ya Yanga kuachana na wewe, ulikwenda wapi?
Mwalyanzi: “Nikaenda Mbeya na kukaa huko. Prisons wakanipigia simu, tukakubaliana kila kitu, nikawaambia mimi nimemaliza ligi sasa hivi, sio ninyi pekee mlioniona, kuna timu nyingine kama Mtibwa, Coastal,  zote zimenipigia simu. Fanyeni haraka ili tumalize hii shughuli, wakasema sawa, lakini wao Mbeya sio makao makuu, inabidi wapate pesa kutoka Dar es salaam.
Nikakaa siku mbili, viongozi wa Mbeya City wakanipigia Simu, tukaongea nao na wakawa haraka, tukamalizana kila kitu, nikasaini mkataba kuitumikia  msimu uliokwisha mei 9 mwaka huu.
2
Swali: Kabla ya kutakiwa na Simba, ulipata ofa ngapi hapa katikati?
Mwalyanzi: Hapa katikati kabla ya kuja Simba nimepata ofa mbili kutoka Mwadui na Yanga. Watu wa kwanza kuwasiliana na mimi walikuwa Yanga. Ile mechi ya mwisho dhidi ya Polisi sikucheza kwasababu nilikuwa na majeruhi, siku hiyo akanipigia simu kiongozi wa Yanga, Aron Nyanda wakati timu yao inacheza mechi Mtwara, akaniambia kocha amesema anakutaka wewe Peter Mwalyanzi ili uchukue nafasi ya Mrisho (Ngassa) kwasababu una kasi inayofanana na yake.
Nikawa nawasiliana na Aron, lakini akawa hanielezi kwa ufasaha, anaongea na mimi kama mdogo wake tu. Nikawa namsikiliza tu,   kuna siku nikamtumia meseji nikimuuliza ‘Broo’ mboni kimya? Siku ya pili yake akanipigia simu, lakini sikuipokea kwasababu nilikuwa nje. Siku ya pili viongozi wa Simba wakanipigia simu, nikawa naongea nao kwa makini na jamaa alionekana yuko makini, akaniambia Simba tunakuhitaji si kwababu umetufunga mechi ya Mbeya, tumekufuatilia kwa muda mrefu.
Swali: Vita ya Simba na Yanga ilikuwaje siku mbili kabla ya kusaini Msimbazi?
Mwalyanzi: Jana (juzi) niliendea kuangalia mpira pale Mwenge-Mbeya, kuna watu wakaniambia utapigiwa simu na kutumiwa tiketi uende Dar. Mimi sikujua kitu na sikutaka kuuliza. Nikiwa pale Mwenge-Mbeya akanipigia simu kiongozi mmoja akiniambia mpango huo, lakini awali nilikuwa na mpango wa kuja Dar kwa ndege, kuna binamu yangu anafanya kazi Fastjet, alikuwa amenikatia tiketi achana na ya Simba waliotaka kukata.
Nikamwambia kiongozi wa Simba nakuja Dar jumapili, lakini sijui ni saa ngapi kwasababu hiyo tiketi natumiwa kwenye e-mail, akaona kama namdanganya hivi. Akaniambia kwani hiyo tiketi vipi? Sisi tunakukatia nyingine, nikawaambia sasa hiyo nyingine itakuwaje? Akaniambia usijali, akanitumia tiketi nyingine, nikamwambia binamu aachane na kunitumia tiketi.
Yule kiongozi wa Simba akawa ananipigia simu mara kwa mara akisema bwana nimesikia Yanga wanakutumia tiketi uje, nikamwambia mimi sijui. Kila muda ananipigia bwana usirubunike, tunakuomba sana. Nikamwambia mimi nikikwambia kitu nitafanya basi nitafanya, siwezi kurubunika kwasababu ya kitu fulani.
Juzi asubuhi saa 12 kanipigia simu mtu mmoja akiniuliza, vipi uko wapi? Nikamwambia nipo home, akasema uko home wapi wakati uko Airpot hapo (Mbeya)? Nikamwambia naenda Dar kuonana na Mtibwa sio huko unakosema wewe. Kweli nikasafiri na kukutana na wale jamaa wa Simba. Jinsi walivyokaa huwezi kujua kama wanamsubiria fulani, mmoja kakaa huku, mwingine kakaa kule. Kuna broo nilikuwa namjua pale, nikaenda alipo, akanichukua tukaenda mpaka kwenye gari, hatimaye tukaenda ofsini, tukakubaliana mahitaji ya msingi, tukaafikiana kwa pande zote mbili na nikasaini mkataba wa miaka miwili nikiwa na ndugu yangu anayejua sheria.

REAL MADRID YAMFUKUZA KAZI ANCELOTTI BAADA YA KUMALIZA MSIMU BILA TAJI

KLABU ya Real Madrid imemfukuza kocha Carlo Ancelotti mwaka mmoja na siku moja tangu aipe timu hiyo taji la 10 la Ulaya.
Rais wa klabu, Florentino Perez amethibitisha katika Mkutano na Waandishi wa Habari usiku wa Jumatatu juu ya uamuzi wa kumtimua kocha huyo wa tisa katika miaka yake 12 ya kuwa madarakani, Lakini akazuiwa kwa muda kumtaja Rafa Benitez kuwa kocha mpya.
Kocha huyo wa zamani wa Liverpool anabaki kuwa mwenye nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Ancelotti ambaye kufukuzwa kwake hakujawafurahisha wahezaji na mashabiki.
Carlo Ancelotti has been sacked by Real Madrid after overseeing a trophyless season at the Bernabeu
Carlo Ancelotti amefukuzwa Real Madrid baada ya kumaliza msimu bila taji
Real Madrid president Florentino Perez announced on Monday evening that Ancelotti had been sacked

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ametangaza kumfukuza Ancelotti 

MAKOCHA TISA ALIOFUKUZA FLORENTINO PEREZ NDANI YA MIAKA 12 

Vicente del Bosque (Juni 23, 2003)
Carlos Queiroz (Mei 24, 2004)
Jose Antonio Camacho (Septemba 20, 2004)
Marino Garia Remon (Desemba 30, 2004)
Vanderlei Luxemburgo (Desemba 4, 2005)
Fabio Capello (Juni 28, 2007)
Bernd Schuster (Desemba 9, 2008)
Manuel Pellegrini (Mei 26, 2010)
Carlo Ancelotti (Mei 25, 2014)

May 25, 2015

HUU NDIO UAMUZI WA MAN U KWA FALCAO

 
Frank Lampard, Didier Drogba, Steven Gerrard na Brad Fiedal leo watacheza mechi zao za mwisho katika ligi kuu ya England baada ya miaka zaidi ya 10 kwa kila mmoja wao.
Hata hivyo macho na masikio ya wapenzi wengi wa soka yapo katika kuangalia hatma ya mshambuliaji wa kicolombia Radamek Falcao ndani ya klabu ya Manchester United.

Falcao ambaye alijiunga na United kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Monaco, ameambiwa rasmi na United kwamba klabu hiyo haitoweza kumuongezea muda ndani ya klabu hiyo, hii ni kwa mujibu wa mhariri mkuu wa Dailymail – Ian Ladyman.
Falcao ambaye ameshindwa kung’ara na Man United na hivyo kutumia muda mwingi benchi, ameifungia timu hiyo magoli 4 na kutoa pasi za magoli 4.

Kwa mujibu Ladyman, Falcao alikuwa na mazungumzo na kocha Louis Van Gaal kuhusu hatma yake na hata alikubali kupunguza matakwa ya mshahara ili aendelee kubaki Old Trafford lakini haikuwezekana.

Mchezaji huyo anategemewa kucheza mechi yake ya mwisho leo dhidi ya Hull City katika siku ya mwisho ya Barclays Premier League na baada ya hapo atasafiri kwenda kwao kujiunga na Colombia kwa ajili ya michuano ya Copa America.

TFF YATOA MAAMUZI JUU YA MART NOOIJ


KOCHA-TAIFASTARS
Kamati ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya  Cosafa.
Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.
Baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.
Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.
Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.
Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 – 2012.

KUHUSU CHANONGO KUMALIZANA NA YANGA MENEJA WAKE ANEA

943612_heroa
STORI ya winga Haruna Chanongo kusajiliwa na Yanga imegonga vichwa vya habari nchini, lakini taarifa mpya kutoka kwa Meneja wake, Jamal Kasongo ni kwamba bado nyota huyo hajamwaga wino Jangwani.
Msimu uliopita wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika mei 9 mwaka huu, Chonongo alikuwa anaichezea Stand United ya Shinyanga.
“Ni vyombo vya habari, hatujakaa na viongozi wa Yanga zaidi ya kunipigia simu tu!. Amefananua Kasongo na kuongeza: “Tumezungumza na kufika mahala ambapo tumewaacha wajifikirie (Yanga) na sisi tufikirie, lakini bado hajasaini”.
“Sijakaa mezani kuzungumza nao, nilipigiwa simu tu na kiongozi mmoja wa Yanga na muda si mrefu nimewaambia kwamba tunapaswa kukaa mezani”.
Kwanini Kasongo ambaye pia ni wakala wa Mbwana Samatta wa TP Mazembe, anaweka ngumu kumruhusu Chanongo kusaini Yanga?

“Kubwa zaidi kwangu ni mkataba, kuna vipengele ambavyo nataka lazima viwepo, unajua  tunachotazama ni hatima ya mtoto (Chanongo) kwenda mbele zaidi, nadhani kama Chanongo atakaa zaidi ya mwaka mmoja Yanga atakuwa wa hapa hapa, nina ofa nyingi za nje, kwahiyo nataka kujua kama Chanongo atasaini Yanga hatima yake itakuwaje?’ Amesema Kasongo.

HUYU NDIYE ATAKAE ZIBA PEGO LA NGASSA YANGA



Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
YANGA SC imewapiga bao wapinzani, Simba SC na Azam FC katika vita ya kuwania saini ya kiungo hodari wa pembeni, Deus Kaseke.
Kaseke amesaini Mkataba wa miaka miwili na Yanga SC asubuhi ya leo, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam mbele ya Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji.
Kaseke anatua Yanga SC kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Mbeya City, aliyoichezea kwa miaka mine iliyopita.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya kusaini Mkataba huo, Kaseke amesema; “Nimefurahi kutua Yanga SC, ni timu ambayo kwa kweli nilikuwa nina ndoto za kuichezea kwa muda mrefu,”. 
Deus Kaseke katikati akisaini Yanga SC leo, kulia ni mjomba wake, Bahati Kaseke na kushoto Katibu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha
Kaseke amesema anafahamu changamoto inayomkabili baada ya kusaini Yanga SC, ushindani wa nafasi dhidi ya wachezaji wengine bora waliopo kwa mabingwa hao wa Tanzania.
“Yanga SC ni timu kubwa, ina wachezaji bora na ndiyo maana ni mabingwa. Baada ya kusajili, sasa natakiwa kufanya mazoezi kwa bidii ili niwe katika kiwango bora zaidi na kuwashawishi makocha wanipe nafasi,”amesema.
Kaseke amesema lengo lake ni kufika mbali zaidi kisoka na anataka aitumie Yanga SC kama ngazi ya kupanda kwenda nje kucheza soka ya kulipwa.
Yanga SC wanamsajili Kaseke baada ya kumpoteza kiungo wake bora wa pembeni, aliyekuwa anaweza kucheza pia kama kiungo wa kati na mshambuliaji, Mrisho Ngassa aliyesaini Free State Stars ya Afrika Kusini.
Kaseke pia ana sifa kama Ngassa, mbali na kuteleza pembeni kwa kasi, pia anaweza kucheza kama kiungo wa kati na mshambuliaji.
Ilikuwa vita usiku wa kuamkia leo, viongozi wa Simba na Yanga wakifukuzana kumsaka Kaseke hadi hatimaye wana Jangwani kufanikiwa kumnasa na wamemalizana naye. 
Azam wenyewe walikuwa wanamfuatilia kimya kimya mchezaji huyo- na hawakuwa na spidi ambayo walikuwa nayo Simba SC- maana yake hili ni pigo zaidi kwa wana Msimbazi.  
Deus Kaseke sasa anapatikana Jangwani, Dar es Salaam

PETER MWALYANZI ASAINI SIMBA MIAKA MIWILI



Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES ALAAM
WAKATI Yanga SC wakisherehekea saini ya winga Deus Kaseke, Simba SC nao wamefanya yao mchana huu.
Kiungo hodari mchezeshaji Peter Mwalyanzi kutoka timu ile ile, Mbeya City aliyotokea Kaseke amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.
Mwalyanzi moja ya viungo waliong’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Barav msimu huu ambaye alikuwa anamchezesha vizuri Kaseke, amesaini ofisini kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe, Mbezi, Dar es Salaam.
Na Poppe aliyekuwa na Mjumbe wa Kamati ya Uteneaji, Collins Frisch akasema; “Sisi tunajua wachezaji bora na Simba SC ndiyo nyumbani kwa wachezaji bora,”.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch akimshuhudia Peter Mwalyanzi wakati anasaini ofisini kwa Hans Poppe leo

Poppe amesema kwamba Mwalyanzi ni pendekezo la kocha Mserbia, Goran Kopunovic lakini hata washauri wengine wa masuala ya kitaalamu wameridhishwa na uwezo wa mchezaji huyo.
Kwa upande wake, Mwalyanzi ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba anajisikia furaha kusaini timu hiyo kubwa, kwani ni hatua moja kubwa mbele katika maisha yake ya soka.
“Mchezaji yeyote anapokuwa anaibuka katika nchi hii, ndoto zake ni siku moja kucheza timu kubwa kama hizi, na mimi nimefurahi sana kujiunga na Simba SC,”amesema.
Mwalyanzi ameongeza kwamba baada ya kusaini, anaomba ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzake, viongozi na mashabiki ili aweze kufanya vizuri.  
Zacharia Hans Poppe akimshuhudia Peter Mwalyanzi wakati anasaini leo Mbezi

Mapema leo, Yanga SC imemsainisha Mkataba wa miaka miwili kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam mbele ya Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji.
Kaseke anatua Yanga SC kama mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake Mbeya City, aliyoichezea kwa miaka mine iliyopita.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya kusaini Mkataba huo, Kaseke amesema; “Nimefurahi kutua Yanga SC, ni timu ambayo kwa kweli nilikuwa nina ndoto za kuichezea kwa muda mrefu,”.
Kaseke amesema anafahamu changamoto inayomkabili baada ya kusaini Yanga SC, ushindani wa nafasi dhidi ya wachezaji wengine bora waliopo kwa mabingwa hao wa Tanzania.
“Yanga SC ni timu kubwa, ina wachezaji bora na ndiyo maana ni mabingwa. Baada ya kusajili, sasa natakiwa kufanya mazoezi kwa bidii ili niwe katika kiwango bora zaidi na kuwashawishi makocha wanipe nafasi,”amesema.

May 24, 2015

HII NI REKODI NYINGINE ALIYOIVUNJA RONALDO BAADA YA MCHEZO WA LEO

Mshambuliaji hatari wa Real Madrid ameivunja rekodi aliyoiweka mwenyewe ya misimu 3 iliopita baada ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania na kufikisha magoli 61 kwa michuano yote ya msimu huu,amefikisha idadi hiyo baada ya kufunga Hat-trick mapema leo baada ya mchezo wao dhidi ya Getafe.
Matumaini ya kuifukuzia Barcelona katika mbio za ubingwa wa la liga yalifutwa wiki iliyopita lakini hiyo haikuwazui vijana wa Carlo Ancelotti kwa kuanza kwa stlye yaka mchezo wa leo baada ya krosi safi kutoka kwa Marcelo na Ronaldo kijitwisha kichwa safi na kufunga goli la kwanza dakika ya 13 na kuufanya ubao usomeke 1-0.
WAgeni walicharuka na walifunga magoli mawili ya haraka haraka na kuwafanya waongoze hata hivyo Hiyo haikutosha kwa wageni hao baada ya Ronaldo kiungia nyavuni kwa mpira wa adhabu ndogo na kufanya usawa wa magoli na kua 2-2 na kufanya Ronaldo kufikisha magoli 60 na kuifikia rekodi yake ya misimu wa 2011-12.
Lakini rekodi yake hiyo aliivunja dakika mbili baadae baada ya kupata mkwaju wa penati na kufunga na kufanya waongoze kwa goli 3-2 pale Santiago Bernabeu nakua goli lake la 313 katika mechi 300 alizocheza hadi sasa.
Hat-trick ya Ronaldo inamfanya kufikisha goli 48 za ligi msimu huu,hiyo inamfanya kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania na ulaya nzima kwa ujumla na kumfanya kuchukuia tuzo ya Pichichi,pia amebakisha magoli 10 kumfikia Raul na kuwa mfungaji wa muda wote wa Real Madrid.

NGASSA PUSHAPU 200 KILA SIKU, MAANDALIZI YA PSL SI MCHEZO

Mshambuliaji wa Free State Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Mrisho Khalfan Ngassa hupiga pushapu 200 kila siku asubuhi kabla ya kuingia kwenye programu nyingine za mazoezi kama kukimbia na kucheza na mpira. 
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC kwa sasa yupo mapumzikoni akijiandaa na msimu mpya katika klabu mpya, Free State Stars

Ngassa alikuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki michuano ya Kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini na kufanya vibaya, baada ya kufungwa mechi zote tatu za Kundi B

May 23, 2015

MECKY MEXIME ATAJA KIKOSI CHAKE BORA VPL2014/2015

mtibwa-picha
TUNAENDELEA  kuangalia vikosi bora vya makocha wa timu za ligi kuu soka Tanzania bara, makocha wasiokuwa na timu na wachambuzi wa soka kwa msimu wa 2014/2015.
Jana tulikuwekea kikosi bora kilichopendekezwa na kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi na tukaahidi kukupatia kikosi bora cha kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime….
Hiki ndicho kikosi bora cha ligi kuu soka Tanzania bara msimu 2014/2015, kwa mujibu wa Mexime;
  1. Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
  2. Hassan Ramadhan Kessy (Simba)
  3. David Charles Luhende (Mtibwa Sugar)
  4. Salim Mbonde (Mtibwa Sugar)
  5. Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ (Yanga)
  6. Mudathir Yahya (Azam fc)
  7. Simon Msuva (Yanga)
  8. Haruna Niyonzima (Yanga)
  9. Amissi Tambwe (Yanga)
  10. Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
  11. Emmanuel Okwi (Simba)

NDANDA FC KUMUIBUKIA ALIKO DANGOTE

Aliko Dangote, President and CEO of Nigeria's Dangote Group speaks during the final session of the World Economic Forum
Bilionea Aliko Dangote
Uongozi wa Ndanda FC unajipanga kukutana na bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kwa ajili ya kumuomba kuwa mmoja wa wadhamini wa juu katika timu hiyo kabla msimu ujao haujaanza.
Salehjembe ameripoti kwamba  mwenyekiti wa Ndanda FC, Hamad Omari alisema licha ya kuwa na udhamini wa Kampuni ya Binslum na Big Tanzania, lakini wanajipanga kumuona tajiri huyo anayemiliki kiwanda cha saruji kwenye mkoa wao.
“Tunafikiria kufanya mikakati ya kuweza kukutana naye ili aweze kuwa mdhamini mkuu kwenye timu yetu ambayo imenusurika kushuka daraja.
“Unajua tangu ligi imemalizika bado hatujakaa kuweza kujadili hayo mambo na kama ataweza kukubali basi litakuwa ni jambo jema kwa sababu fedha zinazotolewa na wadhamini wa ligi hazikidhi mahitaji ya timu kwa msimu wote, sasa lazima njia nyingine zitumike kuhakikisha tunakuwa vizuri zaidi msimu ujao,” alisema Omari.

Dangote, raia wa Nigeria, kwa sasa ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara ambako timu hiyo inatokea, anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4 (shilingi trilioni 2.7) na hivi karibuni alitangaza nia ya kuinunua Klabu ya Arsenal ya England.

MWAMBUSI AICHOMOLEA NJE AZAM FC


 IMG_5671
WAKATI Azam fc wakidai idadi ya wachezaji wa kigeni ligi kuu soka Tanzania bara iongezwe kutoka idadi ya sasa ya watano, kocha wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi amepinga mtazamo huo.
Hoja ya Azam kutaka idadi iongezeke ni kupata wachezaji wengi wa kigeni watakaowasaidia katika michuano ya kimataifa pamoja na kuwapa changamoto wachezaji wazawa ndani ya timu hiyo.
Makamu bingwa hao wa ligi kuu msimu wa 2014/2015 wanadai wamejifunza kwa TP Mazembe na El Merreikh ambao wamesheheni wanasoka wengi kutoka nje ya nchi zao.
Azam wakitoa hoja hizo, Mwambusi amesema haoni haja ya kuongeza wachezaji wa kigeni bali vipaji vya ndani viangaliwe zaidi.
“Siungi mkono kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni katika soka letu la Tanzania kwasababu sisi tuna wachezaji wengi wenye vipaji. Muhimu ni wachezaji wetu kujitambua kwanza, halafu viongozi wa klabu zetu wanawachukuliaje wachezaji wetu?” Amesema Mwambusi na koungeza: “Saa nyingine watu wanataka kusajili kwa fasheni, vilabu vikubwa vinashindana kusajili wachezaji wa nje, tusichukue wachezaji kwasababu tu tunataka kushindana na fulani, tuwachukue wachezaji wa nje kwasababu wana kiwango cha juu ili waje kuleta changamoto hapa kwetu”.
“Kwa idadi iliyopo inatosha kwasababu tumeshaona hata hao watano kuna wengine wanakaa nje kwa kushindwa na wazawa. Mimi nasema wachezaji wetu wanatakiwa kujitambua tu ili wajue kuwa mpira ni kazi, wajitoe na kucheza kwa juhudi zote uwanjani ili kuweza kuendeleza soka letu”.
“Wanaweza kuja hata wachezaji 11 wa kigeni, sijui kama itatusaidia, kikubwa tuangalie tulipojikwaa, tusiangalie tulipoangukia. Viongozi wanaweza kusema vijana wetu hawajitambui, sawa!, watajitambuaje? Kila mtu kwa nafasi yake katika mpira afanye kazi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na kwa umakini mkubwa, viongozi wanaotawala soka katika nchi yetu wana nia kweli ya kuendeleza soka letu?. Tunaweza tukakubali kuleta wachezaji wengi, lakini tusipopita kwenye mfumo sahihi hatuwezi kufika kokote”.

May 22, 2015

JULIO ATAJA KIKOSI CHAKE BORA CHA VPL 2014/2015

BAADA ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 kumalizika mei 9 mwaka huu na Yanga wakiibuka mabingwa, mtandao huu unaendelea na zoezi la kukuketea vikosi bora vilivyochaguliwa na makocha wa timu za ligi kuu na wasiokuwa na timu pamoja na wachambuzi wa soka nchini.
Jana kocha mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm alitaja kikosi chake bora na tukaahidi kukuletea kikosi bora cha VPL 2014/2015 cha kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Katika mahojiano na mtandao huu Julio amesema kikosi chake bora kutokana na mechi za ligi kuu alizoziona ni:
1. Ally Mustafa ‘Bartez’ (Yanga)
          2. Shomari Salum Kapombe (Azam fc)
3.  Paul Ngalema (Ndanda fc)
 4.   Juma Nyosso (Mbeya City)
   5.     Paschal Wawa (Azam fc)
6.    Jonas Mkude (Simba)
7.     Simon Msuva Yanga)
8.    Salum Telela (Yanga)
     9.       Amissi Tambwe (Yanga)
10.   Ibrahim Ajib (Simba)
     11.   Malim Busungu (Mgambo )

IVO MAPUNDA ATIMKIA OMAN, MIPANGO YA MUSLEY HIYO


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MAKIPA wote wa Simba SC, wakiongozwa na ‘mkubwa wao’ Ivo Mapunda watakwenda mafunzoni nchini Oman.
Ivo pamoja na kipa wa pili, Hussein Sharrif ‘Casillas’ na makipa wa timu ya vijana wanaokomazwa kikosi cha kwanza, Peter Manyika na Dennis Richard wanatarajiwa kuondoka wakati wowote kwenda Oman.
BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba mipango ya makipa hao kwenda mafunzoni, imefanywa na mmoja wa wafadhili wa timu hiyo, Musley Al Ruweh.
Ivo Mapunda anatarajiwa kuwaongoza makipa wenzake wote Simba kwenda Oman kwa mafunzo maalum

Musley ambaye pia amegharamia safari ya kwenda Oman kwa kocha wa makipa Meja na kocha Msaidizi, Suleiman Matola hakupatikana alipotafutwa kuzungumzia safari hiyo, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu ni wakati wowote kuanzia sasa.
Makipa hao wanatarajiwa kwenda kunufaika na mafunzo ya kocha wa makipa aliyebobea, Haroon Amur Al Siyabi ambaye mara kadhaa huja nchini kuwanoa makipa wa Simba SC.
Matola yeye ambaye kwa sasa anaendelea na mafunzo ya ukocha Dar es Salaam, anatarajiwa kwenda kupatiwa programu maalum ya kujiendeleza zaidi kielimu nchini humo.
Musley kulia ndiye amefanikisha safari ya makipa wa Simba SC mafunzoni Oman

JOHN BOCCO AFICHUA SIRI YA TAIFA STARS KUBORONGA,


"Nikiwa kama mchezaji waki TANZANIA ninaecheza ligi ya hapa nyumbani na nikiwa mmoja wa wachezaji katika Timu ya Taifa ya kizazi hiki cha sasa wa Mudamrefu. Naandika hivi nikiwa na huzuni na masikitiko makubwa juu ya mpira wetu wa TANZANIA kwa ujumla kuanzia club zetu, ligi yetu na mpaka kwenye Timu ya TAIFA 'TAIFA STARS'.
Sijaandika ivi kwania ya kufundisha wala kukosoa MSHABIKI, KIONGOZI WA MPIRA, VILABU VYA TANZANIA, SHIRIKISHO LA MPIRA WA TANZANIA na wala TIMU YETU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU. Toka nilipopata akili ya kuutambua mpira wa TANZANIA kwa kuusikiliza kwenye redio na pia kuona bahazi ya mechi kwenye Tv za vilabu pamoja na Timu ya TAIFA nilikuta ukiwa na lawama upande wa Wachezaji pamoja na Uongozi wa uendeshaji wa mpira wa VILABU pamoja na TIMU YA TAIFA mpaka nilisikia timu yetu ya TAIFA IKIITWA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU. Mimi nikiwa kama Mtanzania pia nikiwa miongoni mwafamilia ya mpira wa tanzania pia inaniuma sana nikiiona mioyo ya watanzania wa penda soka mamilioni ikiteseka kutopata furaha ya mpira. 
Wewe kama mtanzania mpenda soka, Unahisi furaha inakoseshwa na Wachezaji wa kitanzania, Uongozi na uendeshaji mpira wa kitanzani, Mashabiki wa kitanzania au TATIZO NI NINI?????????
Kwafikra zangu mimi nahisi mpira wa tanzania unaasiriwa 1. Kutokuwa na program za kuendesha mpira kisasa 2. Kutokuwa na misingi endelevu ya kuendesha wachezaji wa dogo kisasa 3.kutokua na ligi kuu bora nchini 4.Kuwa na huaba wa wachezaji wachache wanachezesha njee ya nchi ndani ya Timu ya TAIFA 5.Kutothamini na kueshimu wachezaji wakitanzania walio ndani ya ligi yetu na njee ya ligi yetu etc.
1. PROGRAM ZA KISASA ZA KUENDESHA MPIRA WETU. Tanzania tupo nyuma sana yani tunaongoza mpira kizamani sana kwa upeo wangu mimi wa sasa mpira hauchezwi na kipaji tu Bali pamoja na elimu ya mpira Ndio manawenzetu wanakuwa na shule za mpira, mfano' sisi watanzania tunaleta makocha wa kisasa kwenye club zetu pamoja na timu yetu ya taifa, ila mnasahau kuwa wachezaji wenu hawajaandaliwa kisasa pia hata makocha wanaowafundisha sio wa kisasa. Tunatakiwa sasa tuamke kuwapeleka makocha wetu wakajue mpira wakisasa unavofundishwa ili waje kuwafundisha wachezaji mpira huo ili hata tukileta makocha wakigeni ambao ni wakisasa wawe wanatuongezea kipya sio kuanza tena moja. Pia na shirikisho la mpira liongoze mpira kisasa hata kwakuiga basi nchi zilizoendelea zaidi yetu kimiprira kuwa walianzaje na wamewezaje sio kwa mifumo yetu hii yakizamani na mawazo yetu ya mtu mmoja mmoja.
KUTOKUWA NA MISINGI ENDELEVU YA KUENDESHA WACHEZAJI WA DOGO KISASA. Tanzania tunauhaba wa vituo vya kuendesha soka na kutengeneza vipaji vya vijana wadogo pia tuna utamaduni ambao sio wakisasa wa kuinua na kutengeneza vipaji hapa nchini, sisi watanzania club na shirikisho letu huwa wanainua vipaji sio kutengeneza vipaji kama kwa nchi za wenzetu. Kutengeneza kipaji ni nini ?? Kutengeneza kipaji katika soka nikumchukua Mtoto asiejua hata maana ya kupiga pasi, krosi shuti na kuanza kumfundisha moja baada ya moja mpaka kufikia kugeuka na mpira na kupiga chenga. Kuinua kipaji ni nini?? Kuinua kipaji nikumkuta Mtoto wa umri wamiaka 15,16 mpaka 17 na kuendelea akiwa anajua nn maana ya kupiga pasi,krosi,kugeuka na mpira na mpaka kupiga chenga, kwamaana hiyo sasa ukifatilia club zetu hata shirikisho letu la mpira hawana malengo na watoto wenye umri wa miaka 8,9,10,11,12,13,14 na 15 kuwaandaa ambao hawa unaweza kuwapa msingi wowote wa soka unaoutaka Bali tunaanza na watoto wa umri wa miaka 17,18,19 na 20 na kuendelea ambao washapitia kwenye misingi ya kizamani ambayo yamitaani ya kupiga pasi,krosi na chenga, ambao umri huo nchi za wenzetu zilizo endelea umri huo wa miaka 17.....20 unawakuta wakiwa tayari na wekicheza Timu kubwa pamoja na timu ya taifa kwa mafanikio sio kwakupata uzoefu. Tuamke watanzania pamoja na shirikisho letu na vilabu vyetu tusitake mafanikio ya haraka ambayo yanazidi kutupotezea muda kumchukua mchezaji wa umri wa miaka 17 nakuendelea aliepitia misingi mibovu ya mpira ndio ukataka umbadilishe na kocha wa kisasa wakigeni wa u17 wa timu ya taifa bali tuchukue Mtoto wa miaka 8..mpaka..12 tumpe kocha wa kisasa, madocta wakisasa, elimu ya kisasa na malezi ya soka la kisasa alfu tuone kama hatutoweza shiriki kombe la Africa.
3. KUTOKUWA NA LIGIKUU BORA NCHINI. kuwa na ligikuu bora chini nikioo kwa kuinua mpira wa nchi yetu, kwa mfano kama kwa sisi tanzania naweza kusema asilimia 90% ya wachezaji wa Timu ya taifa wanatoka katika ligi yetu ya nyumbani lakini kiukweli ligi yetu haina ubora kuanzia kwa maandalizi ya wachezaji toka walipoanzia soka (mafunzo ya soka waliyoyapata) pili uendeshaji wa club zetu hapa nchini miundombinu inayotumiwa kuendesha ligi yetu hapa nchini mfano viwanja tunavotumia vibovu, mipira tunayotumia mibovyu kwenye ligi jezi mbovu waamuzi sio wazuri ni waamuzi wanachezesha kizamani, kwasababu tukija kucheza mechi zakimataifa tunakutana na mipira mizuri viwanja vizuri waamuzi wazuri wakisasa na ndio mana timu za tanzania kwenye mashinda ya kimataifa tunapata kadi nyingi ofsaidi nyingi mwisho tunafungwa kumbe tatizo tulizoeshwa vibaya na marefa wa ligi yetu. Kwamaana iyo basi huwezi kumpata mchezaji wa Timu ya taifa mzuri kutoka kwenyeligi yetu mbovu isiyo na viwanja bora mipira bora uongozi bora marefa bora wala mashabiki bora, hiyo nichangamoto kwetu watanzania wote wapenda soka tushtuke na tubadilike ili mpira wetu uinuke bilaivo mtalaumu wachezaji tu mpaka Somalia watashiriki world cup sisi hata Afican cup hatutagusa.
Waandishi wa habari na mashabiki wa MPIRA WA TANZANIA muamke na mbadilike kunavitu muhimu sana vya kusema ili soka la tanzania libadilike kunavitu Vingi sana vya kusema ili vibadilishwe ili tanzania tusiwe tena vipofu kwenye ulimwengu huu wa soka la kisasa sio soka la mdomoni wala magazetini sio soka lakupanga Timu ya TAIFA kwenye gazeti au kwenye vijiwe jioni tukikaa ila imefikia wakati wa kupanga timu au kuchagua timu kwa mtu husika sio kwamawazo ya mtu mmoja mmoja, kwakufanya mabadiliko ya kuwa na ligi bora ili tupate wachezaji bora kwa ubora wao utatengeneza Timu ya taifa bora na tutapata wachezaji wengi watakao fikia kiwango chakucheza mpaka njee ya nchi ambao tukifikia hatua hiyo tutakua na Timu ya TAIFA bora zaidi kwa badae ambayo tukija kupangwa tena na NIGERIA miaka ya badae tutakua na uwakika wakuwafunga ila kwa hivi tunavoenda hatatukiwafunga tumewabahatisha tu kiukweli TANZANIA tulipo sasa na soka la ulimwenguhuu lilivofikia bado sana. Tubadilikeni watanzania hii niaibu si kwa wachezaji tu ila ni kwanchi nzima mtawalaumu wachezaji tu ila wachezaji sio tatizo tatizo tunamifumo ya kizamani alafu bado tunailazimisha iendelee. TULISHAFELI..TUMEFELI..NA TUSIPOAMKA TUTAFELI KABISA yani tutakua wa mwisho KABISA duniani. Ebu jiulize wewe mwenyewe uliviona vizazi vingapi tanzania vilivyopita na vilikua na wachezaji wazuri????? Ukipata jibu jiulize tena vilietea mafanikio gani kwenye timu ya taifa au vilabu vyetu ambayo tunajivunia sasa???? Kwa mimi toka nivisikie na kuadisiwa mpaka leo nacheza sijao mafanikio zaidi ya kuwa na sifa zisizofaidisha nchi. Tubadilikeni jamani hayo nimawazo yangu tu kama nimewakosea nisameeni ila hata sisi wachezaji mnaotutukana mais kutuona sio wazalendo inatuumapia kwasababu tunatumia nguvu zetu bilamafanikio nakinachouma zaidi hatupendi kufeli ila tunafelishwa inauma kwa kweli ila nyumbani ni nyumbani TUNAIPENDA NCHI YETU NA TUTAIPENDA MILELE ila tusikubali kupelekwa tubadilikeni watanzania,".

(Makala haya yameandikwa na Nahodha wa timu ya taifa, Taifa Stars katika Kombe la COSAFA, John Bocco)