SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

May 15, 2015

WAYNE ROONEY NJE MAN UNITED NA ARSENAL JUMAPILI, VAN PERSIE KUANZA NA DI MARIA


MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ataikosa mechi ya timu yake, Manchester United dhidi ya Arsenal Jumapili kutokana na kutopona mguu.
Nahodha huyo wa United, alilazimika kutoka nje Jumamosi iliyopita timu yake ikishinda dhidi ya Crystal Palace, na ameshindwa kupata ahueni kuelekea mechi na Washika Bunduki.
Mchezaji mwingine aliyetoka nje pia siku hiyo ni Luke Shaw baada ya kuumia Uwanja wa Selhurst Park na kocha Louis Van Gaal amethibitisha wawili hao wote wanaweza kukosa mechi zote mbili za kumalizia msimu.
Wayne Rooney has been ruled out of Manchester United's clash with Arsenal with a dead leg
Wayne Rooney ataukosa mchezo wa Manchester United dhidi ya Arsenal Jumapili kutokana na maumivu ya mguu

"Hali si nzuri kwetu, hawawezi kucheza, wote kati yao,"amesema kocha huyo Mholanzi, akizungumza na MUTV"Ndiyo, ni kitu cha muda mfupi, tutabakiza mechi moja, hivyo nafikiri ni vigumu kwao kucheza tena msimu huu,"
Nafasi ya Rooney ilichukuliwa na Radamel Falcao baada ya mapumziko wiki iliyopita, lakini Robin van Persie anaweza kuziba pengo lake dhidi ya klabu yake ya zamani, Arsenal baada ya kuthibitika yuko fiti.
Mholanzi huyo ambaye alikosa mechi dhidi ya Palace kutokana na virusi, lakini ataanza pamoja na Angel di Maria - ambaye pia anarejea baada ya kupona majeruhi yake.

MSHITUKO MAN UNITED, DE GEA AMALIZANA KILA KITU NA REAL MADRID AKARITHI GLAVU ZA CASILLAS

KIPA wa Manchester United, David de Gea yuko mbioni kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu, baada ya kufikia makubaliano ya vipengele binafsi vya Mkataba na Real Madrid, kwa mujibu wa taarifa nchini Hispania. 
Gazeti la Marca limeripoti kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 amefikia makubaliano na vigogo hao wa La Liga katika dili ambalo ameahidiwa mshahara wa Pauni Milioni 4 kwa mwaka, baada ya makato ya kodi, ambalo linaaminika litakuwa la miaka mitano au sita.
Gazeti hilo la Madrid pia limesema kwamba kitu pekee kinachokosekana katika dili hilo ni makubaliano baina ya United na Madrid juu ya ada ya uhamisho ya mchezaji huyo. Inaweza kuwa Pauni Milioni 30.
Manchester United goalkeeper David de Gea looks set for a summer move to Real Madrid
Kipa wa Manchester United, David de Gea anatarajiwa kuhamia Real Madrid msimu ujao

De Gea akiondoka litakuwa pigo kubwa kwa kikosi cha Louis van Gaal, baada ya kuwa na msimu mwingine mzuri Manchester ambao imeshuhidiwa kipa huyo wa Hispania akiteuliwa katika kikosi bora cha mwaka 2014-2015 cha PFA 
Kipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid, anatakiwa kwa udi na uvumnba Madrid akazibe pengo la mkongwe Iker Casillas aliyepoteza ubora wake Bernabeu.
Mzuia michomo huyo alionekana Uwanja wa ndege wa Liverpool akisafiri kwenda Madrid Jumatatu kabla ya kurejea mazoezini Jumatano kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya mahasimu, Arsenal.

MANJI AAMBIWA; “UMEMALIZA MUDA WAKO YANGA SC”, KAMATI YAITISHA UCHAGZUI JULAI 12 DAR

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM 
UCHAGUZI Mkuu wa Yanga SC utafanyika Julai 12, mwaka huu katika ukumbi ambao utatajwa baadaye.
Taarifa ya Katibu Kamati ya Uchaguzi ya Yanga SC, Francis Kaswahili iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo imesema kwamba, fomu za wagombea zitaanza kutolewa Mei 17, mwaka huu kwa kuzingatia ratiba.
“Jambo hili ni la kikatiba na wala halina mjadala, tunataka Yanga iwe na viongozi ambao watatokana na utashi wa Wanayanga ni matumaini ya kamati ya uchaguzi kwamba hapatatoka mtu mwingine wa kutaka kuvunja misingi ya katiba.
Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji ameambiwa amemaliza muda wake madarakani

“Huu ni utamaduni wa mwanadamu anayeishi katika mfumo wa demokrasia na hasa ikizingatiwa kwamba mwaka 2015 ni mwaka pia wa uchaguzi, wa Rais , Wabunge na Madiwani,”amesema Kaswahili. 
Ameongeza kwamba, lengo ni mwendelezo wa kupokezana vijiti na kwamba kiongozi bora atapatikana kwa misingi bora ya kikatiba na si vinginevyo.
Itakumbukwa kwamba kwa mara ya mwisho Yanga SC ilifanya uchaguzi wake Julai 18, mwaka 2010 na Wakili Lloyd Biharangu Nchunga alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu wake, Devis Mosha na Wajumbe; Charles Mgondo, Ally Mayayi Tembele, Mzee Yussuf, Theonest Rutashobolwa (marehemu), Titus Ossoro, Sara Ramadhani, Mohamed Bhinda na Salum rupia. 
Hata hivyo, kwa vipindi tofauti baadhi ya viongozi walijiuzulu nyadhifa zao na hivyo ikalazimika kufanyika uchaguzi mdogo ufanyike Julai 15, mwaka 2012 na Yussuf Manji alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Makamu wake Clement Sanga na Wajumbe; Aaron Nyanda, George Manyama, Abdallah Bin Kleb na Mussa Kutabaro. 
“Na itakumbukwa kamba wale wote ambao waliingia kwa kuziba nafasi wzi walikuwa wanatumikia mhula ulioanza tarehe 18/07/2010 na ulikoma tarehe 17/07/2014 na hivyo viongozi wote nafasi zao kwa sasa zipo wazi,”amesema Kaswahili.

SIMBA SC YATUPA NDOANA ZAKE KWA BEKI TEGEMEO RWANDA, TENA KINDA TU

Na Princess Asia, DAR ES SAALAM
SIMBA SC imetupa ndoana zake kwa Emery Bayisenge wa APR ya Rwanda, lakini kumpata kazi ipo.
Bayisenge, beki hodari wa kati mwenye umri wa miaka 21 tu, ni tegemeo la Rwanda kuelekea michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika CHAN mwakani, inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Kwa sababu hiyo, Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) halitapenda kukipoteza kisiki hicho kabla ya CHAN ya mwakani, ambayo wao watakuwa wenyeji. 
Simba SC inamtaka Emery Bayisenge, lakini kikwazo ni FERWAFA inayotaka kumtumia katika CHAN mwakani

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ni shabiki mkubwa wa beki huyo na BIN ZUBEIRY inafahamu yuko katika jitihada kubwa za kuhakikisha anamhamishia Msimbazi.
Bayisenge mwenyewe kwa mvuto wa maslahi na hamu yake kubwa ya kucheza Tanzania, yuko tayati kutua Simba SC- lakini FERWAFA ndiyo kikwazo. 
Bayisenge ambaye kabla ya APR alichezea Amagaju na Isonga, amekuwa akiichezea Amavubi tangu mwaka 2011.
CHAN ijayo inatarajiwa kufanyika Rwanda kuanzia Januari 16 hadi Februari 7 ikishirikisha jumla ya timu 16.