SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 2, 2015

DR SLAA AIFAGILIA AZAM FC

DSC_0242_thumb[2]
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilbroad Slaa, amezitolea uvivu klabu za Simba na Yanga kusema hazina jipya.
Slaa alitoa kauli hiyo juzi Jumapili kwenye mkutano wa kumpongeza mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kibwegere, Edson Nyingi, uliofanyika kwenye viwanja vya Makombe, Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo, Dk. Slaa alisema kwa sababu Simba na Yanga zimeshindwa kufika popote, ni lazima zitafutwe timu mbadala za kuweza kuchukua nafasi zao.
Alisema anasikitishwa na klabu hizo kwani licha ya ukongwe zilionao katika Soka la Tanzania zimeshindwa kuitangaza nchi kimataifa.
“Sina ugomvi na Simba wala Yanga, lakini lazima tukubaliane kuwa zimeshindwa kuitangaza nchi kimataifa na hii ni kutokana na mipango mibovu ya klabu hizi, hivyo ni wakati wa vijana kujipanga kuanzisha timu zenye malengo.
“Angalia Azam, licha ya kwamba ni timu changa iliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni, lakini imeonyesha dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo ya soka kama tunavyoshuhudia tayari wana uwanja wao,” alisema Dk. Slaa.
“Wana vitendea kazi vingi na wapo wanazingatia soka la vijana lakini Simba na Yanga ziko pale pale miaka nenda rudi, ni dhahiri kwa mwenendo huu hawatafika.”

SCHURRLE AIHAMA CHELSEA



kiungo mshambuliaji wa Chelsea Andre Schurrle amejiunga rasmi na klabu ya Wolfburg kwa ada inayokadiliwa kuwa ni paundi millioni 24.
Kiungo huyo alikuwa na kipindi kigumu katika klabu yake ya Chelsea mara baada ya kutopewa nafasi ya kutosha kucheza hasa katika kikosi cha kwanza hali iliyopelekea kuuzwa kwa wakali hao wa bundesliga ambao wako nafasi ya pili kwa sasa.
Ikumbukwe tu Andre Schurrle mwenye umri wa miaka 24 alisajiliwa na klabu ya Chelsea kutoka Bayer leverkusen mwaka 2013.

HII KUHUSU USAJILI WA ANDERSON MAN U






Mchezaji wa Man united Anderson amesafiri kwenda nchini kwao Brazil kujiunga  na timu ya Internacional baada ya mambo kwenda kinyume katika klabu ya Man United.

ATLETICO MADRID WAISTUKIA PSG

Mabingwa wa soka nchini Hispania Atletico Madrid, wanajipanga kuwasilisha malalamiko yao FIFA baada ya kubaini njia za udanganyifu zilizokua zikifanywa na mabingwa wa soka kutoka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain dhidi ya Diego Pablo Simeone.
PSG wanadaiwa kutumia njia za kipuuzi kwa ajili ya kumrubuni meneja wa Atletico Madrid ili aweze kujiunga nao huko jijini Paris nchini Ufaransa kutokana na mwenendo wa meneja wao Laurent Blanc kutokua mzuri.
PSG wanadaiwa kufanya udanganyifu huo kwa mara ya pili sasa na wamekua hawafanikiwi kutokana na Simeone kushikilia msimamo wake wa kutaka kusalia mjini Madrid huku akivujisha siri kwa viongozi wake.
Hata hivyo Atletico Madrid watakua na hoja ya kusikilizwa endapo watabisha hodi huko FIFA kwa kuwashtaki viongozi wa PSG kutokana mkataba wa Simeone uliopo hivi sasa ambao utafikia kikomo mwaka 2017.
Sheria zilizowekwa na FIFA duniani kote zinaikataza klabu yoyote kuzungumza na mchezaji ama kocha akiwa ana mkataba wa muda mrefu zaidi ya kufanya mawasiliano na viongozi wa klabu husika.
PSG wangekua na nguvu ya kuzungumza na meneja huyo menye umri wa miaka 44, endapo mkataba wake ungekua umesaliwa na muda wa miezi sita

AZAM FC KUFUNGA ZIARA DRC KWA KUIVAA DON BOSCO KESHO


10502243_903983952975295_7904939974675269474_n
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Azam FC kesho watafunga ziara yao ya wiki moja DRC kwa kuivaa Don Bosco FC.
Mechi hiyo ni ya mwisho kwa Azam FC katika michuano maalum ya kimataifa iliyoandaliwa na klabu ya TP Mazembe ya DRC wanayoichezea washambuliaji Watanzania Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.
Azam FC walianza kwa kupoteza 1-0 dhidi ya wenyeji TP Mazembe kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia, Zesco FC.
Michuano hiyo ni maalum kwa timu zote kuajiandaa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

FIFA YAMCHUNGUZA DIAFRA SAKHO

 
Mchezaji Diafra Sakho na kilabu ya West Ham zinakabiliwa na uchunguzi kutoka shirikisho la soka duniani FIFA kufuatia hatua ya mchezaji huyo kujiondoa katika kikosi cha Senegal katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

FIFA inasema kuwa imefungua uchunguzi wa kinidhamu kwa kukiukwa kwa sheria.
Sakho 25,alijiondoa akiwa na jeraha la mgongo ,lakini baadaye akaifungia bao West Ham katika mechi yake ya FA dhidi ya Bristol City.
Sheria za FIFA zinasema kuwa mchezaji hawezi kuichezea kilabu yake iwapo anatakikana kuichezea timu yake ya taifa,lakini West Ham imekana kufanya makosa yoyote.

AC MILAN YASAJILI KIFAA KIPYA

 

Ac milan imemsajili  Luca Antonelli kutoka Genoa kwa ada ambayo haijawekwa wazi Antonelli mwenye umri wa miaka 27 amesaini mkataba ambao utaisha mwezi june 2018 na amepewa jezi no 31. Antonelli ambaye amekuwa katika Academ ya milan alishindwa kufanya vizuri na akatolewa kwa mkopo katika klabu ya Bari 2007 - 2008 na baadae akasajiliwa Parma 2008  kabla ya kujiunga na genoa 2011 na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho .

MATRI AMERUDI JUVENTUS


 Juventus sign Matri on loan from AC Milan

Juventus imemsajili Alessandro Matri kwa mkopo kutoka Ac milan hadi mwisho wa msimu. Mshambuliaji huyo amerejea Turin baada ya Sebastian Giovinco ambaye aliondoka klabuni hapo jumatatu na kujiunga na  Toronto fc. 
Matri mwenye umri wa miaka 30 alifunga mabao 29 katika michezo 83 kati ya mwaka 2010 na 2013. Mapema January 2014 akapelekwa kwa mkopo Fiorentina kisha kupelekwa tena kwa mkopo klabu ya Genoa June mwaka jana. Msimu huu Matri amefunga mabao saba katika mechi kumi na sita.

KOCHA AMSIFIA DOMAYO

 
KOCHA wa Azam, Joseph Omog, amesema kiungo wake Frank Domayo ameonyesha kiwango cha juu na cha kushangaza ikiwa amecheza mechi chache tu baada ya kupona majeraha ya nyama za paja.
Domayo aliifungia Azam mabao yote mawili katika sare ya 2-2 na Zesco ya Zambia juzi Jumamosi, lakini mbali ya hilo alionyesha kiwango cha kuvutia kilichowashangaza wadau wengi wa soka waliokuwepo uwanjani hapo.
 Kiungo huyo ameanza kucheza mwezi uliopita baada ya kukaa nje kwa miezi sita tangu alipofanyiwa upasuaji Afrika Kusini.
Omog alisema hakutarajia kama Domayo angeweza kurejea katika makali yake ndani ya muda mfupi kama ilivyokuwa lakini bado anashindwa kumtumia kwa dakika zote 90 kwa hofu ya kumuumiza.
Katika hatua nyingine, kocha wa Zesco, George Lwandamina amesema
Azam wanahitaji kufanya marekebisho kidogo tu katika kikosi chao ili waweze kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa yanayowakabili.
Azam itacheza Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka huu baada ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika miaka miwili mfululizo.

HII NDIO BIASHARA ANAYOTAKA KUFUNGUA MSANII FEROUZ

 

Good news ambayo imesikika leo inamhusu msanii mkongwe Ferooz ambae amezungumzia kuhusu biashara ya mgahawa ambayo anategemea kuuzindua Jumatano ya February 04, baada ya kufanya maandalizi kwa miaka miwili mgahawa huo uko maeneo ya Darfree Market unaoitwa Hollywood Café, amesema mgahawa huo umegharimu kama milion 30 za Kitanzania na utakua ukitoa huduma za vyakula vya aina zote.

BARNABA AKARIBIA KUFUNGA NDOA

Mchumba wa Barnaba, Zebeda  amesema anafurahia  maisha yake na mpenzi wake Barnaba na kwamba watafunga ndoa hivi karibuni.bb-4ll
Zubeda amesema kuwa mipango ya ndoa imekamilika na kwa sasa wanasubiri kupanga tarehe tu.

Teyari ameshatoa pesa ya barua, na mahali kwahiyo bado kupanga tarehe ya ndoa tu alisema mama Steve. Barua alitoa mwaka jana na pesa ya mahali alitoa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana japokuwa bado haijafika lakini najisikia furaha sana na naomba Mungu ifike siku yenyewe ntajisikia furaha zaidi.

Licha ya kuisubili ndoa hiyo kwa hamu amekiri kuwa kunachangamoto nyingi ndani ya mahusiano yao.
Kuna Challenge nyingi sana mfano unaamka asubuhi unasikia simu inaita ukipokea unasikia baby,massage za mapenzi lakini mwanzo zilikuwa zina niumiza sana lakini kadri siku zinavo zidi kwenda  nikawa na zoea.
Mpaka leo hii natarajia kufunga ndoa ujue nilipambana vya kutosha ili kutetea ndoa yangu alisema Zubeda.

AY AFUNGUKA KWA NINI ALIJITOA EAST COAST TEAM

Mwanamuziki Ambwene Yesaya maarufu kama Ay ambae kwa sasa anatamba na ngoma kama Touch Me amefunguka na kuweka wazi kuwa kujitoa kwao katika kundi la East Coast Team lenye makazi yake Upanga mashariki kuwa pesa nayo ilihusika licha ya
Ay
kutofautiana na kutoelewana kimtazamo na mambo ya biashara ambayo ndiyoi yalipelekea Ay na Mwana FA kujitoa katika kundi hilo ambalo kwa sasa lipo katika mikakati ya kurudi kimuziki.
Ay alifunguka hayo jana alipotoa dakika 45 kwa mashabiki wake kumuuliza maswali kupitia Account yake ya Twitter aliyoipa jina la #ASKAY ndipo watu walitaka kujua chanzo cha wakali hao kujitoa katika kundi hilo la ECT ambalo lilikuwa likiongozwa na Gwamaka Kaihula (GK).
"Unahisi pesa ndio ilifanya EAST COAST kuvurugika?” Ofcoz ilihusika pia" lakini mbali na kutoa sababu ya pesa Ay alisema kuwa utofauti na kupishana katika mitazamo ilikuwa sababu nyingine kubwa wao kuondoka ila kuondoka kwao haikuwa na maana East Coast Team kuvunjika maana lilikuwa ni kundi na kulikuwa na watu wengi hivyo kundi kama kundi liliendela kuwepo ili hali wao walijitoa.
"kutoelewana kimtazamo na mambo Ya Biashara yalifanya tuondoke mimi na FA,ila si kama kundi lilivunjika"
Lakini Ay kupitia kipengele hicho ameweka wazi kuwa kwa sasa kuna kazi wamefanya na kundi la East Coast Team na siku za karibuni itatoka lakini amesisitiza kuwa wamefanya kazi na kundi hilo kama ambavyo wasanii wengine wanavyofanya nao kazi lakini haina maana kuwa wamerudi katika kundi
#AskAy hivi ni kweli Fa na Ay mmerudi East Coast Team ? @AyTanzania” hapana ila tunafanya nao Kazi kama artists wengine na mapaka sasa tumefanya kazi nao na Kazi itatoka very soon"
Mbali na kuzungumzia kundi la East Coast lakini pia mashabiki wa Ay walitaka kujua kuhusiana na mwanamuziki Amani ambae awali alikuwa akitambulika kama shemeji na Ay amesema kuwa katika mahusiano ya kimapenzi yeye na Amani yalikwisha muda mrefu na sasa amebakia kama rafiki wa kawaida na wanaowasiliana na kusaidiana ikiwa pamoja na kushauriana.
"Shemeji yetu amani umemwaga #AskAY” miaka mingi iliyopita sasa ni marafiki wa kawaida"
Ay leo anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Zigo na pia anatarajia kuachia video mpya ya wimbo wake mwingine mpya Its going down ambao kafanya na ms triniti pamoja na l'yamia.

KOCHA SOUTHAMPTOM ATHIBITISHA KUSAJILI USIKU WA LEO

Koeman Athibitisha Kusajili Usiku Wa Leo

Meneja wa klabu ya Southampton ya nchini England Ronald Koeman, amesisitiza kufanya usajili angalau wa mchezaji mmoja kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa usiku wa kuamkia kesho.
Koeman alitoa uhakika huo jana jioni mara baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England ambapo Southampton waliaibika nyumbani baada ya kufungwa na Swansea City bao moja kwa sifuri.
Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi amesema ameona kuna haja ya kufanya hivyo kufuatia uhitaji wa mchezaji mmoja katika kikosi chake ambacho kipo kwenye mikakati mizuri ya kuwania ubingwa msimu huu.
Wachezaji wanaohusishwa na mipango ya kusajiliwa na Koeman licha ya kutolewa msisitizo wa kusajiliwa mchezaji mmoja ni kiungo kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Feyenoord Tonny Vilhena pamoja na Filip Djuricic kutoka nchini Serbia ambaye anaitumikia klabu ya Benfica ya nchini Ureno.
Sababu kubwa ya Koeman kusisitiza suala la usajili wakati saa kadhaa zikisalia kabla ya dirisha dogo kufungwa ni kutaka kuziba pengo la kiungo Jack Cork, aliyempeleka kwa mkopo Swansea City.

WALICHOSEMA TFF KUHUSU USHAHIDI WA PICHA ZA VIDEO NA MAGAZETI

 

Shirikisho la mpira nchini Tanzania (TFF) limesema kuwa kanuni haziruhusu kupata matukio ya ugomvi uwanjani kwa kutumia ushahidi wa TV, redio au magazeti.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema matukio mengi yanatokea uwanjani kwa mchezaji kufanyiwa faulo ya makusudi au bahati mbaya, lakini ni vigumu kutoa uamuzi kwa ushahidi wa kutegemea teknologia.
“Wenzetu, kwa mfano chama cha mpira cha Uingereza (FA) wanaweza kufanya hivyo na kesi nyingi zimeamuliwa kwa ushahidi wa kutegemea video kwa sababu wana media centre yao.
“TFF kwa sasa hatuna media centre yetu inayohusu masuala ya
viwanjani ikiwa na vifaa vya kisasa, kwa hiyo tunategemea ripoti kutoka kwa kamishina wa mechi akiwa kama msimamizi ikiwa refa, msaidizi wake au washika vibendera (wasaidizi wa refa) hawajaona tukio”, alisema Wambura.
“Hatuwezi kuchukua sehemu ya mkanda wa mechi kutoka television binafsi au ya taifa kutafuta ushahidi kwani kwa sababu ya teknologia wanaweza kupunguza au kuongeza kitu katika kuhariri (editing), alisema Wambura.
 
Kauli ya Wambura inakuja huku kukiwa na matukio tata kadhaa yanayotokea katika ligi kuu ya wachezaji kuumia uwanjani na mashabiki wakiona hakuna hatua stahiki.
Miongoni mwa matukio tata ni la hivi karibuni ambapo mchezaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi alizimia uwanjani Jumapili iliyopita muda mchache baada ya kufunga goli dhidi ya Azam, kwa kile kinachodhaniwa na mashabiki wa Simba alipigwa kiwiko katika shingokwa makusudi wakati wa kugombania goli na refa hakuchukua hatua kwa mhusika kwa vile hakuona.
Kwa mujibu wa mmoja wa madaktari kutoka Chama Cha Madaktari wa Michezo nchini (Tasma),wambao ndio wanatoa huduma ya kwanza uwanjani hapo, Richard Yomba, Okwi alizinduka muda mchache baade na kuelezea kuwa alihisi kupigwa kipepsi (na kiganja cha mkono) katika shingo kabla ya kuanguka.
Tukio kama hilo pia lilimkuta mchezaji Amisi Tambwe kutoka Uganda katika mechi ya ligi kuu alipodai kukabwa koo na mchezaji kutoka timu pinzani na vyanzo visivyoaminika vinadai yeye alianza ugomvi kabla ya kushambuliwa katika malipizi.