SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 19, 2015

YANGA YAPAA KILELENI LIGI KUU BARA

Na Prince Akbar, MBEYA
YANGA SC imeweka ‘kishoka’ kiti cha mbele kwenye basi la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Prisons jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Yanga SC sasa wanatimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 14, wakiwazidi kwa pointi mbili, mabingwa watetezi, Azam FC ambao jioni ya leo wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting. 
Winga Simon Msuva alifunga mabao mawili katika ushindi huo, wakati bao lingine Prisosn walijifunga wenyewe.
Lakini sifa zimuendee kiungo Mbrazil, aliyepika mabao yote matatu jioni ya leo Uwanja wa Sokoine.
Simon Msuva kulia amefunga mabao mawili

Coutinho anayecheza pembeni pande zote mbili, alipiga kona nzuri dakika ya tatu ikaunganishwa nyavuni na Msuva kabla ya kupiga shuti kali dakika ya 11 ambalo beki wa Prisons, Lugano alijifunga katika harakati za kuokoa.  
Coutinho tena, alipiga kona nzuri kumsetia Msuva kufunga bao la tatu dakika ya 62. 
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan/Rajab Zahir dk78, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite/Salum Telela dk54, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Danny Mrwanda dk66.
Prisons; Mohammed Yussuf, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, James Mwasote, Nurdin Chona, Lugano Mwangama, Jeremiah Juma, Freddy Chudu, Jacob Mwakalobo, Amir Omar na Boniface Hau.

LOGARUSIC APATA TIMU KENYA

Na Vincent Malouda, NAIROBI
KOCHA wa zamani wa Simba SC ametua Kenya mchana wa leo kwa madaha ya aina yake akiwa amevalia miwani nzito ya jua.
Mcroatia huyo ambaye aliteuliwa kocha mkuu wa klabu hiyo ya ligi kuu ya taifa la Kenya, AFC Leopards, ameshuka na ndege ya saa kumi na mbili unusu mchana kwenye uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Alipokelewa na mwenyekiti wa Leopards Allan Kasavuli na naibu katibu Profesa Asava Kadima waliyomvisha jezi ya klabu hiyo. Anatarajia kujiunga na timu ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi Yusuf Chippo kambini Mumias, magharibi mwa Kenya hivi leo jioni.
Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Zdravko Logarusic katika jezi ya AFC Leopards baada ya kuwasili Kenya
Logarusic akiwa na viongozi wa AFC Leopard waliompokea Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, Nairobi, Kenya leo

Mechi yake ya kwanza itakuwa siku ya Jumamosi dhidi ya Chemelil Sugar katika uga wa Chemelil siku ambayo ligi kuu ya taifa itakuwa iking’oa nanga licha ya mgogoro unaoendelea na Shirikisho la Soka Kenya, FKF, kuhusu idadi ya timu zitakazoshiriki ligi kuu.
 ‘Loga’, ambaye tayari mashabiki wa AFC wamefurahia kurejea kwake Kenya, pia amezifunza klabu za Ashanti Gold na King Faisal FC za Ghana pamoja na wahasidi wa Leopards, Gor Mahia.

AZAM FC YABANWA NA RUVU, SARE 0-0 MABATINI

Na Princess Asia, MLANDIZI
RUVU Shooting imewapunguza kasi mabingwa watetezi Azam FC, baada ya kuwalazimisha sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 26 baada ya kucheza mechi 14, hivyo kuangukia nafasi ya pili, Yanga SC ikipanda kileleni baada ya kufikisha pointi 28, kufuatia ushindi wao wa eo dhidi ya Prisons mjini Mbeya.
Hata hivyo, Azam FC itabidi wajilaumu wenyewe kwa sare hiyo, kwani walipata nafasi kadhaa za kufunga mabao wakashindwa kuzitumia.

Dakika ya 26 Kipre Tchetche alipata nafasi nzuri, lakini akapiga nje, kabla ya John Bocco naye kushindwa kumalizia kazi nzuri ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 35.
Bocco tena alichelewa kuifikia krosi nzuri ya beki Shomary Kapombe aliyepanda kusaidia mashambulizi. Bocco tena dakika ya 62 akashindwa kumalizia pasi ya Himid Mao.
Ruvu Shooting nao walipata nafasi mbili japokuwa hazikuwa nzuri kama za Azam FC dakika ya 37 wakati kipa Aishi Manula alipodaka shuti la Yahya Tumbo. 
Dakika ya 83 pia, shuti la Abdulrahman Abdulrahman lilipanguliwa na kipa bora chipukizi Tanzania, Aishi Manula baada ya pasi ya Tumbo. 
Kikosi cha Ruvu Shooting kilikuwa; Abdallah Abdallah, Michael Pius, Said Madega, Hamisi Kasanga, Frank Msese, Kassim Dabbi, Juma Nade/Bakari Miawi dk63, Hamisi Maulid/Justin Chagula dk63, Yahya Tumbo, Juma Nampaka na Abdulrahman Abdulramhan. 
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Said Mourad, Serge Wawa, Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo/Didier Kavumbangu dk60, John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipre Tchetche. 

YANGA SC, AZAM FC KATIKA VITA YA USUKANI LIGI KUU LEO, ATAKAYEPIGWA ATAMSOMA NAMBA MWENZAKE

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja viwili tofauti nchini.
Timu mbili zinazoongoza mbio za taji, mabingwa watetezi, Azam FC na washindi wa pili wa msimu uliopita, Yanga SC zote za Dar es Salaam, zitakuwa ugenini leo kusaka pointi.
Azam FC inayofundishwa na makocha watatu wa kigeni, Mcameroon Joseph Marius Omog, Mganda George ‘Best’ Nsimbe na Mkenya Ibrahim Shikanda watakuwa wageni wa Ruvu Shooting kilomita kadhaa baada ya kulimaliza Jiji la Dar es Salaam, huko Mlandizi mkoani Pwani.
Yanga SC watakuwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya leo
Azam FC watakuwa Uwanja wa Mabatini mjini Morogoro leo

Timu hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), inayofundishwa na Mkenya, Thom Olaba imekuwa ngumu kufungwa Uwanja wa nyumbani, Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.
Hata hivyo, Azam FC ilivuna pointi tatu na mabao matatu katika mechi za mwishoni mwa msimu uliopita kwenye Uwanja huo na leo itajaribu kufanya hivyo tena.
Kwa upande wa Yanga SC, inayofundishwa na Mholanzi Hans van der Pluijm akisaidiwa na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa wao watakuwa wageni wa Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Prisons inayofundishwa na mwalimu mkongwe nchini, David Mwamwaja pamoja na historia yake ya kutotaka kufungwa nyumbani hususan na vigogo, lakini kwa kuwa katika hatari ya kushuka, leo inatarajiwa kupambana zaidi.
Azam FC ina pointi 25 za mechi 13, sawa kabisa Yanga SC, lakini mabingwa hao watetezi wana mabao mawili zaidi katika wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa (GD).

PORTO YAPATA SARE KWA BASLE LIGI YA MABINGWA


Basle's Taulant Xhaka (left) fights for the ball against Porto winger Yacine Brahimi during the last-16 clash
Taulant Xhaka wa Basle (kushoto) akipambana na winga wa Porto, Yacine Brahimi katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika Uwanja wa Jacob Park usiku huu. Timu hizo zilitoka 1-1, Derlis Gonzalez akianza kuifungia Basle kabla ya Danilo kuisawazishia Porto kwa penalti baada ya Walter Samuel kuunawa mpira kwenye enero la hatari.
 Danilo fires home a penalty for Porto during the 1-1 draw with Basle in the first leg of their Champions League last-16 clash
 The Brazilian right back celebrates with his team-mates after netting the equaliser at St Jakob-Park on Wednesday nightLLL
 
 
 

RONALDO APIGA BAO LA 58 LIGI YA MABINGWA

REAL Madrid imebisha hodi robo Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Schalke nchini Ujerumani. 
Cristiano Ronaldo aliifungia bao la kuongoza timu ya Carlos Ancelotti dakika ya 25 kwa kichwa na kumaliza ukame wa mabao uliodumu kwa karibu saa tano upande wake. Kwa Ronaldo hilo linakuwa bao lake la 58 Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa timu yake Real Madrid.
Marcelo akaifungia Real Madrid bao la pili dakika ya 78 na kuihakikishia timu yake ushindi mzuri wa ugenini.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Marcelo, Pepe, Varane, Carvajal/Arbeloa dk81, Silva, Kroos, Isco/Illarramendi dk84, Bale, Benzema/Hernandez dk78 na Ronaldo.
Schalke: Wellenreuther, Uchida, Howedes, Matip, Nastasic, Aogo, Neustadter/Kirchoff dk56, Hoger/Meye dk81, Boateng, Choupo-Moting na Huntelaar/Platte dk32.
Cristiano Ronaldo scored his 58th Champions League goal for Real Madrid as his side earned a 2-0 win against Schalke
Cristiano Ronaldo amefunga bao lake la 58 Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa timu yake Real Madrid ikishinda 2-0 dhidi ya Schalke usiku huu
 The Portuguese forward finds himself unmarked in the Schalke penalty area before heading past goalkeeper Timon Wellenreuther
 The Madrid players join Ronaldo in celebration of the away side's opening goal in Gelsenkirchen
 

DIDIER KAVUMBANGU: MSHAMBULIAJI UNAYEHITAJI KUWA NAYE KATIKA KIKOSI

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AKIWA katikati ya msimu wake wa kwanza katika klabu ya Azam FC, tayari mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu amefikisha nusu ya mabao aliyofunga ndani ya misimu yake miwili Yanga SC.
Yanga SC ndio waliomleta Tanzania mshambuliaji huyo mrefu mwaka 2012, baada ya kuvutiwa naye kufuatia kumuona katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Dar es Salaam akiwa na klabu ya Atletico ya kwao.
Na katika mechi ya makundi akiwa na jezi ya Atletico, baada ya kuwafunga mara mbili Yanga SC, Kavumbangu ‘aliwaloga’ kabisa wana Jangwani na kuingia msituni kuisaka saini yake.
Didier Kavumbangu amefikisha mabao 14 katika mechi 27 Azam FC
Kavumbangu alifunga mabao 31 katika mechi 63 ndani ya misimu miwili Yanga SC

Hatimaye akasajiliwa kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu 2012/2013 na mwisho wa msimu akaiwezesha timu hiyo kurejesha taji la ligi hiyo kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
Yanga SC ikazidiwa kete na Azam FC msimu wa 2013/2014 katika vita ya taji la Ligi Kuu na wakati huo Kavumbangu tayari amemaliza Mkataba wake Jangwani akiwa amecheza mechi 63 na kufunga mabao 31, moja tu la penalti. 
Kwa wastani huu wa mabao unataka nini zaidi kwa mshambuliaji? Lakini ajabu Yanga SC wakazembea kumsainisha Mkataba mpya na mchezaji huyo akaibukia Azam FC ambako hadi sasa amecheza mechi 27 na kufunga mabao 14.
Mabao 14 tayari ni karibu nusu ya mabao aliyofunga Yanga SC ndani ya mechi 63 za misimu miwili- maana yake moto wa Kavumbangu unazidi kukolea.  
Mchezaji ambaye anaonekana kuwa na makali ya kutishia ufalme wa mabao wa Kavumbangu ni Mrundi mwenzake, Amissi Tambwe. 
Tambwe alifunga mabao  26 katika mechi 43 za msimu mmoja na nusu Simba SC, pia akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita na baada ya kutua Yanga SC Desemba mwaka jana, hadi sasa amecheza 10 na kufunga mabao matatu, moja la penalti.
Mjfungaji bora wa Kenya misimu miwili mfululizo iliyopita akiwa na Gor Mahia, Dan Sserunkuma baada ya kutua Simba Desemba pia, hadi sasa amefunga mabao matano katika mechi 12. 
Mfungaji bora wa zamani wa Liberia na Cyprus Kaskazini, Kpha Sherman aliyetua Yanga SC Desemba pia, amefunga mabao mawili katika mechi 12.
Winga Brian Majwega aliyesajiliwa Azam FC Desemba pia kutoka KCCA ya kwao, Uganda amecheza mechi 13 bila kufunga, lakini amekuwa mpishi mzuri wa mabao na tegemeo la timu yake mpya.
Hapa unaweza kuona Didier Kavumbangu ni aina ya mshambuliaji ambaye unapaswa kuwa naye katika timu. Ana uchu wa mabao na ni mfungaji wa uhakika, si wa kubahatisha.

KURASA ZA MWANZO ZA MAGAZETI LEO 19 FEB

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.