SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Jun 30, 2016

GUARDIOLA ANAMTAKA STAA HUYU WA BARCELONA

Na Haji balou
Kocha mpya wa Manchester City Pep Guardiola anampango wa kumsajili kipa namba moja wa Timu ya Taifa ya Chile Na Klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania Claudio Bravo.

Guardiola anataka kumsajili Bravo ambaye ameisaidia Timu yake ya  Taifa kushinda kombe la Copa America lakini pia kumpa changamota kipa namba moja wa Timu hiyo Joe Hart ambaye hajafanya vizuri katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa.

ATLETICO MADRID KUIBOMOA LIVERPOOL KWA STAA HUYU HAPA

Na Haji balou
Gazeti moja la nchini Hispania limeripoti kuwa Timu ya Atletico Madrid imeanza mazungumzo Na klabu ya Liverpool kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji wa Timu hiyo Christian Benteke.

Benteke raia wa Ubelgiji amekuwa Na wakati mgumu katika kikosi cha Liverpool mbele Daniel Sturridge Na Divock Origi.

Benteke ambaye alisajiliwa Na Liverpool kwa Ada ya Euro million 32 akitokea Aston Villa Na Liverpool wapo tayari kumuuza kwa Euro million 24 Mpaka 30.

Jun 27, 2016

HAYA NDIO MAAMUZI MAGUMU ALIYOYAFANYA LIONEL MESSI

Na Haji balou
MAUMIVU ya moyo
yamemshinikiza Mwanasoka
Bora wa Dunia, Lionel Messi
kustaafu kuichezea timu
yake ya taifa ya Argentina
baada ya jana kufungwa
katika fainali ya tatu
mfululizo ya Copa America
ndani ya miaka mitatu.

Messi si mgonjwa wa moyo,
bali ameumizwa n a kitendo
cha kukosa penalti ya
kwanza Argentina ikifungwa
kwa penalti 4-2 katika
fainali ya Copa America
Centenario baada ya sare
ya 0-0 ndani ya dakika 120.

Messi ambaye alimwaga
machozi na kilio baada ya
mechi hiyo alizungumza na
Televisheni ya Argentina
baada ya mechi na
kufafanua uamuzi wake. "Ni
hivyo. Mimi baso na timu ya
taifa,"alisema.

"Si kwangu. Hii ni fainali ya
nne. Uamuzi umefanyika,
nafikiri hivyo. [kushinda]
ndicho ninachoitaka zaidi.
Sikuja. nafikiri ni hivyo.
Hivyo ndivyo ninavyojisikia
kwa sasa, ninachofikiria. ni
maumivu makubwa,".

Jun 25, 2016

NYOTA WA UBELGIJI AKARIBIA KUSAINI ARSENAL

Na Haji balou
Baada ya kumkosa staa wa Leicester city Jamie vard kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameamua kuamishia nguvu zake kwa staa wa Everton na Timu ya taifa Ubelgiji Romelu Lukaku.

Mwandishi wa habari za michezo nchini Italy ameripoti kuwa Lukaku amekubali dili la kusaini Arsenal dili hili limekuja baada ya kumkosa staa    wa England Jamie Vard.

Kwasasa Lukaku yupo nchini Ufaransa Na Timu yake ya taifa ya Ubelgiji inayoshiriki michuano ya Euro Na ameshafunga magoli mawili katika mechi tatu walizocheza.

LIVERPOOL YAKARIBIA KUMSAJILI STAA HUYU HAPA

Na Haji balou
Timu ya Liverpool ipo tayari kutoa Euro million 30 kwa Timu ya Southampton kwaajili ya kuinasa saini ya Mshambuliaji wa Timu hiyo Sadio Mane Raia wa Senegal.

Kocha wa Liverpool Juggen kloop amekuwa akimfuatilia kwa karibu Mshambuliaji huyo tangu alipo wafunga goli mbili katika mchezo wa Ligi mwishoni mwa msimu uliopita.

Jun 22, 2016

WALICHOSEMA REAL MADRID KUHUSU ALVARO MORATA

Na Haji balou
Timu ya Real Madrid imethibitisha kuwa nampango wa kumsajili Alvaro Morata kutoka Juventus msimu huu.
Morata alijiunga na Mabingwa wa Italy Juventus mwaka 2014 akitokea Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne (4) uliogharimu Euro million 20 lakini vigogo hao wa Spain wapo tayari kutoa Euro millioni 30 ilikuinasa saini ya staa huyo.
Taarifa za kina zinasema kuwa Real Madrid imewajulisha Juventus maamuzi yao ya kumwitaji mchezaji Alvaro Morata na atajiunga katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayonolewa na Zinedine Zidane.
Kwasasa Alvaro Morata yupo kwenye michuaono ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa na amefunga magoli matatu katika mechi tatu nakuisaidia timu yake ya Hispania kuingia katika hatua ya 16 bora.


YANGA WAMEFIKIA HAPA KUHUSU HASSAN KESSY KUCHEZA MICHUANO YA CAF

Na Haji Balou
YANGA wamewaandikia
barua Simba SC kuwajulisha
kumsajili beki Hassan
Ramadhan Kessy na kuuliza
kama kuna pingamizi lolote
kutoka kwao, na wakati huo
huo nakala zimepelekwa
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) na Shirikisho la Soka
Afrika (CAF).

Yanga ilishindwa kumtumia
Kessy Jumapili katika
mchezo wake wa kwanza
wa Kundi A Kombe la
Shirikisho Afrika wakifungwa
1-0 na wenyeji MO Bejaia
nchini Algeria, baada ya
CAF kuomba barua ya
kuruhusiwa kwake kuondoka
klabu yake ya zamani,
Simba SC, ambayo
hawakuwa nayo.

Na mara baada ya mchezo
huo, Yanga imewaandika
barua mahasimu wao hao
wa jadi, ikiwa
imeambatanisha Mkataba
wa Kessy na Simba ambao
unaonyesha umemalizika
Juni 15, mwaka huu na
mchezaji huyo alikuwa
sahihi kuingia Mkataba
mpya na klabu nyingine.

Na Yanga imepanga iwapo
hadi kufika Jumatano Simba
haitakuwa na majibu yoyote
ya barua hiyo – wataomba
TFF iwasaidie
kumuidhinisha beki huyo wa
kulia kuanza kazi Jangwani,
maana yake klabu yake ya
zamani haitakuwa na
pingamizi naye.

Na iwapo Simba SC
watamuwekea pingamizi
Kessy, watapaswa kuwa na
hoja za pingamizi ambalo
litasikilizwa na Kamati ya
Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF, chini ya
Mwenyekiti wake, Wakili
Richard Sinamtwa.

Na kulingana na uzito wa
suala hilo, inatarajiwa hadi
kufika Ijumaa Kessy
atakuwa amekwishapewa
baraka za kuanza kuitumikia
Yanga.

MAYANJA AREJEA DAR KUANZA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA

Na Haji Balou
KOCHA wa Simba, Mganda
Jackson Mayanja
anatarajiwa kuwasili Juni 25
au Juni 26 na siku moja
baadaye ataanza programu
ya mazoezi ya kujiandaa na
msimu mpya.

Hayo yamesemwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia
Hans Poppe alipozungumza
na mwandishi wetu  leo kuhusu mikakati
ya usajili na maandalizi ya
msimu mpya jana mjini Dar
es Salaam.

Kapteni huyo wa zamani wa
Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), Popppe amesema
kwamba mara Mayanja
atakapowasili, wachezaji
wote wenye Mkataba na
Simba SC wakiwemo wapya
ambao wamesajiliwa hivi
karibuni wataanza mazoezi.

MZAMBIA WA YANGA APEWA JEZI YA COUTINHO

Na Haji balou
SIKU chache baada ya kusaini mkataba
wa miaka miwili ya kuichezea Yanga,
uongozi wa Yanga umemkabidhi jezi
namba saba mshambuliaji wake Mzambia,
Obrey Chirwa.

Chirwa alitua nchini wiki iliyopita akitokea
FC Platinum ya Zimbabwe aliyokuwa
anaichezea pamoja na mshambuliaji
tegemeo, Donald Ngoma.
Mzambia huyo, alisaini kuichezea Yanga
akichukua nafasi ya Mniger, Issoufou
Aboubacar aliyesitishiwa mkataba wake
wa kuendelea kukipiga Jangwani hivi
karibuni.

Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh
alisema jezi iliyobaki ni namba saba
iliyokuwa inavaliwa na Mbrazili, Andrey
Coutinho.

Jun 20, 2016

YANGA YAANZA VIBAYA KOMBE LA SHIRIKISHO

Na Haji balou
YANGA SC imeanza vibaya mechi za
Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika,
baada ya kufungwa bao 1-0 wenyeji
Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja
wa Unite Maghrebine mjini Bejaia
usiku huu.

Goli pekee la MO Bejaia alikuwa ni beki
Yassine Salhi aliyefunga bao hilo
pekee dakika ya 20, akimalizia kazi
nzuri ya mshambuliaji Ismail
Belkacemi.

Matokeo hayo yanaifanya MO Bejaia
ishike nafasi ya pili katika kundi hilo,
nyuma ya TP Mazembe ambayo
iliifunga Medeama ya Ghana 3-1
katika mchezo wa kwanza mjiji
Lubumbashi Jumapili, wakati Yanga
inashika nafasi ya tatu.

Mechi zijazo za kundi hilo, Yanga
watakuwa wenyeji wa Mazembe Dar
es Salaam na Medeama
wataikaribisha Mo Bejaia.

Jun 10, 2016

DALILI MPYA YA IBRAHIMOVIC KUHAMIA MAN UTD

Na Haji balou
Staa wa zsmani wa
klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa
Zlatan Ibrahimovich kuhusishwa kujiunga na
klabu ya Man United zimechukua sura mpya,
Zlatan anaripotiwa kukamilisha hatua ya nne ya
kujiunga na klabu ya Manchester United .

Dalili inayotajwa kuwa staa huyo yupo mbioni au
katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya
Man United zinazidi kudhihirika, baada ya
kuripotiwa tayari ametafutiwa nyumba ya kuishi
katika jiji la Manchester ambapo ndio makao
makuu au mji inapotoka klabu ya Man United.

Kwa mujibu wa nyaraka iliyopostiwa katika
websites ya Proto Group Ltd ambao ni mawakala
wa nyumba inaashiria kuwa mipango ya Zlatan
kutangazwa kujiunga na Man United ipo tayari
kutokana na mji alipotafutiwa nyumba ya kuishi,
kwani kabla ya hapo alikuwa akiishi Paris
Ufaransa .

Jun 4, 2016

IBRAHIMOVIC ATAJIUNGA NA TIMU HII ENGLAND

Na Haji balou
Sky Sport wameripoti kuwa Zlatan Ibrahimovic  atakamilisha
usajili wa kujiunga na Man United wakati
wowote kuanzia sasa ila ni kabla ya michuano
ya mataifa ya Ulaya kuanza, Sky Sport
wanaeleza kuwa kocha wa Man United Jose
Mourinho amepanga kusajili mshambuliaji
mmoja katika dirisha hili la usajili ila Zlatan
Ibrahimovic ndio chaguo lake.

Mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward na
wawakilishi wa Zlatan wanaripotiwa kuwa katika
mazungumzo ya mwisho ili kumsajili staa huyo
kwa mkataba wa mwaka mmoja, Zlatan kwa
sasa yupo na timu yake ya taifa ya Sweden
anajiandaa mchezo wao wa kwanza wa Euro
2016 dhidi ya Ireland utakaochezwa June 13.

Jun 3, 2016

ULIMWENGU HATARINI KUWAKOSA MISRI

Na Haji balou
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe ya
DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu
'Rambo' jana hakufanya mazoezi na
timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
kwa sababu ya maumivu ya mguu.

Ulimwengu baada ya kuwasili na
wachezaji wenzake Uwanja wa Taifa,
alijaribu kufanya mazoezi ya awali ya
kuamsha misuli kidogo, kabla ya
kushindwa kuendelea na kutoka nje.

Madaktari wa Taifa Stars walijaribu
kuhangaika naye kumrejesha
uwanjani, lakini hakuweza kabisa
kurudi mazoezini.

Daktari Mkuu wa Taifa Stars, Gilbert
Kigadye akasema Ulimwengu aliumia
juzi Taifa Stars na jana ameshindwa
kabisa kufanya mazoezi kwa sasa wanaangalia namna ya ya punguza maumivu.