SAMATTA ATUPIA GENK IKIUA 2-1

HII NDIO DROO KOMBE LA FA

SIMBA CHALII KESSY AONESHWA NYEKUNDU

MANARA APATA AJALI

MKENYA APIGA MBILI LIVERPOO IKIUA 4-1

Feb 18, 2015

WAYNE ROONEY AOMBA RADHI

 
Golikipa wa timu ya Preston Thorsten Stuckmann ameeleza kuwa mshambuliaji Wayne Rooney
alimuomba msamaha baada ya kuanguka katika eneo la hatari na kupata mkwaju wa penati.
Kipa huyu alimwangusha Rooney wakati mchezaji huyo akielekea kufunga bao na kusababisha penati,
Stuckmann, alisema "Rooney aliniomba msamahani na kuniambia ilikua ni nafasi yake ya kupata penati".
"Naamini tukio kama lile lingetokea kwenye goli la Manchester United toka kwa mshambuliaji wetu refa asingeweza kutupa penati sina shaka na hilo".
"Sisemi kama haikuwa penati, nachokisema hakukua na mgongano wowote"
Rooney alifunga mkwaju huo wa penati na kuipa timu yake ushindi mnono wa mabo 3-1dhidi ya Preston.

YANGA AZAM VITANI KESHO LIGI KUU BARA


Simo Msuva mchezaji wa Yanga

Vita ya kugombea usukani wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kati za Azam FC na Yanga inaendelea Alhamis.
Baada ya kushinda mechi zao za CAF nyumbani,Yanga ikiwafunga BDF XI ya Botswana (2-0)
katika kombe la Shirikisho na Azam ikiwafunga El-Merreikh ya Sudan (2-0)
katika kombe la Klabu Bingwa Afrika, timu hizo sasa zinaelekea nguvu katika mechi za
ligi, ikiwa pia ni kama sehemu ya maandalizi ya mechi zao za marudiano za
ugenini.
Yanga watasafiri hadi Botswana na Azam wataenda Khartou, Sudan wakitafuta
ushindi ili kusonga mbele baada ya Juma moja lijalo. Kuelekea mechi zao za Ligi Kuu Alhamis, kila timu
ina pointi 25,Azam ikiongoza kwa tofauti ya goli moja. Yanga itacheza na Tanzania Prisons mjini
Mbeya na Azam watacheza na Ruvu Shooting mkoa wa Pwani.
Kocha wa Yanga, Hans Pluijm ametamba kushinda, huku akikabiliwa na kibarua kigumu kingine dhidi ya Mbeya
City wikiendi hii mkoani Mbeya, kwa lengo la kuongoza ligi yenye ushindani mkubwa.
Akizungumza jana, msemaji wa Azam, Jafar Iddi amesema baada ya kuwafunga Mtibwa
Sugar 5-2 majuma mawili yaliyopita, sasa ni Azam ya Ruvu Shooting katika jitihada za kukaa mbali na Yanga katika msimamo

KOCHA REAL MADRID AMTETEA RONALDO

 
Mkufunzi wa kilabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti anaamini mchezaji nyota Christiano Ronaldo ataimarika punde tu atakapopata bao.
Mchezaji huyo wa Ureno hajafunga katika mechi zake tatu zilizopita ,na hivyobasi kuzua utata kuhusu kiwango cha mchezo wake kabla ya mechi ya kilabu bingwa Ulaya dhidi ya Schalke.
Ronaldo amekuwa akiugua jeraha la mguu,lakini kocha Ancelotti hana wasiwasi.
''Itakuwa fursa kwa yeye kupata bao wakati wa mechi dhidi ya Schalke'',alisema.
Ni kipindi cha mda mrefu kwa Ronaldo kucheza bila kufunga msimu huu licha ya yeye kupata mabao 38 katika mechi 35.

SAMATTA APATA MTOTO


Kareem Mbwana Samatta amezaliwa
Mchezaji Mbwana Samatta ameweka historia nyingine katika maisha yake baada ya kupata mtoto wa kiume wiki hii.
Hiyo inafuatia mchezaji huyo wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba SC kupata mtoto wa kiume aliyempa jina Kareem.
Mtoto huyo amezaliwa Dar es Salaam wiki iliyopita wakati baba yake akiwa kazini, Lubumbashi, yalipo makao makuu ya Tout Puissant Mazembe. 
Mbwana Ally Samatta, ukipenda muite 'Baba Kareem'

ANELKA AMPELEKA POGBA CHELSEA

KIUNGO Paul Pogba ameshauriwa na Nicolas Anelka kuhamia Chelsea au Real Madrid ikiwa ataondoka Juventus mwishoni mwa msimu huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amesaini Mkataba mpya wa mshahara wa Pauni 70,000 kwa wiki na vigogo hao wa Serie A Oktoba mwaka jana ambao utamalizika Juni 2019.
Lakini taarifa zinasema kwamba, kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Pogba anataka kuondoka.
French midfielder Pogba has been linked with some of the biggest clubs across Europe
Kiungo wa Ufaransa, Paul Pogba anatakiwa na klabu kubwa mbalimbali Ulaya
Nicolas Anelka (right) celebrates with Didier Drogba after scoring for Chelsea against Burnley in August 2009
Nicolas Anelka (kulia) akishangilia na Didier Drogba baada ya kuifungia Chelsea dhidi ya Burnley Agosti mwaka 2009

Na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Anelka, ambaye alicheza pamoja na Pogba katika mkopo wake wa miezi mitano Juventus mwaka 2013, anaamini kwamba Mfaransa huyo anapaswa kwenda Stamford Bridge au Santiago Bernabeu, kuliko kurejea Manchester United ambako alikaa kwa miaka mitatu.
"Mtazamo wangu ni Chelsea, ambao hakika wana wachezaji wakubwa na nguvu ya kifedha ya [Roman] Abramovich au Real Madrid, ambao ni moja ya klabu kubwa duniani - ikiwa si kubwa kabisa.
"Na ninaweza kuona yeye anafanya vizuri huko, pamoja na staili yake ya uchezaji na kocha wa huko, Carlo Ancelotti atapata mengi kutoka kwake. Kichwani mwake, Paul atakuwa tayari anafahamu klabu anayotaka kuchezea,"amesema Anelka.

KOPUNOVIC AMTAJA KIONGOZI ANAYE MPANGIA TIMU SIMBA

Na Saleh Ally
TAKRIBANI wiki moja sasa imepita baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic kuvunja ukimya na kusema kitu ambacho kitakuwa ni mapinduzi makubwa kwenye soka katika klabu hiyo.

Kopunovic, raia wa Serbia, ameamua kumtaja kiongozi ambaye amekuwa akimpangia timu, kiongozi aliyekuwa akimlazimisha hata mfumo wa uchezaji anaotakiwa kuutumia!
Kocha huyo Mserbia amemtaja kiongozi huyo mbele ya viongozi wengine wa Simba, akieleza namna ambavyo amekuwa akimsisitiza aina ya wachezaji wanaotakiwa kutumika na ambao amekuwa haamini kama wanatakiwa kucheza katika kikosi cha kwanza.
Achana na kucheza, Kopunovic alieleza namna kiongozi huyo alivyokuwa akimlazimisha angalau kutumia mfumo wa 4-4-2 au vinginevyo, kitu ambacho ni cha ajabu kabisa.
Simba na kundi zima la Friends of Simba (Fos), wamekuwa katika lawama na kashfa muda mrefu, kwamba wanahusika katika kuwapangia makocha timu wanapokuwa Simba.
Baadhi ya viongozi wa Fos, wamekuwa wakilikanusha jambo hilo kwa nguvu na kusema makocha wako huru kupanga wachezaji au kutumia mifumo wanayotaka.
Wamekuwa wakisisitiza kwamba wao wanaweza kutoa ushauri, hasa wanapoona mambo yanakwenda mlama. Jambo ambalo linaweza kufanywa hata Ulaya au kwingineko.
Inawezekana kabisa mtindo wa kuwapangia makocha vikosi au kuwalazimisha watumie mfumo fulani, umekuwa ukiendelea muda mrefu bila ya wengine kujua.

Nakumbuka wakati Kocha Patrick Phiri anakaribia kuondoka baada ya Simba kumtupia virago, nilimhoji kutaka kujua kama alikumbana na tatizo hilo, akakataa katakata.
Sioni ajabu kwa Phiri kukataa kutokana na namna mwili wake ulivyoumbwa. Mtu mkimya, msiri, asiyependa kuwaumbua watu na mwenye huruma sana. Kweli binadamu tunatofautiana na Mzambia huyo ndivyo alivyo.
Pia inawezekana na makocha kadhaa waliopita hapo awali wapo hivyo, ingawa tuliona Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Abdallah Kibadeni waliwahi kueleza kero walizokutana nazo, ingawa ilionekana hatujawaamini sana kwa kuwa ni wazalendo!

Sasa Kopunovic ameweka mambo hadharani, amekuwa jasiri kutokana na kuona namna kiongozi huyo anavyofanya mambo ya kizamani, nje ya weledi kumlazimisha au kumuonyesha kazi yake inafanywa vipi.
Inaonyesha tabia ya kiongozi huyo haijaanza leo na sasa amejulikana. Ninachohoji, vipi viongozi wa Simba wanashindwa kumuweka hadharani ili kujisafisha na kashfa hiyo mbaya iliyowaandama miaka nenda rudi?
Wanasema za mwizi 40, huyu mtu amepatikana na huu ndiyo ulikuwa wakati mwafaka wa kumuweka hadharani kila mmoja ajue upuuzi aliokuwa akiufanya.
Kama kiongozi anawapangia makocha timu, halafu mashabiki wanapiga kelele kulazimisha eti Kocha Msaidizi, Selemani Matola ndiyo tatizo, basi huu ndiyo wakati mwafaka wa kuweka mambo hadharani.
Atajwe, kukaa kimya ni kuficha maradhi ambayo mwisho, Simba wataumbuliwa na kifo. Kiongozi wa namna hiyo hawafai na wala hapaswi kufichwa.
Pia ningependa kuweka angalizo, Kopunovic ni kocha na amekuwa wazi, amefanya jambo jema kwa Simba na soka la Tanzania, sasa asionekane adui na kiongozi huyo kuanza kumpangia njama za kutaka kuonekana hafai.
Viongozi wote wa soka wanaofanya kama alivyofanya huyo kiongozi wa Simba hawafai na hawapaswi kufumbiwa macho kwa kuwa wanachangia kurudisha nyuma mpira wetu.
Kiongozi anayeona anajua zaidi ya kocha, basi akakae kwenye benchi. Najua akipatikana atasema alikuwa anatoa maoni, lakini hadi kufikia kocha kusema, hauoni ni tatizo?
Maana yake hata Phiri alikuwa katika wakati mgumu, huenda alishindwa tu kusema. Bado inaonyesha hata makocha wengi waliopita walikutana na tatizo kubwa la kiongozi huyo anayejidai ana uwezo mkubwa kuliko kocha.
Juhudi zimefanyika, lakini inaonekana Simba wanafanya siri kubwa katika jambo hilo. Hawataki kumtaja, wanadai wanataka kuvuruga umoja na hata Kopunovic amekuwa hataki kulizungumzia.
Ila siku itafika, Simba wakiendelea kukaa kimya nitamsaka na kumuweka hadharani ili kukomesha viongozi kama yeye wenye tabia mbaya na zinazolenga kuumaliza kabisa mpira wa Tanzania na mwisho yakitokea matatizo, wanaangushiwa makocha kama ilivyokuwa kwa Phiri au tulivyoona kwa Matola halafu kiongozi husika anakaa kimya na ikiwezekana anakuwa kati ya wale wanaotangaza kuondolewa kwa kocha. Ujinga kabisa.

ALIYE TEMWA SIMBA APATA TIMU RWANDA


Kiungo wa zamani wa Simba, Mrundi, Pierre Kwizera, amebamba dili baada ya kufanikiwa kujiunga na timu ya Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda.

Kiungo huyo ambaye aliichezea Simba kabla ya kufungashiwa virago sambamba na ‘ndugu yake’, Amissi Tambwe, amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu, lakini kama uwezo wake ‘utawakuna’ mabosi wake, ataongezewa mkataba.
Akizungumza kutoka jijini Kigali, Rwanda, kiungo huyo alisema kuwa anafurahia maisha mapya ndani ya klabu hiyo inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
“Ninamshukuru Mungu nimepata timu, nipo na Rayon Sports ya Kigali. Wamenipokea vizuri na ninafurahi kuwa hapa, wikiendi walikuwa Cameroon kucheza mashindano ya Caf.

“Simba bado hawajanilipa fedha zangu mpaka sasa, lakini akili yangu kwanza ninaielekeza katika kuisaidia timu yangu mpya, baadaye ndiyo nitaanza kufuatilia kuhusu malipo yangu,” alieleza Kwizera ambaye alikuwa Mchezaji Bora wa Ligi ya Ivory Coast msimu wa 2013/2014.

ANGALIA TAKWIMU ZA USHINDANI KATI YA RINALDO NA MESSI

Na Saleh Ally
KIUNGO Said Ndemla wa Simba na Simon Msuva wa Yanga ni kati ya Watanzania wanaofanya vizuri katika soka kipindi hiki.


Mwendo wao umekuwa mzuri ingawa si rahisi kujua kipimo chao ni nani hasa. Kwamba wanataka kumfikia au kushindana na nani wanayetaka kumpita.

Kushindana na mtu ni sahihi kwa lengo la kufanikiwa. 
Ushindani wa Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona, uko wazi na hauhitaji mtu kuutafsiri au kutangaza.

Si rahisi kusema Ronaldo na Messi wanalala usingizi wa pono kutokana na ushindani mkubwa ulio mbele yao, ushindani binafsi, wa klabu na wa dunia nzima.

Wana kila kitu kwa maana ya kipato bora, lakini kila mmoja hana amani na ndiyo maana juhudi zao hazijawahi kukoma na leo huyu yuko juu, kesho mwingine.

Sasa Messi anaonekana kukwea kileleni kwa mambo kiufundi hali ambayo bila shaka inamfanya Ronaldo asiwe na amani au usingizi wa kutosha.

Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani wachezaji wakubwa wenye uwezo wa juu ambavyo wamekuwa wakifanya kila linalowezekana ili kung’ara.

Ushindani wa Messi na Ronaldo, unawasaidia wote wawili lakini ni msaada mkubwa kwa Barcelona na Real Madrid kuendelea kufanya vizuri. Je, Msuva na Ndemla nao wana presha za namna hiyo?

Inawezekana ikawepo lakini kwa kiwango cha chini, lakini kama hakuna kabisa, basi ni tatizo maana yake ni sawa na mwenyewe kushindana na mwenyewe na haiwezi kuwa sawasawa na badala yake ushindani wa Messi na Ronaldo unaweza kuchukuliwa kama ushindani wenye shule hata hapa nyumbani Tanzania. 

Angalia takwimu zao na bado wanaendelea kuchukuana.
MABAO
Cristiano:
Amefunga mabao 36 katika mashindano yote. Kati ya hayo, 28 katika La Liga, matano Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mawili mechi ya Super Cup na moja Copa del Rey.
Messi:
Ametupia mabao 37 katika mashindano yote. Mara  26 katika La Liga, nane katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na matatu Copa del Rey.
PASI ZA MWISHO
Cristiano:
Katika pasi zilizozaa mabao, Mreno huyo ametoa tisa kwa wenzake.
Messi:
Muargentina huyo ndiye anaongoza kwa pasi zilizozaa mabao, amegawa 12.

UMBALI
Cristiano:
Kila mmoja amekimbia kiasi cha juu uwanjani katika kila mechi aliyocheza. Ronaldo ameweza kukimbia kilomita 8.38 kwa mechi.
Messi:
Messi ana kasi zaidi uwanjani, pia ana uwezo wa kukimbia umbali mrefu katika mechi kwani ameweza kukimbia kwa wastani wa kilomita 7.6.
HAT-TRICK
Cristiano:
Amepiga hat-trick tatu msimu huu, yaani mabao tisa katika mechi tatu. Pia katika mechi moja kati ya hizo tatu alifunga mabao manne peke yake. Mechi alizofunga hat-trick ni dhidi ya Deportivo, Athletic, Celta na Elche.

Messi:
Sasa amefikisha hat-trick nne ikiwa ni moja zaidi ya Ronaldo. Mwanzoni alianza taratibu kabla ya kubadili kasi na sasa anaongoza. Hat trick zake amefunga dhidi ya Espanyol, Deportivo, Levante na Sevilla.

BAO BORA LA LIGA
Cristiano:
Ilikuwa ni bao la kichwa katika mechi dhidi ya Deportivo, ndiyo lilikuwa bao lake bora hadi sasa msimu huu.
Messi:
Alionyesha ana kasi na maamuzi ya haraka, bao lake bora lilipatikana katika mechi dhidi ya Espanyol na likapewa sifa ya ‘best finish’.